Habari za weekend wadau,
Leo sikupanga kutoka kabisa nikaonelea nitulie tu home nimalizie mwisho-juma na familia
Basi siku ikaanza vizuti tu kifungua kinywa story nyingi kucheka furaha kama kawaida
Mambo yamebadilika muda wa lunch
Wife katengeneza pilao fresh kabisa msosi umekuja mezani kila mtu ajihudumie kiasi chake anachokitaka
Sasa binti yetu wa Kwanza yupo kidato Cha 2 shue ya bweni Longido huko na kama mnavyojua kwa Sasa shule zimefungwa so yupo likizo nyumbani mpaka January Basi nikamwambia biti yangu nichotee msosi hapo
Eti mama yake kamind ile mbaya mpaka kazira kula, nauliza tatizo ni Nini anasema kwa Nini akiwa shuleni najichotea chakula mwenyewe
Nimekasirika mno na nimeondoka kwa hasira Niko zangu bar napiga gambe Kama vile sitajakaa ninywe Tena napiga maji mpaka usiku mkubwaaa nikirudi home ni kitandani halafu alfajiri mm huyoooo kwa mishe zangu na nitafanya hivi wiki nzima sitaki stress zisizokua na maana Mimi
Eti wadau kwani kosa langu ni Nini hapo