Mke wangu alirudi kwa ex wake siku ya ndoa yangu

TAXI42

Member
Jan 13, 2023
22
37
Nimekwambia hapa hatoki mtu na kama utaniacha basi hutokuja kuoa mwanamke mwingine nife leo nife kesho,Hayo ni maneno ya mke wangu.

Ilikuwa ijumaa tulivuu tukiwa hotel ya Wanyama Sinza baada ya kutoka kwenye sherehe iliyo fanyika hapo hapo sinza ukumbi wa Mirado imekuwa ni kawaida ya watu wenye kipato cha kati wakati wa harusi kutafuta sehemu ambayo watasuza mioyo yao baada ya kupitia msoto wa huko uswahilini kwa miaka. Hutumia siku ya ndoa yao kuondoa hizo nuksi kwa kutafuta sehem nzuri yakupumzika baada ya ndoa.

Sherehe ilikuwa baabu kubwa zawadi zilikuwa nyingi majirani na marafiki zangu walinisapoti sana kufanikisha harusi hii tulipata pongezi nyingi.Hii ilitokana na msimamo wangu niliokuwa nimeuweka kuwa stokuja kuoa mpaka nifikishe miaka (30)lakn haikufika hata (29)nilikuwa tayari nimekutana na mtoto mkali.

Katika kumchallenge nikaona kidogo IQ yake na yangu zinaendana Basi nikafanya kila kitu hatimaye nikatoa mahari na kupanga siku ya harusi.

29 June nikiwa nimetulia kwenye suiti nilishona kwa Sheria NGOWI huyu huyu anayekula deal za Jezi za Yanga. Suti imenikaa imetulia kama mnavyojua sherehe zetu huwa zinapangwa kwa mda lakin kufuata huo mda ni changamoto.Wakwe wamepangiwa kuingia ukumbini saa 1 usiku lakin mpaka saa 1 hiyo inafika hakuna mtu na kama unavyojua mira na desturi zetu wakwe hawaguswi wanaingia saa 1:45usiku mda umeenda.

Nimepoa kwenye Gari V8 ya mwaka 2018 na wife amatulia upande wa pili tunaongeaa mambo yako safi kabisa.

Shetani alianza kuingilia harusi yangu baada ya DJ kupiga nyimbo ya King Crazy GK ntakufaje ambapo kila mtu alishangaa.Dj akaomba msamaha mambo yakaendeleea katikati ya harusi akaja jamaa akaninong'oneza kwamba Private room kuna mtu anakusubiri nikashangaa harusi inaendelea tena kuna mtu ananisubiri nikazuga baada ya mda nikamtarifu msimamizi wangu nikaenda naye.

Kufika private room maana haikuwa mbali nikamwambia msimamizi naomba mcheki wife ikinyanyuka niambie.Kuingia private namkuta SUZAN huyu ni EX wangu tumeaachana kama 1yrs imepita nikamliza kulikoni.Akaniambia mbona hupokei simu zangu?

Nikajibu ntapokea vipi wakati unaona shughuli inaendelea ni hicho ndio umeniitia si unajua shughuli ni yangu sitakiwi kuwa mbali.Basi alilalamika nikaona malalamiko yake hayana msingi nikaondoka zangu kurudi ukumbini lakini akaniambia Honeymoon ikiisha atanipigia kuna jambo anieleze.

Sherehe iliendelee wa kunywa walikunywa.Mambo yalikuwa bambam kama unavyojua sherehe hukusanya kila kitu na ambao ulipita nao wanakukata jicho lakin sasa ndio tayari unaaga ukapera unaenda kuuliza ukichelewa ulikuwa wapi.Kunawengine wanakukumbatia matani ya hapa na pale kama pale FRED alivyonitania kuwa wewe si ulikuwa mke wa J basi mzee baba jiandae kuliwa tena wako waiti Dah mapigo ya moyo yakaenda kasi jumlisha na wivu .Akaja mwingine ni mshikaji oya Adam wamekaa kule nyuma lakini BIA zinaishia hapa katikati fanya mambo si unajua wamejitoa sana.

Mama ambaye ni jirani huyu aliniacha hoi aliniambia wao na kikundi chao gari yao imepata break down kama nina sh.30k niwakopeshe baada ya harusi atarudisha lakin pia alisisitiza hata kama sina basi nimwambie msaidizi wangu ampe zile walizo tunza watu dah.

Harusi ilijaa mambo mengi yani hawa wadau wakilewa ni taabu kila mtu anakuja na lake lakini yote heri mambo yalienda kama tulivyo panga.

Tarehe 31 june niko bafuni wife anapokea simu nikajua mambo ya kawaida ni pongezi lakin baada ya sekunde nikasikia anapiga ukunga.Nikauliza nini tena kuna msiba? hapana GEORGE kapata ajali alikuwa amepakizwa kwenye bodaboda na ndio maana jana hakutokea.

Nikauliza G ni nani ni mtoto wa Ba mdogo na huyu ndio nilisoma naye na kuna wakati alinisaidia sana Zimbabwe tulipo kuwa tunarudi DSM aliniletea stry ambayo hata kama ni wewe ungemwambia basi twende tukamwangalie yupo Hosptal gani? akanijibu yupo Muhimbili MOI nikasema poa pale nina jamàa Dr.Faraji chapu tuu tukifika atatusaidia kwa haraka .Akasema jana tu harusi leo unahangaika na masimu wewe baki ngoja mimi niende kwa vile gari iko tinted basi hakuna kitakacho haribika basi kama tulivyo shauriwa kule kanisani kwamba mwenzio akiwa anahitaji kufanya jambo fulani mwache atimize maana mzozo huanzia hapo.

Baada kama ya lisaa hivi nikapiga simu ya WIFE ikawa haipatikani nikapiga simu ya wakwe nikawaelezea wakasema mbona sisi hatuna tarifa Duh mapiga ya moyo yakaenda kasi ikafika wakati nikajituliza labda chaji.Lakini nikikaa naona kama kunajambo halipo sawa why wazazi waseme hawana tarifa hii imekaaje nikajituliza.

Nikarudi kwa wazee kuuliza kuwa kuna tarifa zozote au niende kituo cha police wakasema ni mapemaa mno maana now ni masaa 3 yamepita tusubiri kidogo.
Nimetulia napokea simu nauliza nani SUZAN nikamuliza kulikon si ulisema utanipigia baada ya honeymoon akasema ameshindwa kuvumilia nikamwambia funguka.Taxi pls naomba kama stoeleweka liache kama lilivyo nikamliza mbona unajikanyaga nenda kwenye point akaniambia mkeo anatoka na GEORGE akakata simu.

Nilifikiria na ukitazama SUZAN ni EX wangu maneno yake sikuyatiria maanani maana nilijua nachezewa mchezo basi baada ya kama masaa 5 wife akarudi.Jambo la kwanza mbona hupokei simu kulikoni akasema chaja si unajua jana tulikuwa busy hatukuchaji ok mgonjwa anaendeleaje Hajambo wamemfunga P.O.P ok naweza mpa pole akasema wazazi wake ndio wana simu zake.

Baada ya kumaliza honeymoon tukarudi home kama mwezi hivi Simu yake ikawa ina shake AIRPLANE NA DISTURB zikawa zinajibonyeza kwa wakati mmoja ikawa hapatikani niliporudi nyumbani nikamliza ndio kaniambia simu ina shida Basi nikamwambia K/koo nina jamaa pale NIZO MATELEPHONE Hizo ndio kazi zake ntamwachia ntapitia baadaye.
Nilipo rudi jamaa akaniambia tatizo ame badilisha kioo na touch inasumbua nikamwambia gharama 50k hii kishikaji nikarudi home lakin kabla sijafika simu inaita G (kifua bega) nikasema hii sipokei atapokea mwenyewe lakin nikajiambia huyu si mke wangu nimetoa mahari why sina uhalali wa kupokea simu zake (kibabe) nikaweka sikioni.Hello baby mbona hupatikan toka jana kulikoni vipi unaendeleaje je umemaliza kuchinja (period) Dah nikakaa chini maana nilikuwa karibu na home duka la Mangi.
Mangi kuniona akacheka sana akasema yani Yanga bwana mkifungwa tu Ruvu shooting mnakaa chini hivyo je ikiwa SIMBA. Taxi Si utavua nguo wewe.

Nikamwambia Mangi bora tungefungwa nikamliza Mangi mbona nyumban kwangu sipaoni Aisee bwashee unajua umri unaenda huo unatakiwa ukatayarishe mashamba unakaribia kustafuu.Nikaendelee kupekuwa simu nilichokikuta nikajilaum why nilienda kuitengeneza KWELI MKE WANGU ANATEMBEA NA GEORGE NA SIKU MOJA BAADA YA HARUSI WALIKUTANA MOUNT LODGE.

Hii ilinikata kiasi kwamba nipo tuu wiki nipo tu ninachokifanya sikielewi naangalia HATUA ZA KUCHUKUA.
 
Nimekwambia hapa hatoki mtu na kama utaniacha basi hutokuja kuoa mwanamke mwingine nife leo nife kesho,Hayo ni maneno ya mke wangu.

Ilikuwa ijumaa tulivuu tukiwa hotel ya Wanyama sinza baada ya kutoka kwenye sherehe iliyo fanyika hapo hapo sinza ukumbi wa Mirado imekuwa ni kawaida ya watu wenye kipato cha kati wakati wa harusi kutafuta sehemu ambayo watasuza mioyo yao baada ya kupitia msoto wa huko uswahilini kwa miaka. Hutumia siku ya ndoa yao kuondoa hizo nuksi kwa kutafuta sehem nzuri yakupumzika baada ya ndoa.
Piga chini huyo..Ya nini kujipa stress?
Ni ngumu sana kumbadilisha Tabia mtu mzima aliye amua kwenda kinyume na maadili....
 
Mhh aisee huyo mukeo kiboko

Anampenda sana G
Pengine G hana uchumi wa kati na kwako/ ndoa imemleta sababu ya material things. Ndio maana kwako yupo na kwa G haondoki.

Au pengine G ana makandokando ya mkeo, ambayo yakiwekwa hadharani ni noma ndio maana mkeo anashindwa hata kukaa mbali na G. Hata kufikia kukutoroka wakati wa harusi.

Very stupid.
 
Nmesoma yote,

1.mkeo kaolewa kwasababu zingine, hajakupenda kwa dhati

2.Mapenz yake kwa huyo George
Ndo maana Yuko radhi kurisk kutoroka na kusingizia ajali ili akamkate jamaa Nyege.

3.Uyo George anakudharau sn,
Katumia mgongo wa honeymoon kukuonesha nguvu aliyonayo kwa mkeo.

4. .....
 
Nmesoma yote,

1.mkeo kaolewa kwasababu zingine, hajakupenda kwa dhati

2.Mapenz yake kwa huyo George
Ndo maana Yuko radhi kurisk kutoroka na kusingizia ajali ili akamkate jamaa Nyege.

3.Uyo George anakudharau sn,
Katumia mgongo wa honeymoon kukuonesha nguvu aliyonayo kwa mkeo.

4. .....
Hii ni aibu mkuu we na falsafa zako ungefanyaje just imagine ndo ww daaah 😭😭😭😭😭 mi imeniuma Sana japo si mimi
 
Back
Top Bottom