Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,172
- Thread starter
- #41
(d)Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano
Mahakama ya Rufani
158.-(1) Kutakuwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano,itakayojulikana kwa kifupi kama "Mahakama ya Rufani" na ambayo itakuwa na: (a) Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufani; na
(b) Majaji wengine wasiopungua kumi na saba.
(2) Majaji wa Mahakama ya Rufani watateuliwa kwa kuzingatia sifa zitakazoainishwa katika Katiba hii na uwiano wa uwakilishi wa sehemu mbili za Washirika waMuungano. (3) Sheria zitakazotungwa kwa mujibu wa Katiba za Washirika wa Muungano zitaweka masharti kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufani mbele ya Mahakama ya Rufani, nyakati na sababu za kukata rufani.
Bungeni tunasema kijinsia nusu kwa nusu sasa mahakamani mbona jinsia ni kimya? Huu ni ubaguzi wa kijinsia ulio wazi ila unaendeshwa kimyakimya.
Pili kuna uhaja wa kuweka ukomo wa idadi ya majaji ili kuzuia kuwa na ajira za shukrani.
USHAURI: Idadi ya Majaji tajwa wasipungue 20 na wasizidi 40.