Tandale One,
umeandika vyema, nashukuru kuwa katika wachangiaji wa thread hii yawezekana ni wewe wa kwanza labda pia unaweza ukabaki wa pekee ambae amehoji na kutaka ufafanuzi wa haja juu ya kuwepo kwa mgogoro huo, athari zake kwa chama,na taifa kwa ujumla, lakini pia umehoji juu ya yale niliyodhani ni ya msingi kuyajadili katika baraza kuu lililokwisha hivi karibuni na kuacha kuyajadili hayo, na kwa uhakika upi kuwa hayo hayajajadiliwa, umetaka kujua haya.,nami bila ya khiyana nitayabainisha haya kwa kina, moja baada ya jingine;
i) Nilichokieleza ni mgogoro uliokuwepo baina ya viongozi waandamizi wa bavicha na chadema, mgogoro ambao ni wa kimaslahi zaidi na umejaa UNAFSI.,,kwa kumbukumbu ya maandiko ya mwalimu nyerere katika kitabu chake alichoandika mwaka 1962.,TUJISAHIHISHE ameeleza kwa upana juu ya athari mbaya zitokanazo na unafsi na hivyo inabainisha wazi kuwa mgogoro huu ni mbaya na mpana kuliko mgogoro wa kiitikadi, kisera na kikatiba.,kwani mgogoro huu wa UNAFSI unaathiri utendaji wa chama, unaathiri utekelezaji wa sera, unasababisha kushindwa kuisimamia itikadi ya chama na mbaya zaidi unapindisha KATIBA na MAADILI ya chama, vitu ambavyo ni misingi mikubwa ya chama ambayo ikiguswa misingi hiyo chama kizima hutetereka kama ilivyo kwa chadema hivi sasa.
ii) Bigaraone.,umetaka kujua pia mwanachadema anaathirika vipi, ama taifa linaathirika vipi ama chama juu ya katiba yake, strategy zake, ideology ama mode na conducts, nitakujibu kama ifuatavyo; Katiba ya chadema inasema katika madhumuni ya Chama kuwa; Kukuza, kulinda, kuelimisha na kutetea haki za binadamu katika misingi ya Tangazo laUlimwengu la haki za Binadamu na miKataba yote ya Kimataifa inayolinda haki hizo na
inayofutilia mbali ukandamizaji wa watu katika misingi ya rangi, jinsia, ukanda, umri au
itikadi jambo hili linaloendelea katika chadema limeenda kinyume na madhumuni ya chadema kikatiba, na kwa maana ideology yake pia itaathirika kuwa "
CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki. na jambo hili linabainisha wazi kuwa kuna ukandamizaji ndani ya chadema kwa kigezo cha udini na ukanda-mind u, hayo ni kwa mujibu wa kauli ya shonza, makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa.,not just mere street virus.,ni mtu ambae anakifahamu chama kuliko unavyodhani..,pia imebainishwa kuwa katika chadema hakuna haki kwa walio chini, bali haki ni kwa wakuu wa chama hiko tu na kinachoamuliwa na wao ndio haki hata kama hakina misingi ya haki-zingatia rufaa ya chagulani ya kufukuzwa uanachama,zingatia rufaa ya madiwani wa arusha, zingatia kauli ya zitto kwenye press yake ya february akiwa kigoma,hayo yote yanatoka kwa viongozi ambao ndio hasa wanaishi katika laboratory ya Chadema na wanaijua zaidi ya mimi na wewe, wameyasema hayo wewe na mimi ni nani hata tupinge ukweli huu..???
iii) Kuhusu kuwa nilichokiandika ni fabricated forged propaganda, ambayo inawatoa watu katika hoja za msingi zihusuzo umasikini.,dah hapa naanza kupata shaka kuwa ukumaliza kuisoma thread yangu mpaka mwisho kwani hili la watu kufikiri katika mlengwa wa wafikirivyo akina fulani nilishalitolea angalizo hapa;
ANGALIZO:
Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao, ni bora kujilazimisha kufikiri hata kuliko kikomo ulichodhani unacho kwa kufanya hivyo unaweza kugundua kuwa unaweza kufikiri na kuwaza kuliko vile ulivyodhani awali.Tusiweke kando fikra na hoja zetu zenye ufasaha kwa kufuata ushabiki.
hili halina sura ya kutaka watu wasahau juu ya umasikini wao, wala halisemi kwa nia ya kuchochea mgogoro na wala si sawa kusema kuwa haya ni mambo ya kutunga na non-constructive kama ulivyoandika, bali nimeshauri kwa ukweli wa kushauri, kwa maana kwa nia ya kuiona chadema inasimama na inakuwa imara ili iwe inaikumbusha CCM juu ya makosa yao na hivyo kuichochea katika kasi ya kuleta maendeleo kwa watu na hivyo kuondoa umasikini, ama ili uone nimegusa umasikini ulitaka nianze kutaja orodha ya wezi wa EPA na kisha kuonyesha picha za madarasa mabovu na wanafunzi wanaokaa kwenye mawe kwenye madarasa mabovu ndipo uone kuwa nimedhamiria kuondoa umasikini, hivi haikuwa ni jambo jema kushauri chadema ili kuleta upinzani imara utaochochea maendeleo ya watu..??? unafikiri namna ipi wewe..?
iv) umetaka pia nikutajie makundi yaliyopo chadema, nikutajie list ya kundi la Slaa, ili uone.,unataka kuniambia kuwa bado haujaona wala hutaki kukiri kuwa Chadema kuna makundi.,hutaki kulikubali tatizo kwa maana na mtazamo huo hautaweza tatua tatizo lililopo,usiwe kama mbuni kuficha kichwa na kuacha mwili, ni kwa mawazo kama yako chadema waliacha kujadili haya kwenye baraza lao wiki iliyopita na three days ahead mtu anakuja kuyamwaga hapa JF kinyume na taratibu ni kwa kuwa hakupata nafasi ya kuyajadili hayo kwenye vikao vya chama, vikao havikumpa nafasi, wakuu wa chama wanambana na kumfanya ashindwe kuyasema huko, hivi bado hujaona kuwa hilo ni tatizo..??
kamati kuu imeshindwa na nitasema hili kokote haikutoa fursa na kuwaacha watu wajadili kwa upana wa kujadili hoja ambazo ni zenye kujenga na kubainisha mustakabali wa chama, hii ilikuwa ni hoja na ajenda ya msingi kujadiliwa lakini haikujadiliwa, na ajenda nyingine iliyokuwa skipped ni ya kuhusu maadili na rufaa za waliohisi kuonewa katika maamuzi ya chama. watu hawa wanayo haki na wanastahili kupewa nafasi kwa baraza kuwajadili kwa mara ya pili(kama walijadiliwa kwa mara ya kwanza) juu ya malalamiko yao kuhusu hukumu za kipilato zilizowapata ndani ya chama hicho.
Naweza nisieleweke na nisionekana kuwa ni mshauri mwema lakini hilo sijali sana, ila ningeridhia zaidi kama mngenielewa na kufanyia kazi ushauri wangu;
JAMII YA KISTAHARABU HUKOSOANA KWA UPENDO NA KUONYESHANA NJIA...!