WHY SLAA MUST RESIGN...! "..effect of the crowded house.."

WHY SLAA MUST RESIGN...! "..effect of the crowded house.."

ONYO - CHADEMA AIHUJUMIKI ! Kama UMECHUKUA HELA YA WATU , RUDISHA ! VINGINEVYO UTAADHIRIKA VIBAYA SANA !
 
Mkuu uwasilishaji wako wa hoja kimantiki unaweza ukaonekana sawa licha ya kwamba katikati ya hoja yako umedhihirisha kwamba uko biased na your in favour of Dk Slaa quiting his position ..kiuhalisia kwa kutumia LOGIC iwe Inductive reasoning or deductive reasoning hoja yako aishabahiani na ushauri unao utoa kwani fact in issue ziko tofauti sana.
 
hakuna cha team nani wala nini ? Kilichopo ni oparesheni kimbunga dhidi ya wasaliti , acheni kupotosha !
Sema ukweli ili ukweli ukuweke huru na mficha maradhi kifo humuumbua. Msisubiri kuumbuka fanyeni maamuzi thabiti na fanyeni maamuzi hayo sasa.
Unataka kukataa hata hili ambalo kila mmoja sasa analijua..? U are not serious.
 
Sema ukweli ili ukweli ukuweke huru na mficha maradhi kifo humuumbua. Msisubiri kuumbuka fanyeni maamuzi thabiti na fanyeni maamuzi hayo sasa.
Unataka kukataa hata hili ambalo kila mmoja sasa analijua..? U are not serious.

ni zitto vs lema , na labda nikuambie kitu , lema hana team labda kama zito anayo , hiyo shauri yake ! Bali team ya Mbowe na Slaa ni chadema , sasa wewe umedai ni team zito vs team mbowe / slaa , unamaanisha kwamba zito anapambana na chadema ? Kama ni hivyo ATASHINDWA VIBAYA SANA !
 
Kwa hali inayoendelea chadema hivi sasa ni wazi kuwa busara inamtaka Dr Wilbroad Peter Slaa kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu Mkuu kwa kuwa ni wazi kuwa matendo yake yanakipeleka chama hiko mrama na kwamba kama busara hiyo haitafuatwa upo uwezekano mkubwa chama kikamfia mikononi.
 
Hii thread imenikumbusha mbali sana nilipokuwa nakumbuka matukio yaliyopita mwaka jana..hasa yaliyowakuta chadema chama cha slaa na mbowe. Nikajikuta nimeikumbuka thread hii.
 
Hivi unajua kuna shehena kubwa ya pembe za ndovu inataka kusafirishwa kinyemela hapa bandari salama!?

Wewe watukane tu watetezi wako wakati serikali yako inapiga dili haramu!

Ukija kuamka utakuwa umeshachelewa!POLE!
 
zitto akifukuzwa


next battle will be between slaa and Mbowe...........list goes one

mbowe, slaa lazima waondoke
 
……….it was on Thursday evening, 10[SUP]th[/SUP] December in the year 1936 on 10 Downing Street, Garden Entrance, two people had been in serious conversation., one was ALBERT FREDERICK ARTHUR GEORGE-the then DUKE OF YORK who three days later came to be known as KING GEORGE VI OF THE UNITED KINGDOM and DOMINIONS OF THE BRITISH COMMONWEALTH and the other was MR. STANLEY BALDWIN-THE PRIME MINISTER OF UNITED KINGDOM who later replaced by NEVILLE CHAMBERLAIN..,

The conversion was all about the scandal that touch the Kings’ name EDWARD VIII over HIS proposed married to MRS SIMPSON.., MR BALDWIN argued…”it’s not because she is American, that is least, it’s because she is assumed to be twice divorced American and the King as a head of the church of England cannot marry a divorced woman….and Sir I real apologize to be true this, but according to Scotland yard, the King has not always possess the exclusive rights…..should his Majesty continue to ignore the advice of His government..? He must abdicate otherwise His government has no choice but to resign.., and ALBERT the DUKE poses a question; Prime Minister, do you lead the country without the government…? And MR BALDWIN responds this by question; does the King DO what he wants or he does what people expect him to do…?

Just after this conversation some minutes later KING EDWARD VIII signed the instrument of abdication to avoid HIS whole government resignation and the next day Friday 11[SUP]st [/SUP]December 1936, MR BALDWIN delivered HIS memorable speech “EFFECT OF THE CROWDED HOUSE” in which MR BALDWIN said at the end of the speech, “Where I failed, no one could have succeeded”

Historia hii inatufunza mambo mengi na muhimu hasa tukiilinganisha na matukio ya kisiasa ambayo yanaendelea nchini kwetu hivi sasa, katika vuguvugu la malumbano na kufarikiana kukubwa kulikoikumba kambi ya upinzani hususani Chadema hivi sasa ambako kunatokana na Viongozi wakuu wa Chama Hicho kugombea madaraka.

Katika kilichotokea hivi karibuni ambapo viongozi wakuu wa chama hicho wamevuana nguo hadharani na kuonyesha utovu mkubwa wa nidhamu na fedhea ya hali ya juu miongoni mwao. Lakini pia imedhihirisha kuwa viongozi hawa hawajui nini maana ya kuwa viongozi, hawajiheshimu wenyewe lakini pia hawaheshimu wengine. Ni watu waliodhihirishia umma kuwa wao ni wababaishaji ambao wanajali zaidi maslahi binafsi kuliko maslahi ya jamii ama umma.
Kupotea kwa nidhamu katika Chama hiki kunatokana na viongozi wakuu ambao wanajukumu la kusimamia nidhamu ktk chama hicho kushindwa kufanya kazi yao ipasavyo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho ambae kikatiba analo jukumu la kuhakikisha kuwa wanachama wanakuwa na nidhamu na wanafuata misingi, taratibu na kanuni za chama kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Chama.

Lakini pia, Mambo yanayotokea hivi sasa yanaonyesha wazi kushindwa kwa kamati kuu ya chama hiko katika kusimamia majukumu yake na hivyo kuruhusu mambo yanayotakiwa kujadiliwa ndani ya vikao vya Baraza hilo kushindwa kufikiwa hatma na hivyo kuyafanya mambo hayo kujadiliwa nje ya vikao, ni kwa sababu viongozi wa chama hicho kuogopa kuyajadili hayo na hivyo kuyaacha na kufanya waathirika na wanaohisi kuonewa katika chama kutafuta platform nyingine na kuyazungumza hayo. Jukumu hilo la Kamati kuu ni la kikatiba ambapo imeanishwa katika katiba ya Chadema Sura ya Tisa;
9.0 MAMBO YA JUMLA KUHUSU KATIBA NA CHAMA
9.2 Kanuni na Maadili ya Chama:

9.2.5 Kamati Kuu itatunga maadili ya kuongoza nidhamu, utii, na uwajibikaji na dhamira ya
watendaji viongozi wa Chama na wanaChama kwa ujumla. Hii ni pamoja na Maadili ya
Mwenendo katika vikao vya Chama.."


Lakini imedhihirika kuwa hata baada ya Kamati kuu la chadema kukutana hivi karibunu, kwa makusudu na maslahi binafsi waliamua ku-skip hoja za msingi ambazo zinagusa mustakabali wa chama hiko na kujisahahulisha mapungufu makubwa yaliyomo katika chama hiko.

Katika kutafuta suluhu na suluhisho la kudumu ni lazima kuangalia kiini cha tatizo hili ambalo bila ya shaka ni mbio za urais 2015 ambazo zimepelekea kuwepo kwa makundi hasimu (antagonistic pacts) yakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Hiko Dr Slaa, na Makamu wake Zitto Kabwe. Kama ilivyotokea kwa Makamba na kama ilivyotokea kwa King Edward VIII ambapo imedhihiri kuwa watu hawa wanaendeshwa na hisia binafsi na tamaa zao za madaraka na wameshindwa kuweka maslahi binafsi pembeni na hivyo kuleta makundi na sintofahamu kubwa ndani ya chama, na mitazamo ya sasa ni kuwa kulingana na ukubwa wa mgawanyiko na makundi haya, Chadema inaweza kumeguka ama kufa moja kwa moja, ili kunusuru kadhia hiyo isitokee busara inamtaka Slaa kulitathimin hili kwa kina na kufanya maamuzi magumu ya kujiuzulu nafasi yake pamoja na sekretarieti yake kwa pamoja ili kupisha uteuzi mwingine ambapo utazingatia hatari ya kuwarudisha watu ambao wataendeleza na kukuza makundi kwa maslahi binafsi. Hili linaweza kufanyika ikiwa tu Dr Slaa atakuwa tayari kuona kuwa linafanyika, kwani kujiuzulu kwake ndiko kikatiba kutakakopelekea reform kubwa kufanyika ndani ya chama, itatoa mpenyo na mwaya wa Vikao vikuu vya Chama kukutana na kujadili dharula hiyo, hivyo kupelekea jambo hili linalohusu mgogoro wa sasa kujadiliwa kwa kina na kufanyiwa maamuzi ya msingi ambayo labda yanaweza kurudisha hadhi na heshima ya Chama ambacho tayari kimeanza kuonekana cha wababaishaji, lakini pia kurudisha imani ya wananchi iliyokuwa tayari imeshuka kwa asilimia kubwa.

Nasema hii ndio suluhu pekee kwa kuwa kulingana na Katiba ya Sasa ya Chadema iliyopitishwa na Mkutano Mkuu tarehe 13/08/2006 ni vigumu na ni jambo lenye uzito kwa viongozi kama Slaa ama Zitto ama Heche ama Shonza kuweza kung’olewa katika nafasi zao kwa vikao vya kawaida vya maadili ndani ya chama kwa kuwa katiba ya Chadema inasema katika Sura ya Sita;

6.3.6 Mamlaka za Nidhamu na Uwajibishaji
(f) Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wanaweza kusimamishwa uongozi endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza Kuu watapiga kura ya siri na kutokuwa na imani na kiongozi mhusika. Baraza Kuu litakuwa na wajibu wa kuteua atakayeshika nafasi hiyo kwa muda hadi uamuzi wa mwisho kufanywa na Mkutano Mkuu.."

Katika hali ya sasa ni wazi kuwa kura itakayopigwa ni wazi itakuwa na msukumo wa makundi yaliyopo ndani ya chama hiko ambapo ni wazi kuwa aidha zitto tayari anayo idadi hiyo ya theluthi mbili ama slaa tayari anayo idadi hiyo ya theluthi mbili kati ya wajumbe wote wa mkutano mkuu na ndio maana nikasema haitakuwa suluhu kwani uamuzi wa kura hiyo utakuwa ni wa kimakundi na badala ya kujenga utabomoa zaidi kwa kuwa wale wajumbe wa kundi litakaloshindwa litaendelea na sabotage na hivyo kukwamisha utendaji makini wa chama ambao kwa sasa unahitajika sana kuelekea 2015.

Nasema haya kwa kuwa najua kuwa katiba ya Chadema inasema kuwa;

7.7.13 Kazi za Baraza Kuu zitakuwa:-
(a) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo yake katika mkutano mkuu kwa uamuzi.."

Katika hali hiyo ni wazi watu hawa tayari walikuwa wameshafanya lobbying ya kutosha kwa wajumbe wa baraza kulingana na nia yao ya kugombea Urais ambao kila mmoja kupitia wapambe ama yeye mwenyewe ameshaweka wazi kuwa 2015 ni zamu yake, Zitto ameliweka hili bayana kwa mdomo wake na Slaa kupitia midomo ya wapambe wake kama Heche.

Ni kama kwa KING EDWARD VIII ambaye alikuwa amefanya makosa makubwa kulingana na sheria za Kanisa lakini pia kwa sheria za Jumba la Kifalme ambalo ndio linasimamia Serikali ya Uingereza, kwa kuwa alitambua na alikiri makosa yake, hivyo aliamua kujiengua yeye ili anusuru Serikali yake kujiuzulu ni kama kwa Slaa na ZZK ambao wamefanya makosa makubwa kulingana na kanuni na taratibu ndani ya chama kwa kutengeneza makundi na kuvunja na kupindisha kanuni kwa maslahi binafsi, makosa ya heche kuilipwa kinyume na utaratibu, makosa ya kuminywa kwa shonza, kumiliki kadi na kuunda CHAUMA, kukuza makundi,n.k

Tofauti na KING EDWARD VIII ambae aliona hatari ya serikali yake kujiuzulu na hivyo kuvuruga Nchi ya Uingereza na hivyo kujiuzulu yeye binafsi, Slaa na ZZK hawashtushwi wala hawaoni hatari inayoikabili Chadema wanachukulia makosa yao kuwa kelele za Chura ambazo haziwazuii wao kunywa maji yao (URAIS 2015) na ku-neglect janga la kukizamisha chama na kukimega. Busara lazima itumike na hakuna namna isipokuwa SLAA ajiuzulu, ili ZZK na wengineo automatically wawe wameachia ngazi.

It's the effect of crowded house.,ni wazi kuwa Nape alikuwa sahihi pale alipowataka Chadema wajitathmini katika wanachama na viongozi ambao mara nyingi Nape aliwaita "..Oil Chafu.." kwani Nape alitambua madhara ya oil chafu katika utendaji na ndio maana aliwaonya Chadema lakini hawakuiona hatari hiyo mpaka hivi sasa.,surely the Chadema house is too much crowded na lazima wapunguze ama wamwage kabisa oil chafu yote ili safari yao iwe ya salama na amani.

USALITI;
Usaliti ni neno pana sana...,
Lina madhara mengi sana...,
Hujuma hukwamisha mambo mengi sana...,
Tamaa huzaa usaliti...,
Usaliti huleta maumivu kwa waliokuamini...!

ANGALIZO:

Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao, ni bora kujilazimisha kufikiri hata kuliko kikomo ulichodhani unacho kwa kufanya hivyo unaweza kugundua kuwa unaweza kufikiri na kuwaza kuliko vile ulivyodhani awali.Tusiweke kando fikra na hoja zetu zenye ufasaha kwa kufuata ushabiki.

JAMII YA KISTAHARABU HUKOSOANA KWA UPENDO NA KUONYESHANA NJIA...!

Natamani chadema wangelisoma habari hii na kuielewa na kuifanyia kazi kuliko hatua hii waliyofikia kwa sasa..,ni aibu.
 
zitto akifukuzwa


next battle will be between slaa and Mbowe...........list goes one

mbowe, slaa lazima waondoke

Dhambi ya ubaguzi ni sawa na dhambi ya kula nyama ya mtu..,ukianza kuila hautaacha,,wameanza kula nyama na wataendelea milele daima mpaka wakose watu wa kuwala ndani ya chama chao na watatafunana wenyewe kwa wenyewe...!
 
Hivi unajua kuna shehena kubwa ya pembe za ndovu inataka kusafirishwa kinyemela hapa bandari salama!?

Wewe watukane tu watetezi wako wakati serikali yako inapiga dili haramu!

Ukija kuamka utakuwa umeshachelewa!POLE!

watetezi..?????
 
Kwa hali inayoendelea chadema hivi sasa ni wazi kuwa busara inamtaka Dr Wilbroad Peter Slaa kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu Mkuu kwa kuwa ni wazi kuwa matendo yake yanakipeleka chama hiko mrama na kwamba kama busara hiyo haitafuatwa upo uwezekano mkubwa chama kikamfia mikononi.
No way hatupokei ushauri toka Lumumba No and Big Noooooooo. Mnataka malengo yenu yatimie ee ss hapo si itakuwa mission accomplished! Nasema tena NO!
 
Back
Top Bottom