WHY SLAA MUST RESIGN...! "..effect of the crowded house.."

WHY SLAA MUST RESIGN...! "..effect of the crowded house.."

CCM jengeni chama chenu kinakufa kabisa acheni siasa za kijinga....
Hakuna anaewasikiliza ....kilo ya sembe Tsh ngapi? mchele Ths ngapi umeme .nk....nyie mko madarakani pigeni kazi!
 
Duh hivi Dr SLAA ana nini mpaka watu wanatetemeka hivi?
 
Tatizo letu kubwa chadema nn kujifanya hatukubali mapungufu na kukosolewa
no one is perfect
slaa si mungu kama tunataka kuwa mfano bora kwa yote yanayo mkuta slaa lazima awajbke na hyo utamuacha salama zaid kuliko wakat mwingine wowote ata kama atakuja gombea tena

slaa lazima awajibe namuunga mkono bwana tandale
 
Mgogoro upi huo ni huu wa kupikwa na CCM baada ya kuona wananchi wamekosa imani nayo au ni upi huo?
Ni mtanzania gani asiyejua mbinu chafu na za zamani zinazotumiwa na CCM kwa yeyote wanayemuona kuwa ni tishio kumpaka matope ili aonekane hafai?

Anzia kwa wakati ule Augustino Mrema, CUF, CDM kuwa ni chama cha wachaga, lakini baada ya kuamka usingizini na kukuta chama kimeenea na kukubalika nchi nzima, sasa wamekuja na gia ya kumchafua Dr. Slaa ambaye wanamhofia kwa kutokuwa na suluhu na wala rushwa na mafisadi.

Mgogoro mkubwa uko kati ya wananchi walioamka toka usingizi wa kudanganywa kila siku kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani wakati wachache wanaendelea kugawana raslimali za nchi, na watawala wanaokumbatia rushwa na ufisadi uliokithiri. Acha kupagawa kwa mageuzi yanayokuja kwa kasi nchi hii dhidi ya utawala dhalimu.

Yako wapi mabilioni yaliyowekwa Uswiss kutokana na rushwa, wako wapi wanyama wetu, madini yetu na misitu yetu na ardhi yetu?. Mbona huoji hayo kama unaitakia mema nchi hii?

Wako wapi usalama wa Taifa waliopaswa kuhakikisha raslimali za nchi hii zinalindwa lakini badala yake wamekuwa ni taasisi ya kuhakikisha watawala wanaendelea kutawala kwa gharama yoyote ile?. Ni vipi mwananchi raia tu wa kawaida aambiwe ataje majina ya mafisadi wakati vyombo vya dola ambavyo leo vinatanua kutokana na kodi zetu vipo na vinajua kila kinachoendelea ktk nchi hii?

Unapaswa kuwa mwangalifu ktk hoja zako, zisizidishe hasira kwa watanzania waliokata tamaa na kuvumilia kwa muda mrefu. Nchi inahitaji kuwa na kiongozi ambaye yuko tayari kuifia nchi ili iwe na usawa ktk mgawanyo wa rasilimali za nchi na isonge mbele, na aone matatizo ya wananchi kama mzigo wake, hata kama itabidi afe maskini.

Mfano wa marehemu Sokoine. Na usitegemee hata siku moja kuwa mtu wa aina hiyo atakubalika ktk mfumo wa utawala wa sasa.
 
Wabongo huwa hawataki kabisa kusikia kitu inaitwa RESIGNATION
 
Binafsi nadhani jamaa ana points, na sidhani kama ni kundi la kina Tuntemeke hata kama ni mmojawapo lakini amekuja vizuri! Lakini suala la kujiuzulu Slaa siafiki hata kidogo, ila nachojua kwa namna yoyote ile hizi scandal zitaharibu staha ya chama!

Mimi concern yangu ni kwa Watz, wengi wao si wa kuchambua mambo kwa kina, hivyo haya mambo yanayoendelea hatujui jinsi gani yanavyowagawanya! Watz ninaomaanisha si wale ambao kila siku wako humu JF, bado kuna asilimia kubwa dunia kwao sio kijiji kama ilivyo sasa! Binafsi nina imani V, wanajua kinachoendelea lakini wana subira ya kufanya maamuzi kwa wakati muafaka, lakini nina imani wamepima umuhimu wa maamuzi hayo sasa na athari zake, ama kufanya maamuzi hayo baadae na athari zake hii ndio imani yangu! Lakini huwa nawaza kuwa, ili kuchukua nchi tunahitaji hata hzo kura za hao wengine, ambao wana excuse kibao utadhani kwenye nyumba yao ni wasafi kihivyo!

Uchaguzi uliopita, niliwahi kumsikia Mzee mmoja wa makamo akimuuliza mtu, " Hivi kwa mfano V wakichukua nchi watatosha kweli kwenye baraza la mawaziri"....Yaani bado kuna kazi ya kuwaaminisha watu kwamba na jinsi gani wana nia ya dhati kuchukua nchi, siasa ni game moja mbaya sana unawezwa kupotezwa sekunde tuuu! Yes cc tunajua kuna watu wanatumiwa, lakini unaweza kuona bado kuna watu wanawasapoti hao wanaotumiwa, na hwa lazima washughulikiwe ili wasieneze hizo sumu kwa watu ambao wakisikia kitu basi wanakibeba kama kilivyo! Bado naamini Slaa anastahili, lakini lazima Chama kishughulikie hawa wapuuzi mapema kwa maslahi wa Watz wengi ambao nina mashaka nao kwenye uelewa wao!

Mimi Nawaza hivyo,
 
Maamuzi ya Lumumba tunawaachia Lumumba wenye IQ ya mmbu. Ya Lema hayajaisha yanaendelea ya Dr. Slaa. Ni ushahidi wa kuweweseka wa jalalani TANDALE
 
Wabongo huwa hawataki kabisa kusikia kitu inaitwa RESIGNATION

Kweli mzee pamoja na mauaji ya raia Mwema, Chagonja, Pinda, Kamuhanda list ndefu hakuna mwenye wazo hilo. Ila kwa kuwa ni Chadema tutayasikia ya kila aina.
 
Tatizo letu kubwa chadema nn kujifanya hatukubali mapungufu na kukosolewa
no one is perfect
slaa si mungu kama tunataka kuwa mfano bora kwa yote yanayo mkuta slaa lazima awajbke na hyo utamuacha salama zaid kuliko wakat mwingine wowote ata kama atakuja gombea tena

slaa lazima awajibe namuunga mkono bwana tandale

CHADEMA wanafahamika na pumba zinajulikana,acha kupiga mayowe mtoto.Slaa mziki mzito na mtaucheza hivyohivyo hata kwa viboko
 
If he resignes do you expect the party to survive in next coming election?Who is going to push it to the next step.Dr,Slaa is a giant man,learned properly knows to read the future signs has majority acceptance too.If he has to resign the will be at the stake.completely is going to have a solvent death.The can not resolve the issues by focring somebody to resign rather than sitting together,looking the root cause of the problems then come to the resolution.One party i dont like to mention the name it has a slogan (kuvuana magamba) tell me know whtat is going on now.Has it succeded to uproot the purpates and how many are they?What i can see people are discussing siple mind rather great issues.deal with great issues and siple things that have small consequencies.
 
Nimegundua, members wenye uwezo wa kusoma threads za kiphilosofia ni wachache san. TandaleOne amewawekea mifano hai, amewawekea katiba ya Chadema, watu hawasomi na kuchambua memba wengi wanaishia kutukana na kubeza kisa tuu kashauri Dr. Slaa ajiuzulu!.

Niliwahi kusema humu, Chadema ina wanachama, wafuasi na washabiki ambao wao wanaabudu watu!. Kuna watu wao wanawaona kama ndio Mungu, ukiwataja tuu, wanakushukia as if umetenda dhambi ya mauti!. Hawa miungu watu wa Chadema, hata wafanye makosa vipi,kwao wao ni malaika, na wataendelea kuabudiwa huku Chadema kikiendelea kuzama kwenye tope zito la usaliti na kutokuaminiana!.

Haya yote yanayoendelea ni tisa, kumi ni mgombea wa 2015!. Msipompitisha mgombea mwenye uwezo, anayekubalika na wengi nje ya Chadema, then, jiandaeni tuu kuendelea kuwa ni chama cha upinzani cha kudumu!, 2015 ni CCM Tena!.
P.
 
Hivi TandaleOne jeshi la adui linapokuwa na 'silaha mbovu', kwa nini tuhangaike kuwaambia silaha zao ni mbovu? Kwa nini tusiwaache waendelee na silaha mbovu ili tushinde vita?

Tafakari.
 
Mtasema mengi sana wakati huu kuondoa fikra zetu katika hisia za kuleta mabadiliko. Hata hivyo bidii hizo hazitafua dafu mpaka lengo letu la kujikomboa likamilike. Baada ya hapo kama kuna mtu mwenye agenda yake ajitokeze na tutamsikiliza.
 
Mbona huyo wenu ambaye meli zake zilizokamatwa na meno ya tembo haja achia ngazi au ndio anatekeleza hizo sera zenu za wizi

Two wrongs do not make a right. Ufisadi wa CCM na kutowajibika hauwapi CHADEMA haki ya kufisadi na kutowajibika kwakuwa kufanya hivyo kutafanya wasiwe na tofauti baina yao na CCM
 
Tatizo letu kubwa chadema nn kujifanya hatukubali mapungufu na kukosolewa
no one is perfect
slaa si mungu kama tunataka kuwa mfano bora kwa yote yanayo mkuta slaa lazima awajbke na hyo utamuacha salama zaid kuliko wakat mwingine wowote ata kama atakuja gombea tena

slaa lazima awajibe namuunga mkono bwana tandale

Naungana nawe inaniuma sana kuona wanachama wa chadema hawataki kuona mapungufu ya chama na kukemea na wao ndiyo watasababisha kuharibika kwa cham. Mtu yoyote anayejaribu kupingana nao basi wanamwita gamba. Kumbuka viongozi wa chadema nao ni binadamu wanakosea na wanatakiwa kukosolewa kwa maendeleo ya chama.
Ukikosoa utasikia mbona ccm imefanya vile. Two wrongs do not make up a right
 
Back
Top Bottom