winner forever
JF-Expert Member
- Mar 6, 2012
- 1,094
- 269
Hujanishawishi,another pro-masalia,
Kwanza mimi sio mwanachama wa CHADEMA ni mtanzania mwenye kiu ya mabadiriko, Pili Alichokisema mnyika ni kwamba uchunguzi wa shutuma na tuhuma zinazotolewa umeanza kufanywa, uchunguzi ukikamilika unaweza kuja na matokeo ya kuwapo kwa makundi yote mawili, au moja au hakuna makundi au kuja na mambo mengine kabisa kama tatizo halisi.
Wewe umekwishakutoa hukumu tayari. wewe ni kama mungu kabisa wewe
Mgogoro upi huo ni huu wa kupikwa na CCM baada ya kuona wananchi wamekosa imani nayo au ni upi huo?
Ni mtanzania gani asiyejua mbinu chafu na za zamani zinazotumiwa na CCM kwa yeyote wanayemuona kuwa ni tishio kumpaka matope ili aonekane hafai?
Anzia kwa wakati ule Augustino Mrema, CUF, CDM kuwa ni chama cha wachaga, lakini baada ya kuamka usingizini na kukuta chama kimeenea na kukubalika nchi nzima, sasa wamekuja na gia ya kumchafua Dr. Slaa ambaye wanamhofia kwa kutokuwa na suluhu na wala rushwa na mafisadi.
Mgogoro mkubwa uko kati ya wananchi walioamka toka usingizi wa kudanganywa kila siku kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani wakati wachache wanaendelea kugawana raslimali za nchi, na watawala wanaokumbatia rushwa na ufisadi uliokithiri. Acha kupagawa kwa mageuzi yanayokuja kwa kasi nchi hii dhidi ya utawala dhalimu.
Yako wapi mabilioni yaliyowekwa Uswiss kutokana na rushwa, wako wapi wanyama wetu, madini yetu na misitu yetu na ardhi yetu?. Mbona huoji hayo kama unaitakia mema nchi hii?
Wako wapi usalama wa Taifa waliopaswa kuhakikisha raslimali za nchi hii zinalindwa lakini badala yake wamekuwa ni taasisi ya kuhakikisha watawala wanaendelea kutawala kwa gharama yoyote ile?. Ni vipi mwananchi raia tu wa kawaida aambiwe ataje majina ya mafisadi wakati vyombo vya dola ambavyo leo vinatanua kutokana na kodi zetu vipo na vinajua kila kinachoendelea ktk nchi hii?
Unapaswa kuwa mwangalifu ktk hoja zako, zisizidishe hasira kwa watanzania waliokata tamaa na kuvumilia kwa muda mrefu. Nchi inahitaji kuwa na kiongozi ambaye yuko tayari kuifia nchi ili iwe na usawa ktk mgawanyo wa rasilimali za nchi na isonge mbele, na aone matatizo ya wananchi kama mzigo wake, hata kama itabidi afe maskini.
Mfano wa marehemu Sokoine. Na usitegemee hata siku moja kuwa mtu wa aina hiyo atakubalika ktk mfumo wa utawala wa sasa.
Wabongo huwa hawataki kabisa kusikia kitu inaitwa RESIGNATION
Mtasema mengi sana wakati huu kuondoa fikra zetu katika hisia za kuleta mabadiliko. Hata hivyo bidii hizo hazitafua dafu mpaka lengo letu la kujikomboa likamilike. Baada ya hapo kama kuna mtu mwenye agenda yake ajitokeze na tutamsikiliza.
Slaa akiresign itakua pigo kubwa sana kwa chadema kwa wakati huu wa kukijenga chama. Na itakua ni ushindi kwa chama tawala.
Imani hii haitawaponya kamwe...!Heko TandaleOne a.k.a. Nape!
Lunyungu,hawa watu wanastahili kuitwa wapumbavu.Mara Slaa ni pandikizi lao,mara anataka uraisi 2015,hivi ni wapi Slaa alipotamka anataka hilo? Hata uchaguzi uliopita tuliona jinsi CDM walivyotumia nguvu ya ziada kumshawishi Slaa kusimama kugombea. Ni upuuzi kumsemea adui yako eti fulani ni mzuri zaidi ya yule kupambana na mimi.huyo wanayemuona mzuri sii wamchukue!Uharo mwingine wa kukaribisha Xmas .Bia za bure hizi na bahasha za Kinana .Waacheni Chadema na mambo yao wewe si mwanachadema wala shabiki na mpenzi ya nini kuumia .Jipangeni kuua tembo kaka