SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,836
- 1,846
Mwishoni mwa mwaka 2012 hapa JF liliwepo bandiko maarufu lililotambulishwa na kichwa cha habari "why slaa must resign" https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-must-resign-effect-of-the-crowded-house.html
Katika bandiko hilo, mwandishi wake alielezea juu ya ulegevu na kuyumba kwa uongozi wa juu wa chadema chini ya Dr Slaa kama mtendaji mkuu na kwamba ili kunusuru hali hiyo ambayo mwandishi huyo alitabiri kuwa itakimaliza Chama hicho kwani kitapoteza wanachama lakini pia kitapoteza imani ya watanzania.,mwandishi alipendekeza Dr Slaa ajiuzulu.
Kama ilivyo kawaida ya sikio la kufa, viongozi wa juu wa Chadema walipingana na ushauri huo na kuendelea kubaki vin'ang'anizi katika nafasi zao walizozishikilia na hatimae leo tumeona yanayotokea, watu maelfu kwa maelfu wamekuwa wakiondoka chadema tena watu wenye nafasi nyeti na wenye influence kubwa kwa jamii. Leo lugha ya "KUJIUZULU'' imekuwa ni lugha ya kawaida kwa wanachadema wanaoujua ukweli na uhalisia wa Chama hicho kila uchao.
Lakini mwandishi aliposimamia hoja ya wimbi la watu ambalo aliwaita "oil Chafu" hasa baada ya Ally Bananga na James Ole Milya kujiunga na chama hicho, hoja hiyo sasa ni mfu. Hoja kuwa chadema kimepoteza mwelekeo kwa sababu watu ni wengi ni hoja mfu, hivi sasa Chama hicho kimebakiwa na wanachama wachache ambao ukiwajaza kwenye darasa moja la shule ya msingi ya kata wanatosha. Hoja ya uwingi sio hoja na kwa maana hiyo Dr Slaa aachwe akiongoze Chama, kwani hivi sasa watu wamepungua hivyo atafanya kazi zake za management vizuri na kwa urahisi.
Dr Slaa alisikika kuwa Chama hakijakomaa hivyo hakiwezi kufanya uchaguzi wake wa ndani ila kuanza kwa zoezi la uchaguzi ndani ya Chama hicho ni dalili kuwa Chama iko sasa kimekomaa na kwamba kinajiandaa kuchukua nchi 2015.
KILA LA KHEIR DR SLAA..,IKULU INAKUSUBIRI 2015.
KUNA POST MMU mchumba wako anaomba ushauri huko, anadai ameshajutia uamuzi wake so anaomba wadau wamshauri.....