Why Slaa must not resign, CHADEMA house is no longer crowded!

Why Slaa must not resign, CHADEMA house is no longer crowded!

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,609
Mwishoni mwa mwaka 2012 hapa JF liliwepo bandiko maarufu lililotambulishwa na kichwa cha habari "why slaa must resign" https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-must-resign-effect-of-the-crowded-house.html

Katika bandiko hilo, mwandishi wake alielezea juu ya ulegevu na kuyumba kwa uongozi wa juu wa chadema chini ya Dr Slaa kama mtendaji mkuu na kwamba ili kunusuru hali hiyo ambayo mwandishi huyo alitabiri kuwa itakimaliza Chama hicho kwani kitapoteza wanachama lakini pia kitapoteza imani ya watanzania.,mwandishi alipendekeza Dr Slaa ajiuzulu.

Kama ilivyo kawaida ya sikio la kufa, viongozi wa juu wa Chadema walipingana na ushauri huo na kuendelea kubaki vin'ang'anizi katika nafasi zao walizozishikilia na hatimae leo tumeona yanayotokea, watu maelfu kwa maelfu wamekuwa wakiondoka chadema tena watu wenye nafasi nyeti na wenye influence kubwa kwa jamii. Leo lugha ya "KUJIUZULU'' imekuwa ni lugha ya kawaida kwa wanachadema wanaoujua ukweli na uhalisia wa Chama hicho kila uchao.

Lakini mwandishi aliposimamia hoja ya wimbi la watu ambalo aliwaita "oil Chafu" hasa baada ya Ally Bananga na James Ole Milya kujiunga na chama hicho, hoja hiyo sasa ni mfu. Hoja kuwa chadema kimepoteza mwelekeo kwa sababu watu ni wengi ni hoja mfu, hivi sasa Chama hicho kimebakiwa na wanachama wachache ambao ukiwajaza kwenye darasa moja la shule ya msingi ya kata wanatosha. Hoja ya uwingi sio hoja na kwa maana hiyo Dr Slaa aachwe akiongoze Chama, kwani hivi sasa watu wamepungua hivyo atafanya kazi zake za management vizuri na kwa urahisi.

Dr Slaa alisikika kuwa Chama hakijakomaa hivyo hakiwezi kufanya uchaguzi wake wa ndani ila kuanza kwa zoezi la uchaguzi ndani ya Chama hicho ni dalili kuwa Chama iko sasa kimekomaa na kwamba kinajiandaa kuchukua nchi 2015.

KILA LA KHEIR DR SLAA..,IKULU INAKUSUBIRI 2015.
 
Naomba ujibu swali hili: 'wakati wewe ni mwanachama wa CHADEMA chama kilikuwa na wanachama wangapi na sasa hivi CHADEMA kina wanachama wangapi'? Naomba ujibu swali hili tujue ukweli wako
 
Ndio unataka kusema ya kwamba unaipenda sana Chadema? we jali chama chako ya Chadema hayakuhusu...
 
Naomba ujibu swali hili: 'wakati wewe ni mwanachama wa Chadema chama kilikuwa na wanachama wangapi'? Naomba ujibu swali hili tujue ukweli wako
Kulikuwa na wanachama wengi kiasi kwamba ukiwaweka kwenye shule zote za msingi nchini madara yake yasingelitosha.
 
Mzee wa oil chafu Nape amekuwa mwandishi habari tena.
 
You again! Ndio umepewa kazi ya kuiandama CDM au ndio majuto mjukuu?

Sasa sikiliza wewe kitoto cha kike, hii wewe kuiandama CDM kila uchao ndio hasa indicator kwamba CDM ni mwendo mdundo na inawafanya restless ma- traitors mliokimbilia ufisadini.
Mwache Dr Slaa afanye kazi yake, kama ni dhaifu au laa waache wnaCDM waamue. Wewe uko Lumumba unawashwa na nini?! Wewe unatakiwa u-access utendaji wa katibu mkuu wako, Kinana a.k.a Dr Tembo. Huna right ya kuhoji uendeshaji wa CDM kwa sababu si mwanachama wake, right hiyo unayo huko ufisadini. Angalizo: Huko ufisadini usifungue kibakuli chako, wataku-kolimba straight away.
 
Kulikuwa na wanachama wengi kiasi kwamba ukiwaweka kwenye shule zote za msingi nchini madara yake yasingelitosha.

Wengi wangapi? Ninaamini mpaka unasema haya ulikuwa wajua idadi ya wanachama siamini kwamba wewe waweza kutunga. Ukitutajia idadi ya wanachama iliyo sahihi ya wanachama waliokuwepo kipindi hicho na waliopo sasa tutaamini ukweli wa 'post' yako hapo juu. Vinginevyo itakuwa ni hadithi ya kutunga.
 
Naomba ujibu swali hili: 'wakati wewe ni mwanachama wa CHADEMA chama kilikuwa na wanachama wangapi na sasa hivi CHADEMA kina wanachama wangapi'? Naomba ujibu swali hili tujue ukweli wako
Tupe kwanza takwimu za wanachama wangapi wameshakikimbia CHAMA kabla huyo dada hajakujibu swali lako.
 
Sasa hii maana yake nini..? jaribuni kutumia akili zenu wakati mwingine. Asubuhi yote hii unaanza na matusi yasiyo na sababu.

Juliana Shonza achana na hizi siasa chafu hautafanikiwa. Siku ile unatangaza uchumba kwa Mwansasu ndio siku pekee niliweza kukuona na nilitamani nipande madhabahuni na kukunong'oneza jambo kuwa usisahau lengo la Chadema kukupeleka ccm. Naamini unajua hili na naamini upo smart zaidi,now don't mess!!
 
Last edited by a moderator:
Juliana Shonza achana na hizi siasa chafu hautafanikiwa. Siku ile unatangaza uchumba kwa Mwansasu ndio siku pekee niliweza kukuona na nilitamani nipande madhabahuni na kukunong'oneza jambo kuwa usisahau lengo la Chadema kukupeleka ccm. Naamini unajua hili na naamini upo smart zaidi,now don't mess!!

Hahaaa, mpaka mtaomba po, dada Juli endelea kuwabana.
 
Ha ha ha ha ha haaaa ujue CCM hakuna kitu kimewatesa kama Uongozi imara wa Mbowe na Slaa.. Na mbinu zote walizotumia zimetoka kapa, walizani watanzania wote dizaini za kina Lyatonga, Dovutwa na Cheyo!!

Fanyeni kazi mjenge nchi labda mnaweza kupona na huruma ya wananchi achaneni na siasa za kupambana na jiwe msiloliweza
 
Dada mzuri kama huyu ni mfano wa kuigwa na wanachadema wote
 

Juliana Shonza, nilidhani baada ya kupata mchumba utapata mshauri ili uandike mambo yanayoeleweka, kumbe bado!
Sasa wewe kila ukilala unamuota Slaa, mchumba kakuchosha mara hii?

Halafu unasema eti wanachama wote wa CHADEMA hawajai darasa moja ya sekondari ya KATA...kumbe unazidharau sekondari za kata, unatafuta nini huko CCM basi? Maana sekondari za kata ni zao la CCM, sasa hujui kwamba unadhalilisha chama kinachokutumia vibaya?

Na kama maelfu wanahama CHADEMA, we si ufurahi, kinachokuwasha ninini mpaka uwahurumie CHADEMA. Pilipili wale wenzio, uwashwe wewe..Halafu eti unasoma Masters....Masters kweli siku hizi ni hovyo kabisa.....komaa binti, anza kujifunza kuandika ki Masters-Masters basi ueleweke, ala!
 



Kila la Kheri Juliana Shonza,

Haya ni maneno ya mfa maji haachi kutapa tapa, Mlisema Chadema kinakufa 2013, kumbe mwaka huo ndoyo ilikuwa mwisho wa wasaliti ndani ya Chama, tumeondoa wasaliti wote sasa Chama kiko imara kuliko wanachama wote.

Naona sasa wanaelekea ACT kufanya kazi aliyowahi kuifanya Mrema hakufanikiwa embu tuone kama na ACT aka Wasaliti wa Democrasia watafanikiwa kwa kufanya kazi mitandaoni.

Ni vigumu sana kukihujumu Chama ambacho 80% ya Graduates na Vijana wa nchi hii wanakiunga mkono na mfano mzuri ni kwenye hili lenu. Mnahangaika tangu mlipofukuzwa Chama hadi leo lakini waTZ wamewastukia na wamekata kuendeleza nusu karne ya Uwongo na usanii.

Mwisho wa kupewa hivyo vijisenti ni 2015 mtakapokuwa mmelizamisha hilo jahazi lenu au kijiwe chenu cha kupiga kodi zetu kwa kufanya propaganda za kwenye mitandao ya jamii.

 
Unaweza kukisoma ulichoandika?

Kwanini ukisikia Dr.Slaa unalowa na kuwa na hofu?
 
Sasa hii maana yake nini..? jaribuni kutumia akili zenu wakati mwingine. Asubuhi yote hii unaanza na matusi yasiyo na sababu.

Wewe umeachika kwanini usiongelee chama chako kupya,roho inakuuma eehh kuachika huku bado unapenda?kudhoofika kwa cdm si nafuu kwa chama chako.
 
Back
Top Bottom