Who really killed Prof. Mwaikusa?

vaticans are the "secret terrorists".....Papa John Paul II alihusika moja kwa moja kwenye mauaji ya wayahudi.....ts not a secret anymore......

Ndio nasikia leo, unaweza kutuletea vielelezo ili kutuaminisha tuhuma hizo?
 

Very possible mkuu!
 
Am afraid this might be a flip flop to mislead and misdirect truth and evade true perpetrators away from the book. Sijaona insurable interests za kumfanya Prof, ambaye alikuwa just a company secretary kuuawa na share holders (or people claiming to have insurable interests thereto). Am afraid this passage leave so many stones unturned, henceforth doesnt hold the issue water-tight.

That's my opinion.
 

Mwandishi wa habari hii ni aina ya waandishi wa kipumbavu kabisa.Na ndiyo maana sasa hivi wajanja wanalitizama Raia Mwema mara mbilimbili.Huwezi kutoa tuhuma nzito kama hizi kwa ushahidi wa kuokoteza na wa kijinga namna hii.
 

watishie na kukiona wakiendelea kukupekua. Attach na picha ya mkia wa warthog kiboko ya wambeya
 
Mwandishi wa habari hii ni aina ya waandishi wa kipumbavu kabisa.Na ndiyo maana sasa hivi wajanja wanalitizama Raia Mwema mara mbilimbili.Huwezi kutoa tuhuma nzito kama hizi kwa ushahidi wa kuokoteza na wa kijinga namna hii.

ninavyoona miye, kunaweza kukawepo ukweli kuwa baadhi yao kuhusika kama wanadamu, coz hawajamaliza ushahidi wao kwa nini kusema ushahidi dhaifu, tungoje tuone mwisho wa yote watawasilisha nini kuliko wandugu hapa jamnini kuwashambulia. binafsi nasubiri kwa hamu tena kubwa toleo lijalo kuona watakuja na vielelezo gani. Hapa songea nyumba ya pera siyo km ilivyokuwa zamani, ikizingatiwa uongozi sasa ivi mpya na una takribani miaka zaidi ya mitano. Abate lambet wala siyo liongozi wa sasa na yupo madarakani wanayemuita Annast, msaidizi wake ni buluda fidelis aliyepigiwa simu. fidelis ndiyo atueleze kulikono hapo wala sio abate lambet wala yule wa st otilien ujerumani. nionavyo wana point, kwa nini wampigie buluda fidelis na jonson nchimbi, naona candid unatupotosha, au wewe ni watu hao watajwao juu. kuna watu wanajifika ktk nyumba za sala jamani, nawaamini raia mwema, tujipe tu muda watueleze waliyonayo. tuhuma hizi nzito, wasingeziweka pasipokuwa na ushahidi wa kutosha.
 

Hakuna anayeweza kupingana na ukweli ukithibitika. Tatizo habari hii imechukuliwa kigezo tu kwamba kwa vile waliona sahihi za watawa wawili katika moja ya document za hayati Mwaikusa basi shirika la watawa hawa wamehusika kumwua. Hapo kitu kinaingia akilini hoja dhaifu kama hiyo?

Tukubaliane kuwa kuna tatizo la vyombo vya habari hasa magazeti na kabisa wahariri wakuu kutokuwa makini, pengine huwa hawapitii makala zote zinazowekwa magazetini. Shutuma za mauaji kwa shirika nyeti kama hilo ni jambo linahohitajika kujiridhisha kwa utafiti wa kutosha kabla ya kulituhumu kuhusika na mauaji hayo.
 

Nahisi ka-harufu kazito kwamba mauaji ya prof. Mwaikusa ni organised mission kati ya watu binafsi na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama (excluding jwtz) vya hapa nchini. Akina mwema na othman wanalijua hili.

Pole sana PhD kwa ban.
 
nadhani mwandishi wa hii makala elimu yake ni ya kudesa pia tena ya kidato kifupi.
kuonekana kwa sahihi za watawa watakuwa wamehusikaje? ok tusema prof alikuwa na client wengi sana kama advocate kwa hivo tuseme clients wake wote wanahusika pia hasa wale ambao kesi zao hawakushinda?
haya ni mawazo dhaifu sana kwa gazeti kama hili kuandika habari za kusadikika.
 
sasa kwanini hawawatuhumiwa hawajakamatwa kama ilivyofanyika kwa afande barlow au kwakuwa yeye hayuko kwenye system yetu ya Mkali JK lakini yote haya yana mwisho kwani misri, libya na tunisia na sasa syria mambo yamekuwa yamoto nchi hizi zimekuwakama kaa la mawe.
 
Aisee inaweza kuwa inaukweli maana hata baadhi ya mapapa waliwahi kuuliwa kwa kuwa na misimamo tofauti na kundi la baadhi ya watawa hasa wale washauri wakuu wa kanisa
 

hapo nakuelewa. Nimesoma habari nzima nione eneo ambalo wahusika walijaribu kupata nyara hizo zinazoitwa za mgodi. bila shaka kama unavyosema lengo hapa ni kupeleka taarifa kwa jamii kwamba watawa hawa wanamiliki mgodi.
 

Du wewe una macho lakini huoni. Narudia hilo la kuhusika na mauaji ya Prof M silijui, lakini hilo la nani alikuwa ni mmiliki au akihusika na huo mgodi halina siri. Sijui hata kwanini magazeti wamechelewa kuliandika hilo. Isitoshe si magazeti Mengi yaliyoandika, lakini halikuwa siri hivyo unavyofikiri wewe.

Kwa taarifa yako hata hiyo ardhi waliinunua kwa nani mimi nafahamu. Na zaidi ya hao waliotajwa kuna wa Afrika kusini wawili hawajatajwa katika gazeti hilo ambao ndio walikuwa wahusika wakubwa katika ununuaji wa madini hayo. Sikuelezi nafasi yangu katika biashara hiyo lakini hata baadhi ya vithibitisho vya majina ya wahusika vipo. Waliotajwa ni wachache tu katika gazeti, kuna vigogo gazeti limewaogopa au ni tactical move wakisubiri reaction. Hii usibishe.

Unadai eti pesa zile ni ndogo ukilinganisha na pesa walizokuwa wanapata Ujerumani na Uswiss. Hivi unajua ni kilo ngapi zilikuwa zinapatikana katika mgodi ule kila siku? Hujui kitu, we acha tu kwa sababu hujui vyombo vilivyokuwepo huko, si majembe na sululu bali ni vyombo vikali toka Afrika Ya Kusini. Usilopoke juu ya kiwango kama huna namba, omba tutakupatia.

Unasema "Unamfahamu Rt Rev. Abbot Lambert Dorr OSB wa Abatia Peramihi" wacha huyo hata yule mjerumani aliyeishika Peramiho "Hanzgali" akiwa toka ujana wake mpaka kafia huko Peramiho Namfahamu. Tena si nilikuwa namjua tu bali hata yeye ananifahamu. Baadhi ya nafasi alizozishika ni ukurugenzi wa Hospitali ambaye sasa ameachiwa Dr Remy.

La mwisho ninasikitika sana kwa maelezo yako eti "Huo uchafu wa mgodi ni nini ukilinganisha na makubwa yalifanywa miaka nenda rudi kujenga mashule, hospitali, zahanati, vituo vya afya, na mengineyo" Kwa hili ninakusikitikia sana maana suala la Ethic na Moral values uko ziro. Yaani kwa vile wamefanya hayo mazuri basi wanaruksa ya kuiba malizetu nasi tucheke tu. Unajua hata Huko Ujerumani, huyo Bi Angel Markel licha ya mazuri yote aliyofanya akikutikana kaiba dola 100 000 za kimarekani kazi hana na mazuri yote yanasahaulika. Si umeona kinara wa Italia Beluskoni kaenda jela.

Hapa suala si kiwango bali ni moral values ndio muhimu. Tanzania tujifunze hili vinginevyo tutaimaliza nchi. Tafadhali kasome Ethics and Morals ili uisaidie nchi yako.
 

Hapa ndio mtanzania katoa bonge la hoja kwa mada nzito kama hiyo. Kweli Mtanzania huwezi kumtetea WALA KUMSAIDIA.

Leo nimefahamu kwanini JK alikiri kuwa hajui kwanini Tanzania ni masikini? Nafikieri hakujua kama ni umasikini wa rasilimali au AKILI?
 

Kwanza nikupe pole kwa kutojadili hoja husika katika mada gazetini ambayo maudhui yake ni mauaji ya Maikusa, kwamba yalipangwa ndani ya Abatia ya Peramiho na kuatibiwa na Abate Lambert Dorr OSB akiwa ndiye kiongozi wa juu pale kama mkuu wa Abatia. Ningekushauri anzisha mada nyingine inayohusu moral itajadilika vizuri. Hapo utatuletea vielelezo na viambatanisho vya kutujuza uhusika wao na mradi huo kama walimiliki au walitumika kama washauri kwa wachimbaji au waliwekeza vifaa vilivyotumika katika mradi huo vikiwa kama ndio sehemu ya hisa. Hilo twalisubiri uanzishe mada linajadilika.

Kwa uelewa wako sahihi za Brother Edmond ambaye kama sijachanganya ni Br Edmond Kimario mtaalamu wa umeme anayeendesha kitengo cha hicho katika abatia hiyo pamoja na mwenzake Brother Aidan vinathibitisha kuhusika katika mauaji au ni kwa vile tu ni watawa kufanya usichotegemea kiuchumi basi ndio wahusika na mauaji?

Tunacho kijadili hapa ni kesi nzito ya mauaji. Suala kama walihujumu uchumi wa madini au maadili yao kidhamiri kadiri ya mwenendo wa maisha yao ni kesi nyingine ijadilike kwa namna ya uhujumu uchumi si mauaji kwani ni vitu viwili tofauti. Cha ajabu unachohangaika kujibu umejichanganya kwamba la mauaji ya Maikusa hulijui, unawezaje kulijadili jambo usilolijua wakati maudhui ya mada ni kuhusu mauaji hayo?

Nakushauri sana anzisha mada nyingine ya kujadili hilo, kwani mimi mleta mada nililenga maudhui ya mauaji yalivyoripotiwa na gazeti. Natumaini umenipata na kunielewa vizuri. Jazba tuweke kando tunapo jadili mada kama hizi, kwani kama unavyosema wawajua hao ni wengi sana hapa wanawajua sana tu kama nilivyokufafanulia hata mmoja ya majina na kazi anayofanya sijui kama unafahamu hata hilo.
 
Hapa ndio mtanzania katoa bonge la hoja kwa mada nzito kama hiyo. Kweli Mtanzania huwezi kumtetea WALA KUMSAIDIA.

Leo nimefahamu kwanini JK alikiri kuwa hajui kwanini Tanzania ni masikini? Nafikieri hakujua kama ni umasikini wa rasilimali au AKILI?

Kwa taarifa yako Rt Rev Abbot Lambert Dorr OSB ni Abate mstaafu, kuna Abate mpya aliyechaguliwa miaka kadhaa na makamu wake ambaye kwa cheo ni Prior ni mwingine. Pengine mwandishi huyu wa gazeti amejichanganya kwa kutaja watu ambao kwa wakati huo kama Lambert hakuwapo madarakani.

Halafu unavyoonekana kuvamia kitu usichokijau.
Hospitali ya Peramiho haikuongozwa na Dr Brother Ansgar OSB kama unavyosema, Dr. Ansigar alikuja kuwa Dr. Mkuu Peramiho miaka ya karibuni sana na hajakaa sana, kadiri ya utaratibu wao wa kikazi alirudishwa Ujerumani kushika majukumu mengine ya kiuchumi badala ya uganga.

Kwa taarifa yako Dr. Ansgar hayuko tena Peramiho Hospitali kwa vile shirika lake la St Otilien Ujerumani ambako ni makao Makuu yao walimpa jukumu jipya tofauti na hilo la uganga, alichaguliwa kuwa Procurator Mkuu wa shirika wadhifa ambao anaushikilia hadi sasa huku Ujerumani, maana yake Monastery zote za Peramiho, Uwemba, Ndanda, Hanga, Kurasini Benediction Fadhers, nyingine za Tanzania, Korea, Ujerumani, Marekani kana Newton NJ, Wisconsin, na kwngineko yeye ndiye Procurator Mkuu wao. Je unalifahamu hilo? Usijefikiria watu hawawajui watu hao.
 
Mimi naunga mkono baadhi ya wasomaji, kuwa mtawa c tatizo la kukimbia maumbile na asili ya ubinadamu. Na kwakuwa wengi wanaona dini, dhehebu na misaada pa1 na unyenyekevu basi wanasadiki mara moja bila shaka, na ukizingatia neno lenyewe ni la kizungu basi inaleta tabu. Romani Catholic (RC) huu ni utawala wa kirumi, hii ni pembe iliyotabiriwa ktk ufunuo na itawatesa wengi; watatenda haya wakiwa nyuma ya Imani yao. Tuwe makini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…