Mmmhh, kuna hatari kama serekali haitafuatilia hili, na mimi napata uoga. Fidelis anajivunia pesa ya shilika, huwezi kuamini, kumbe watu wanalijua hili ila hawana pa kusemea. mmojawapo aliniambia wakati tunajadili gazeti kuwa wangejua raia mwema wangekuja tuwaelezee jinsi pelamiho ilivyovamiwa. Mungu walinde watumishi wako aidani na edmund wawe salama. mlinde na buluda God na wengine wanaoonewa.[/QUOT
Serikali haina nafasi ya kufuatilia mambo ya ndani ya nyumba, yanawahusu wanafamilia na sisi wengine tunaumiza vichwa bure. Laiti tungejua yanayoendelea ndani ya monastery, ma-convent, maseminari, ni vioja lakini wanayamaliza wenyewe na inaposhindikana na kumfukuza. Wana vyombo vyao vya kusahihishana ikiwa ni pamoja na 'culpa' (baraza la mashtaka, halmashauri ya nyumba na shirika na hali kadhalika mikutano yao. Hayo ya kwao mimi binafsi sioni sababu ya kuumiza kichwa.
Tunachotaka ni evedence ya kuhusika kwao katika mauaji, hizi blabla haizina maana maana ni malalamiko yesiyo na vielelezo vya kuonyesha evidence ya kuhusika kwao na mauaji ya Maikusa. Kinachoendelea hapa katika majadiliano ni ule uswahili wa vijiweni si misingi ya hoja za great thinkers.
Kwa sasa naelekea kufunga mjadala kwa kuhitimisha kauli yangu na kuomba moderator wafunge majadiliano, maana kinachoendelea si hoja za maana zaidi ya kundi lenye kuleta tu manung'uniko jambo ambalo linapoteza maana ya maudhui ya mada hii.
Wametuhumiwa kuua na wewe unasema serekali haina hoja katika hili. unamdanganya nani. Damu na haki ya mtu haipotei bule amini usiamini. mwisho wa yote ukweli huwa unajulikana hata kama ni muda mlefu kiasi gani itachukua. Nakushauri waambie hao wateja wako kama siyo wewe mwenyewe muwahi mahakamani kushitaki raia mwema kuwa wamewasingizia kuua. mkoba mwanasheria wenu si aliomba aombwe radhi la sivyo mnafungua mashtaka, badala yake hawakuwaomba msamaha na wakaomgeza mabandiko yao wewe huoni kuwa wanao uhakika. vinginevyo ili kujisafisha kuwa ninyi ni wasafi ndugu wahini mahakamani kama mlivyowatishia raia mwema.
Hizi ni bla bla za kutishia nyau, umtishe nani, na wenzio wa raia mwema wamekaa kimya wasitishwe na mkwara wenu, hamshangai tu.
Mwanzoni ulisema kuwa hawa ni watu wa sala muda mwingi hawawezi kuingia ktk mambo mabaya, na sasa kwa vidole vyako unasema ndani ya nyumba zao ni
vioja, nimekushangaa. Sasa ulikuwa unawatetea nini na sasa unaandika nini.
Hata hivo tunawashukuru raia mwema na wewe mwenyewe mmetupatia mwanga wa madudu yenu huko ndani, yaani miongoni mwenu kuna wanakondoo na wengine ni wale waliojiveka mavazi tu ya kondoo ila wapo ili kuwararua.