Ni upumbavu kukataa kukubali kuwa kikwete anajaribu kumpa maelekezo,labda hata tishio na au rushwa akipata urais tendwa aule zaidi.na tendwa kama hakimu anakutana vipi faragha na mtuhuhumiwa? Au elimu yake ni ualimu wa chekechea tuliowaona akiwafundisha?
Kumbuka kwamba Rais KIKWETE ni mkuu wa nchi na serikali na anamamlaka ya kumwita kiongozi yeyote Ikulu na kumwuliza chochote kuhusu nchi. Hivyo wito waTendwa IKULU siyo lazima uwe na uhusiano na pingamizi la CHADEMA,hizo ni hisia zako tu.
Kwanini huna hisia za kwamba Tendwa alikwenda IKULU kumweleza Rais mikakati aliyonayo ya kuendeleza na kukuza demokrasia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Unachotakiwa hapa ni kupinga habari kama si ya kweli whether imetolewa na Ngurumo au Radi.Taarifa ikitoka kwa Ansbert Ngurumo ni ya kuchunga sana kwani yeye ni mdau (chadema damu) katika pingamizi hilo.
kwa nini tunahukumu kabla ya kujua ukweli kama habari hii ni ya ukweli au ni propaganda za kisiasa tu. JK mwaka huu una kazi kila ngoma inapigwa kwako bila hata utafiti wa kutosha. Tatizo kubwa la JK ni kukubarika sana kiasi kwamba wapinzani wanatafuta kila silaha ili wakupige nayo. Ushindi wa kishindio ni lazima mwaka huu. CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeee, Kikwete JUU, juu juu zaidi.
wewe pia una ruhusa kuweka nyundo na jenbe la mkono kwenye avatar yako ni ruhusa. Lakini kwa kuwa hamna hakika ya ushindi mmekaa mkao wa kukimbia.Waliopamba bendera za chadema hapa JF waondoe mapema, ushindi wa CCM ni lazima.
Tendwa aliitwa kuangalia namna ya kuimarisha vyama vya upinzani nchini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Huu ndio mtazamo wangu.
Wababaishaji utawajua tu.Tendwa hakuitwa Ikulu ni uzushi tu. Ansebet Ngurumo ni Majeruhi wa Uchaguzi MKUU 2010 bado anaota ndoto ya CCM kupata viti 21 vya ubunge bila kupingwa na viti 251 vya udiwani. mwaka huu mtasingizia sana ili tuwape kura za huruma.
akili yako na ya kikwete ni sawa sawa tu. Unadhani ukiwa ikulu basi usifuate sheria? Watu kama nyinyi mgekuwa nchi kama china usingelikuwa bado upo ardhini ukivuta hewa ya bure