Kama ni neno la Mungu kwa nini lisiandikwe kwa aina ambayo haina utata?
Hapo majibu yako ninachoona ni kama vile Quran imesema kuna watu Mungu kawaziba macho na masikio na kafunga mioyo yao wasimjue, halafu atawahukumu kwa kutomjua, kitu ambacho ni kum victimize mtu asiweze kumjua Mungu halafu kumlaumu na kumhukumu kwa kutomjua Mungu (kama baba anayemkataza mtoto wake kwenda shule kujifunza kusoma halafu kumhukumu kwa sababu mtoto hajui kusoma)
Baada ya hapo unaanza kuleta maelezo tofauti na Quran inavyosema kwa kusema neno la Mungu halisomwi kama gazeti.
Inaonekana unataka kutumia hii habari ya "neno la Mungu halisomwi kama gazeti" kubadilisha maneno.
Kama kuna Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa nini hakuweka maneno yake vuchwani mwetu kila mtu kwa lugha yake tangu tunazaliwa kwa namna isiyo na shaka vyovyote kwamba hili ni neno la Mungu?
Kwa nini tutegemee vitabu, tafsiri za kutoka kiarabu, utata wa jinsi ya kusoma neno la Mungu huku wengine wakisema halisomwi kama gazeti na wengine wakisema kusema hivyo ni upindishaji wa maneno tu etc?
Kwa nini tunategemea vitabu kumjua Mungu wakati Mungu aliweza kuweka maneno yote hayo ya vitabu vichwani mwetu?