Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Huko whistleblower huku polepole huku Bandari na kampuni feki ya meli nk

Kila jipya likiibuka la zamani linasahaulika
 
Halafu wanatuletea stori za legacy sijui hero! Kumbe mtesi wa wananchi! Kama ni kweli na alaaniwe! CCM imefika mahali kila adhaniwaye ni msafi kumbe ananuka kuliko mwenzie! Chama kimefika hatua kinatumia vyombo vya dola (bunge, jeshi, mahakama, ofisi za serikali - DPP, DCI, Polisi, etc.) kujihalalishia uchafu wao; ni hatari sana.
Yaani mumekuwa wepesi wa kuamini udaku kutoka kundi la wahuni.
 


Ziara ya NSSF na Magereza kwenda kujifunza kwa Bakhresa ni ubia wa watu wawili hiko kiwanda; tofauti na porojo tunazotaka kulishwa.

Binafsi naamini serikalini kuna wazalendo wengi sana wenye nia njema ya kulisaidia taifa. Wanachohitaji ni kiongozi mwenye maono kama yao vinginevyo ukiingia kichwa mwenyewe utapotea kihasara hasara bure tu; kilichobaki unaangalia misimamo ya raisi ukiona yupo kama mama na wewe iba yaishe kuliko kiherehere.

Ata huyo Magufuli alikuwa na ushamba fulani kama kuwasaidia wazalendo serikalini ni kwa asilimia ambazo azifiki za juu kabisa. Walau he did something na alikuwa anasoma mafaili waliyokuwa wanampelekea na kushaurika maeneo kadhaa.

Hii nchi imejaa mijizi japo siungi mkono NSSF kuingia kwenye sukari (simply they don’t have the know to run such a business) lakini Magufuli hana mkono ni kihehere chao. Na NSSF awapo kwenye sukari kipindi hiko hiko cha Magufuli waliingia kwenye ubia wa kuzalisha mafuta ya kupikia (god knows what other production industry they’re involved in) na kwenye sukari wanaenda jenga kwa ubia na Magereza awapo pekee yao.

Mtu anakuja anaandika ujinga mtupu what would you call that, other than nonsense.
Hivi tangu lini uliona mtu akiziba tundu la choo kabla ya kukamilika choo kipya?.Hakukuwa na sababu ya kulazimisha sukari ipande bei kabla ya viwanda kukamilika.
Utetezi wako ni ujinga tu pia.
 
Kuwapa NSSF kazi ya kujenga kiwanda cha sukari ilikuwa ni kukaribisha ufisadi.
Magu alitaka waache kuwekeza kwenye majuba wahamie kwenye kuzalisha sukari.Akitaka uzalishaji wa sukari uongezeke kwa kiwango kikubwa,pia alimuongeza Azam kama eka elfu nane au zaidi kwa kazi hiyo hiyo ya kuzalisha sukari.
Kumbe behind the scenes ndio hawa Mtibwa na Kagera Sugar na labda kuna wengine wanatuchezea likembe.
Dawa yake ni kuwaruhusu wawekezaji maarufu kutoka Brazil waliokuwa wamewekewa kauzibe na taasisi zetu,kwa maslahi yao binafsi wazalishe sukari ya kutosha.
 
BARUA KWA RAIS SAMIA SULUHU KUHUSU UFISADI KWENYE SUKARI

11 December 2021


Mheshimiwa Rais nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini ningependa badala ya kusema kazi Iendelee basi uitikie haki, ustawi wa watu na uhuru wa kweli.

Mheshimiwa Rais nina mengi ya kukueleza kuhusu nchi yetu lakini leo ningependa kukueleza moja ambalo ni maombi yangu kwamba utalifanyia kazi ili kuitoa nchi yetu katika uchafu huu mkubwa. Jambo hili ni ulanguzi katika bei ya sukari na ufisadi mkubwa uliopo katika eneo la bidhaa muhimu (nipatapo wasaa nitakuandikia barua zaidi kuhusu bidhaa nyingine kama mafuta ya kula). Nakiri kwamba bei ya bidhaa hizi inachangiwa na mwenendo wa bei ya soko la dunia lakini pia inachangiwa na ufisadi uliopo katika soko la ndani.

Kwenye sukari tuna kundi dogo la wazalishaji nchini na hawa wana kikundi chao ambacho kisheria si sahihi (cartel). Kikundi hiki kiko chini ya Seif Ally Seif ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Superdoll (wamiliki wa Mtibwa na Kagera Sugar). Bei za sukari zinaweza kupandishwa kwa namna mbili, kwanza kwa kuamua kiasi gani cha sukari viwanda vya ndani vizalishe, maana yake hapa unaamua kiasi gani cha sukari kiwe kwenye maghala.

Ukishaamua kiasi basi bei itapanda kuendana na kiasi. Maana yake ukiamua sukari uzalishe kidogo basi bei itapaa sababu bidhaa inakuwa chache na wahitaji ni wengi. Namna ya pili ni kushirikiana na watendaji walio serikalini kuhakikisha kwamba unapobana uzalishaji soko la ndani ili kuwe na uhaba na bei iwe juu basi serikali haitoi vibali kwa watu kuingiza sukari nchini sababu kwa kufanya hivyo uhaba hautakuwepo na bei unayotaka wewe itavurugika. Huo ndio mchezo unaochezwa Tanzania.

Ilikuwaje?

Endelea kusoma HAPA
Miaka saba baadaye...
 
Mwambie huyo mchambuzi alete ushahidi wa maelezo yake. Mbona Hutaki Unaacha alikuwa anatupa hata na account namba za benki pesa zilipopita, siku hata saa na nani alipokea hizo fedha!? Watu watoe tuhuma kwa ushahidi usiotiliwa shaka. Vinginevyo, huku ni kuchafuana kwa maslahi binafsi.
Ujinga na upumbavu wako ni laana kwa wazazi wako.
 
Sijawahi wala sitakaa nimfikirie Majaliwa kama mtu mwema kwa hili Taifa na watu wake. Mungu anisamehe ila namuona Majaliwa kama mtu mwenye roho mbaya, mnafiki, mzandiki na mwenye tamaa. Hajawahi kuwa mkweli kwa Taifa.

Hata sasa namuona ndie masta mind wa anguko la Mama. Ana jionyesha kwake kama mtu mwema lakini hafai. Muda utaongea. Nani alijua yeye na Jenister ndio wako nyuma ya sakata la sukari? Bado ikija ya mafuta ya kula na mafuta ya gari utamkuta Majaliwa.

Tulimpigia Mama kelele aanze na safu yake akaona watu wana mfundisha kazi. Akabeba uchafu wa mwenda kuzimu. Sasa wazimu una mkuta. Amebaki kusema hato kubali wakati amesha kubali. Hata madudu yaliyopo bandarini ukifuatilia mkono wa Majaliwa upo. Makesi ya hovyo mahakamani Majaliwa yupo. Say all evils lazima yupo.
Umeongea maneno mengi,lkn hujasema chochote.hebu weka hata ushahidi kidogo.
 
Sijawahi wala sitakaa nimfikirie Majaliwa kama mtu mwema kwa hili Taifa na watu wake. Mungu anisamehe ila namuona Majaliwa kama mtu mwenye roho mbaya, mnafiki, mzandiki na mwenye tamaa. Hajawahi kuwa mkweli kwa Taifa.

Hata sasa namuona ndie masta mind wa anguko la Mama. Ana jionyesha kwake kama mtu mwema lakini hafai. Muda utaongea. Nani alijua yeye na Jenister ndio wako nyuma ya sakata la sukari? Bado ikija ya mafuta ya kula na mafuta ya gari utamkuta Majaliwa.

Tulimpigia Mama kelele aanze na safu yake akaona watu wana mfundisha kazi. Akabeba uchafu wa mwenda kuzimu. Sasa wazimu una mkuta. Amebaki kusema hato kubali wakati amesha kubali. Hata madudu yaliyopo bandarini ukifuatilia mkono wa Majaliwa upo. Makesi ya hovyo mahakamani Majaliwa yupo. Say all evils lazima yupo.
Waziri Mkuu haondolewi kirahisi tu kwa hisia zetu tu, ni mtu mkubwa sana na naamini SSH kumteua Biteko nia ni hiyo ya kumpunguza kazi kaka Kassim.

Naamini SSH ni kiongozi mzuri kwenye mikakati ya mapambano ya chini kwa chini, ni mwanamama hivyo moja kwa moja anazifahamu siasa za vijembe, umbea na masuala yote ya unafiki wa usoni.
 
Back
Top Bottom