Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,565
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amejibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa kuhusu kupanda bei kwa sukari huku akiwatahadharisha Wafanyabishara wanaotumia Wanasiasa kuishikilia bango ajenda ya kupanda kwa bei ya sukari kwamba ajenda hiyo haitofanikiwa kwasababu tayari kuna bei elekezi inayotakiwa kulindwa.
Bashe amesema hayo katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kukabidhi vitendea kazi kwa Tume hiyo.
“Kuna upungufu wa msambao wa sukari haina maana kwamba Nchi ina zero supply of the sugar sukari ipo inawezekana haitoshelezi kwa kiwango ambacho tulichotarajia kwasababu viwanda vimesimama na niwambie Watanzania meli ya kwanza ambayo tulitoa kibali cha kuingiza sukari Nchini imeshafika na kuanzia kesho na keshokutwa itaanza kupakuliwa ili sukari iingie Mtaani”
“Ninachotaka niwapelekee ujumbe waache ku-lobby kuzunguka kuijadili bei elekezi, Mimi ndiye Waziri wa Kilimo kama wanahoja waje Wizarani hawatotatuliwa hoja yao kwa ku-lobby kwa yoyote Nchi hii ambaye anaweza kuniambia ondoa bei elekezi wako wanne Rais wa JMT, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, hawa ndio wanaweza kuniita na kunihoji hakuna Mtu mwingine yoyote”
“Tulikuwa na mfumo wa upangaji bei tulikuwa na stability ya price mpaka mwezi December mwanzoni wasi-take advantage tumeilinda Sekta hii kwa jasho na damu, kama wana hoja za msingi wafike ofisini kwa ajili ya kujadili kwani Serikali hutoa nafuu za kikodi ambayo humsaidia Mfanyabiashara hadi Mlaji wa mwisho”