WhatsApp Messenger chat Itanivunjia ndoa yangu..

Ladies and Gents habari za siku nyingi ..

Nilikuwa busy na kitabu pia family ndio maana nimekuwa Kimya Kidogo
Leo nina tatizo naomba ushauri na msaada kimawazo..

Nimekuwa na mme wangu kwa miaka minne sasa na tumebahatika kupata mtoto ana 2 years old girl

Jmos moja mme wangu alinipa simu yake kuongea na mama mkwe baada ya kumaliza kuongea nikawa najifunza kutumia smart phone ya husb tukiwa kwenye sherehe nilishawishika kuingia kwenye picha na whatsApp pia

Huko nikaanza kuingia kila sehemu..Ile nafika WhatsApp walahi niliumia oho sana

Mme wangu alikuwa anachat na wakina dada tofauti tofauti mambo ya mapenzi na kuombana kutumiana picha ...na mengineyo sipendi kusema
Pia nilikuta kwenye Picture profile mme wangu ana picha zaidi ya sita za kina dada waliomtumia kwenye WhatsApp

Nilimuuliza mme wangu hakunipa maneno ya kueleweka ,na mimeshajua mwenzangu ananicheat wakati mie nimejituliza nyumbani nalea mwanangu wa miaka miwili.

Lakini Bado nimesikia sasa ni kilio cha wanandoa wengi na mahusiano yanavunjika kwa sababu ya hizi wasapu..

Wapenzi niambieni nifanyeje roho inaniuma sana!naichukia ndoa kama ndo kuna usaliti wa hivi

Wenu Egyps
*********

Siku nyingine usirudie kushika simu ya mmeo. Hilo ndilo fundisho kuu.

Mi sijawahi shika simu ya mke wangu,na yeye hata akiishika yangu, password ataijulia wapi? Maisha haya ya sasa, ukimchunguza sana bata hutamla. Maisha yenyewe mafupi yanini kujiua na mapresha ya bure??
 
Usi rudie tena kukaguwa simu hisiyo yako!
 
pole sana tumia sana busara na usipanic, muulize na umuonyeshe kuwa umeumia ili nae aweke umakini kwa ukisemacho.
 
ni PM namba yako ya simu au email kwa ushauri murua.

We utingo, ushauri gani murua na wa faragha unaotaka kumpa MKE WA MTU?
Au ndio Yale ya ......we alipo mwagiza Mbunge wa Viti MAALUM amfuate dubai kwa ajili ya KAZI MAALUM.
Hahahahah..........
 
Ladies and Gents habari za siku nyingi ..

Nilikuwa busy na kitabu pia family ndio maana nimekuwa Kimya Kidogo
Leo nina tatizo naomba ushauri na msaada kimawazo..

Nimekuwa na mme wangu kwa miaka minne sasa na tumebahatika kupata mtoto ana 2 years old girl

Jmos moja mme wangu alinipa simu yake kuongea na mama mkwe baada ya kumaliza kuongea nikawa najifunza kutumia smart phone ya husb tukiwa kwenye sherehe nilishawishika kuingia kwenye picha na whatsApp pia

Huko nikaanza kuingia kila sehemu..Ile nafika WhatsApp walahi niliumia oho sana

Mme wangu alikuwa anachat na wakina dada tofauti tofauti mambo ya mapenzi na kuombana kutumiana picha ...na mengineyo sipendi kusema
Pia nilikuta kwenye Picture profile mme wangu ana picha zaidi ya sita za kina dada waliomtumia kwenye WhatsApp

Nilimuuliza mme wangu hakunipa maneno ya kueleweka ,na mimeshajua mwenzangu ananicheat wakati mie nimejituliza nyumbani nalea mwanangu wa miaka miwili.

Lakini Bado nimesikia sasa ni kilio cha wanandoa wengi na mahusiano yanavunjika kwa sababu ya hizi wasapu..

Wapenzi niambieni nifanyeje roho inaniuma sana!naichukia ndoa kama ndo kuna usaliti wa hivi

Wenu Egyps
*********
mama usijali...nataka uelewe kwamba asili ya wanaume ndo hiyo. mme wako anakupenda tu wewe hao wengine wanapita tu..he was just unwinding..ongea na mtu wako kwa upole afu uone vile utabembelezwa. ( ndo utamu wa ndoa)
 
wewe usitake nikuboe kabisa wanaume woteeee malimbukeni,,, na amajui mnataka nini? ni kweli kama unakuwa wakatili kwa nini nisiwafananishe na wanyama loh

mbana unajibu post nusu? Jibu yote usichague. Eti usitake nikuboe! Utaniboaje?
 
Siku nyingine usirudie kushika simu ya mmeo. Hilo ndilo fundisho kuu.

Mi sijawahi shika simu ya mke wangu,na yeye hata akiishika yangu, password ataijulia wapi? Maisha haya ya sasa, ukimchunguza sana bata hutamla. Maisha yenyewe mafupi yanini kujiua na mapresha ya bure??

Umesomeka babu
 
dada kwenye hii dunia hakuna malaika cha msingi ni kumshauri na kumwomba mungu naomba muwa uwe fundisho kwako kwani muwa ni mtam lakini kila baada ya pingili moja unakutana na fundo na hilo ndio fundo ktk maisha yako pole sana ila hakuna kitu kiliwahi kumshinda mungu omba bila kukoma
 
Egyps-women chukua hiyo smartphone ukae nayo wewe. yeye mnunulie mchina ya tochi. Hii itakusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hata wanawake wa siku hizi wanashawishi sana kwa utundu sisi full kulegea mwili mzima una anguka puuuu. Tudada tunatupia picha za kichokozi mara kalio, mara nido jelly, mara kamguu nasehemu zake za juu.... full tabu jamani. Sisi wanaume mashambulizi yametuzidi nguvu. Halafu kumbuka uwiano kati ya wanaume na wanawake kwa TZ haupo sawa. Its obvious mkashare little resources available.
 
Back
Top Bottom