Jinsi nilivyoanza ujasiriamali kipindi nipo chuo

Jinsi nilivyoanza ujasiriamali kipindi nipo chuo

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,039
Reaction score
3,084
nakumbuka kipindi hicho nilikua nimepanga mtaani ilikua ni mwaka wa pili maana mwaka wa kwanza nilikaa hostel

baada tu ya kuingia mwaka wa pili nikatafuta geto nikalipia kodi nikanunua godoro na mazaga machache,

sasa mimi ni mtu ambae napenda wanyama baada ya kuona nimekaa mpweke sana pale geto nikatafuta paka, nikapata katoto cha paka kazuri sana kwaiyo pakawa pamechangamka kwelikweli mudawote ni michezo na kurupushani.

sasa pale tulipopanga kulikua kuna wapangaji wezangu na wengine walikua wanachuo pia nikaona wengine hawajapendezwa kuona kuna paka kwenye maeneo yao.

kuna mdada moja nikamuuliza kwanini hupendi paka ? akasema yeye hapendi tu na anawaogopa sana

huyu mdada kwenye dp yake ya WhatsApp alikua anapenda sana kuweka picha ya vitoto vya paka, kama ambayo wasichana wengi pia huweka maana vitoto vya paka hua vinavutia kuvitazama.

nikamuuliza mbona unapenda kuweka picha ya paka kama unawaogopa ? akasema yeye anawapenda tu kwenye picha ila live anawaogopa.

nikaona sasa hapa wanataka kunipangia maisha, nikaanza kujichanga hela huku nikiendelea kuishi na yule paka wangu.

kuna kiasi kilipofika nikanunua Ng'ombe, ikawa mchana namfunga nje namkatia majani, usiku namrudisha ndani ili tu kuwaonyesha kwamba hawapaswi kunipangia jinsi ya kuendesha maisha, lakini baadae nikaona kuna fursa ya kuuza maziwa kwaiyo yule ng'ombe nikaenda kumpandisha, akazaa nikaanza kukamua maziwa.

ndo nikaanza biashara ya maziwa nikiwa chuo hapo mwaka wa tatu, na majirani zangu wote nikawa nawapa maziwa bure kilasiku.

kwaiyo ndo nikaanzia hapo biashara ya maziwa hadi nikanunua kiwanja nilipokua mwaka wa 4.
 
32340824-1A49-4EE8-BF68-F631F3CA1ADC.jpeg
 
Nafikiri kipaji chako cha kufanya miujiza kimerudi tena,

JF VAR CHECK

 
Back
Top Bottom