My dear, kwanza pole sana na hilo janga lililokukuta, I can imagine ni jinsi gani umekosa amani moyoni.
Pili, ningeomba nikushauri vitu kadhaa kuhusu hilo. Kama wengi walivyosema whatsapp pengine sio chanzo cha matatizo yako, mwanaume mwenye tamaa na uthubutu wa kutembea nje ya ndoa/mahusiano hawezi kuzuiwa na whatsapp au other social networks.
Cha msingi umeshamuuliza, hata kama amekupa majibu ambayo hayajakuridhisha ameshajua kuwa unajua kinachoendelea.
Sasa, jaribu haya yafuatayo jaribu kumuonyesha kuwa hauna furaha. Kama kuna vitu ulikuwa unamfanyia kwa mahaba na upendo wa hali ya juu then do them slightly different. Sikwambii uache kumhudumia hapana, ila muonyeshe kwamba kuna tofauti na imeanza tangu ulipobaini kuwa ana mawasiliano ya kimapenzi na wanawake wengine. If youre lucky enough kuwa na mume sensitive anayejali atajirudi na kuomba radhi na kutaka kuyaongelea kwa lengo la kuyamaliza na kukurejeshea amani wewe mke wake.
However, kama mume wako ni wale insensitive people ambao hawajali hata kidogo na pengine akanotice hauko sawa na kutojali kabisaaa, usifadhaike. Piga moyo konde, muombe Mungu akupe ujasiri na moyo wa kupuuzia lakini pia muombee mume wako mpaka atakapoona kuwa hamna jipya huko kwa hao wadada.
Wanaume mara nyingine ni kama watoto wadogo, akitaka kitu atakililia mpaka akipate na akishakipata ndio anatulia.
Epuka kuanzisha drama na hao wanawake wake wa whatsapp kwasababu hawana hadhi kwako. Pili, usikimbilie kwa washauri wa ndoa na walimu wa dini au wazazi na kuwaeleza umekuta picha za wanawake kwenye simu ya mmeo, labda ikitokea hapo mbeleni matatizo yamekuwa makubwa zaidi, then only nitashauri hilo.
Ni kweli kuwa kama kweli hayo maongezi hayaishii kwenye whatsapp pekee kuna hatari ya kupata magonjwa ya ngono na kukuambukiza ila hapa sidhani kama una la kufanya zaidi ya kumkumbusha mara kwa mara kuhusu hatari hiyo na kusali kwa midii zote.
Epuka pia simu ya mumeo. Hili nimejifunza kutoka kwa wazazi wangu wenyewe. mtaishi kwa amani sana usipomchunguza chunguza mumeo.
Kuwa na kifua kwenye hili, ndio kipimo cha mwanamke.Mwanamke mwenye nguvu na hekima.
You seem like a smart and humble woman, natumai hautashindwa na whatsapp haitavunja ndoa yako. 🙂