Whats your talent...???

Whats your talent...???

Naamini katika jamvi hili la JF kuna watu wenye vipaji vingi na vya kila aina, wengine wana vipaji vya ufundi wengine kuigiza wengine kuimba n.k. Leo ningependa wana Jamii Forums wote tushare vipaji vyetu tulivyonavyo katika thread hii. Huwezi jua pengine kipaji chako kinaweza kumnufaisha mwingine au kipaji cha mwingine kukunufaisha na pengine kipaji chako kinaweza kukunufaisha wewe mwenyewe hapa jamvini kwa namna moja au nyingine.

Ningependa mimi ndio niwe wa kwanza wa kueleza vipaji nilivyojaliwa na Mwenyezi Mungu na vielezea kimoja baada ya kingine kama ifuatavyo;-

  1. Technical talent - Hiki ni kipaji changu kikuu nikipendacho kuliko vyote. Ndicho kinachonilisha, kunivisha na kunifanya nionekane wa muhimu hapa duniani. Kipaji hiki kiligundulika nikiwa mdogo kabla hata sijaanza shule ambapo nilianza kujihusisha na mambo ya ufundi wa umeme na electronics lakini kadiri umri ulivyozidi kuendelea nilikutana na kitu kinaitwa computer wakati nipo darasa la 2 na kujikuta kipaji changu chote kikihamia katika computer ambacho ninakiendeleza hadi sasa as an IT TECNICIAN. Apart from being an IT TECHNICIAN mimi ni fundi wa kila kitu kuanzia useremara mpaka mabomba. Ninaweza kufanya kazi yoyote ya ufundi bila ya kuisomea.
  2. Voice talent - Hiki ni moja wapo ya vipaji vyangu vya ajabu ambacho huwa kinawashangaza watu wengi sana. Kipaji hiki kimenifanya niwe na uwezo wa kuimba sauti yoyote ninayoipenda hata iwe ya Rihanna au Jordin Sparks. Pia nina uwezo wa kuigiza sauti ya mtu yeyote nipendaye kuanzia kuongea kwake, kuimba hata kucheka. Pia nina uwezo wa kuiga sauti ya milio mbali mbali ya wanayama ikiwemo mbwa, paka na farasi.
  3. Acting talent - Hiki ni kipaji changu kingine cha ajabu nilichojaliwa ambacho mara nyingi huwa napenda kukitumia for fun. Nina uwezo wa kuigiza ikiwemo kuigiza jinsi mtu anavyotembea na mambo yote anayoyafanya. Nakumbuka nilipokuwa Sekondari mimi nilikuwa ni mwanafunzi pekee niliyeweza kuigiza karibu walimu wote matendo yao yote bila kukosea.
  4. Body flexibility - Katika watu ambao wamejaaliwa kuwa na miili ambayo iko flexible nadhani mimi ni mmoja wapo kwani mwili wangu uko flexible kiasi cha kujifunza body movements yoyote kwa urahisi na kwa haraka ikiwemo dancing, kung fu n.k
  5. Studying human's mind and actions - Kipaji hiki cha kusoma watu nilikigundua when I first fell inlove wakati niko darasa la tano baada kuweza kusoma mambo kadhaa kutoka kwa mpenzi wangu huyo wa kwanza. Baada ya kukigundua kipaji hiki nilikuwa nikikitumia kuwasoma wapendao kama wanapendana au la na pia kuwasoma wale mbao wako single na kujua ni watu gani wanaowazimia na wangependa wawe wapenzi wao. Baada ya kusoma phylosophy kipaji kimepanuka na kuongezeka kwani sasa ninaweza kusoma kila kitu kuanzia tabia hadi kile unachowaza.
  6. Writting - Pia nimejaliwa kipaji cha kuweza kuandika makala yoyote na ikavutia machoni pa watu ikiwemo poems, CV's na kadhalika.
  7. Cooking - Hiki ni kipaji ambacho kwa kweli huwa nasikia raha kila ninapokifanya. Ingawa mimi ni mtoto wa kiume nina uwezo mkubwa kupika vyakula mbali mbali ambavyo kwa kweli huwa vinawadatisha watu wengi.
  8. Predict the future - Hiki ni kipaji changu cha mwisho ambacho ni cha kurithi kutokana na kipaji hiki nimeweza kutabiri mambo mengi yatakayotokea ikiwemo mitihani n.k

Hivi ni baadhi ya vipaji ambavyo ninavyo. Ninaamini hapa jamvini kuna watu wenye vipaji tena kunizidi hata mimi. Lets share our talents together. Now tell me whats your talent?

Kulala.....na hapa nilipo nimelala
 
I can sing kwa kweli, najua na kila mtu akinisikia naimba huwa wananiambia kwa nn sitaki kuwa muimbaji,hata kanisani?
 
Saaana si kidogo......sinaga muda maalum wa kulala, any time tu naangusha!! Na ukitaka kunichokoza niamshe usingizini haijalishi ni saa ngapi......ni heri unipigie kelele kabla sijalala!!

Nikikuamsha usingizini utanifanyaje?
 
Back
Top Bottom