Tunalimiss sana soka staili ya samba!!

Tunalimiss sana soka staili ya samba!!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
14,191
Reaction score
19,115
Brazil waliingia mkenge kwa kuachana na staili ya soka lao la samba lenye burudani ya kufa mtu, linalowekeza kwenye vipaji na wakaiga soka la ulaya linalo-base kwenye mpira wa kibiashara zaidi kuliko burudani!!
Tusahau kuibuka na kuendelezwa kwa vipaji kama Pele, Maradona, Ronaldo og, Ronaldinho, Messi, nk.

Tunachoshuhudia jwa sasa ni soka la pass linalokwepa kukabiliana mtu kwa mtu. Kukabiliana mtu kwa mtu ndo hutoa nafasi ya kuonesha kipaji! Soka la leo ni kama draft-one touch! Kupigana chenga ni nadra sana, kuvushana kanzu ndo kabisa ni kama kaka kuona! Msimu unaweza kuisha bila kuona watu wakivalishana kanzu!!

Kwa kifupi soka kuwa biashara zaidi kulikoni burudani zaidi kumeharibu mambo!
 
Ndio maana tunakokwenda hakutakuwa na wababe wa soka! Soka la kufundishwa ndilo linalotawala! Heshima ya soka inahamia kwa makocha wa soka kuliko wana soka wenyewe! Kocha anamtaka mchezaji acheze kwa maelekezo zaidi kuliko kwa ufundi binafsi zaidi!
 
Soka la samba mchezaji ana uhuru wa kuchezea mpira kama anacheza ngoma vile!! chenga kwa saba tu na kuvishana kanzu! Yote hayo ni burudani kwa wachezaji wenyewe ba kwa watazamazi!! Tutupie clips hapa za soka staili ya samba!!
 
Kitu kikisha kuwa controlled tu hasa monetization kinakosa Radha. Huo mpira ulikuwa mpira hasa, Leo kama usemavyo hata mtu a kifanya hizo samba anaonekana boya, kana kwamba kafanya kujionesha
 
Mimi namiss sana tik taka ile ya Barca
 
Brazil waliingia mkenge kwa kuachana na staili ya soka lao la samba lenye burudani ya kufa mtu, linalowekeza kwenye vipaji na wakaiga soka la ulaya linalo-base kwenye mpira wa kibiashara zaidi kuliko burudani!!
Tusahau kuibuka na kuendelezwa kwa vipaji kama Pele, Maradona, Ronaldo og, Ronaldinho, Messi, nk.

Tunachoshuhudia jwa sasa ni soka la pass linalokwepa kukabiliana mtu kwa mtu. Kukabiliana mtu kwa mtu ndo hutoa nafasi ya kuonesha kipaji! Soka la leo ni kama draft-one touch! Kupigana chenga ni nadra sana, kuvushana kanzu ndo kabisa ni kama kaka kuona! Msimu unaweza kuisha bila kuona watu wakivalishana kanzu!!

Kwa kifupi soka kuwa biashara zaidi kulikoni burudani zaidi kumeharibu mambo!
Tele Santana kocha maarufu aliyefundisha kikosi cha Brazil 1982 na 1986 alikua muumin mkubwa wa samba. Aliwahi kuielezea falsafa ya soka la samba kwa kusema "Soccer ni sanaa. Samba ni kucheza mpira mzuri sana unaowafurahisha watazamaji, unatengeneza nafani na kufunga magoli"

Brazil ilipata mashabiki wengi dunia nzima kwa aina yake ya uchezaji ulioruhusu vipaji binafsi na ubunifu wa hali ya juu kabisa wa namna ya kucheza na kuuchezea mpira. Tangia enzi ya kina Pele, Garincha, Tostao, Carlos Alberto, kisha kina Careca, Alemao, Casagrande, Mullaer, Zico na baadae Kina Romario, Bebeto, Taffarel, Junior Baiano na miaka ya karibuni Kina Ronaldo OG, Ronaldinho, Rivaldo n.k Brazil ilikua inatoa burudani ya kutosha

Sasa hivi Brazil inacheza mtu unasinzia! Kilichowafikisha hapa ni kuacha aina yao ya uchezaji na kuiga ile ya Ulaya. Lakini utawalaumu vipi wakati wazungu wanatia hela? Mchezaji akichipukia kidogo tu kashafatwa na ma ajenti wa timu za Ulaya kwa dau la kufuru na huku aendako anaenda kuelekezwa kucheza mpira wa takwimu zaidi na kupoteza asili ya uchezaji wao
 
Vini Jr, ni kama anataka kubaki kwenye samba, lakini inashindikana. Hawa Brazil itawachukua miongo mingi sana kushinda kombe la dunia.
 
Back
Top Bottom