What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

Wakati mwingine tunafikiri wapinzani ni dawa ya matizo yetu kumbe si kweli ukimya wa Halima Mdee kwenye tatizo letu la Madale hakika nimeushangaa sana.

Hahaha wewe kila Siku tunakujua ni gamba gumu sasa Leo unapodai wewe ni mpiga kura wa Halima ndio nimegundua wewe ni janga la maendeleo tz, inapoteza muda kujaza thread ukute Hata madale hupajui
 
Nilikuwa na imani kuwa wabunge wa upinzani ni wabunge mbadala. Mimi ni mmoja wa waathirika wa bomoa bomoa ya Madale ambayo kuna kila aina ya ujanja ujanja lakini tangu tupate matatizo hayo sijawahi kuona mbunge wangu HALIMA MDEE akisema lolote au hata kuwatembelea waathirika kujua shida zao na namna ya kuwasaidia kwani ni wapiga kura wake.

wapo wanaolala nje hadi sasa, wapo walionyang'angwa ardhi kwa nguvu ya fedha lakini Halima ambaye ni mjumbe wa baraza la madiwani la Kinondoni nilitegemea angekuwa na kauli ya kutueleza wananchi tulioathirika na bomoa bomoa hiyo katika eneo la Madale nakalekwa, madale tuaroho na madale nakasangwe. Ni zaidi ya mwezi sasa tangu kupita kwa bomoa bomoa hiyo.

Halima anajua ukweli kwa sababu yuko kwenye vikao vya manispaa ya kinondoni lakini pia niliambiwa kasomea sheria ( i stand to be corrected) ni sheria ipi inaruhusu kumnyang'anya mwananchi aliyekaa eneo kwa miaka kumi bila kuendelezwa hao wamiliki halali akina Michael Chacha na wenzake walikuwa wapi miaka yote. Sheria inatoa miaka mitatu tu kwa ardhi ambayo haijaendelezwa kunyang'anywa au kuwa mali ya yule anayelindwa na sheria hiyo kwa maana kwamba kama mwananchi ameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu bila mmiliki halali kutokea sheria inatambua na kumpa umiliki yule aliyopo kwa wakati huo.

My take: Halima Mdee acha kukimbilia kigamboni kuwalilia wananchi wake kutokakana na hofu ya mji mpya anza na jimbo lako. Bado tunakusubiri uje kuongea na sisi wananchi wa Madale ingawa umechelewa.

source: Mimi mwenyewe nilikuwa na kiwanja cha nusu heka Madale.

Sijui nia yako ni nini! Mbunge Halima ni imara, jitahidini kufuata sheria.
 
Kwa wale wasioijua hii sakata ya madale ipo hiviiii... Tukiacha siasa na uchama!!
Hawa wavamizi bana wakijakwenye eneo lako hawajalishi ulisha liendeleza kwa vipi. Wao wakifika kama niwewe au ni mlinzi wanampiga mapanga na mkewe na watoto wakiwepo wanabakwa nawanataifisha mali zote wanazokuta hapo kwako. Unfortunately ukiripoti kwapolisi Wazo back then kabla ya huyu OCD wa sasa hajaja wanakwambia hukohawawezi kwenda kwani kunahitajika operesheni maalum na wale watu ni wengi nawana silaha za jadi!Hivyo cha kufanya ni kufungua tu RB unakaa nayo ukisubirihiyo operesheni maalum.
Hayo yametokea in between 2007-2011, alipokuja huyu OCD mpya ndo yakaanzakupungua. Yule aliekuwepo alidiriki kuweka matangazo Polisi Wazo kuwahawasikilizi matatizo na migogoro ya ardhi na yeyote mwenye hayo matatizo aendebaraza la ardhi. Na tiba kwa waliotaifishwa mali zao ikawa ni kufungua RB tubasi.
Sasa basi wakisha taifisha hiyo mali yako na kusikia umeenda kwenye baraza laardhi kufungua kesi, wao wanabomoa any structure uliyo erect kwenye hilo eneo lakona kama una miti wanaikata yote na kama una mifugo wanachinja na kuila yote(kama hawataiuza!) na mwisho wa siku wanaanza kukomaa kwamba wamekuta poriwamelisafisha na kuanzisha makazi!! Kibaya zaidi wanatumia yaleyale materialkutoka kwenye nyumba zako na miti yako kujengea vibanda vidogo vidogo kuzungukaeneo lako lote.
Kama kwamba hiyo haitoshi.. ukionekana tena kwenye hilo eneo lako kama wewe nimwanamme utatekwa na kupewa kipigo kitakatifu ikiwemo na kupigwa mapanga e.gMwanasheria wa Manispaa ya kinondoni yaliyomkuta Mr. Mahenge. na kama nimwanamke utabakwa na virusi wakuachie!
Kuna familia moja ya baba, mama na mtoto wao wa kike wa miaka 5 walikwendakwenye eneo lao kama mwezi mmoja uliopita na ukiacha kipigo alichopata babavile vile walimlawiti mbele ya mkewe na mwanawe na mama akabakwa na mtoto waowa kike only 5 yrs old alibakwa na hao wavamizi na kuharibiwa kizazi kabisa.God have mercy! Hiyo familia ipo na ukitaka muulize OCD wa Kawe Mr Muroto kwasimu no. +255767190990. Bado wapo hospitali.
Baada ya hii operesheni hata matukio ya ujambazi na uporaji maeneo ya Tegeta,Boko, Bunju na majirani zao yamepungua sana. Hii ni ripoti ya OCD kawe kwendakwa wahanga wa uvamizi.
Kuna mama anaitwa Anna Hangaya au Anna Luvanda aka Mama Makete. Yeye nimwenyekiti wa UWT wilaya ya Kinondoni na yeye ndo mfadhili mkuu wa hawawavamizi. Na analo genge lake la kufanya huu uovu mchana kweupee na nnashangaani kwa nini hachukuliwi hatua. Huyu mama ukiacha kwamba ni mvamizi kwenye eneola mzee Chacha lililopo Nyakasangwe, lenye hati miliki no. 45968. Ni mmiliki wamalori ya kubeba vifusi, kokoto na mawe kama anavyokiri mwenyewe kwenye gazetila Tanzania Daima la tarehe 3 Sept, 2012 uk. 4.
Huyu mama na genge lake hilo kwa sasa wamevamia maeneo yote yenye mawe nakifusi huko Nyakalekwa, Nyakasangwe na boko magereza na kwa habari isiyo rasmini kwamba anasupply hivyo vifusi na mawe kwenye ujenzi wa barabara yaMwenge-tegeta. Na hayupo tayari kuyaachia hayo machimbo yanayomsupply materialsfree of charge.
Kwenye mkanda wa mauaji ya mabaunsa huyu mama na genge lake hilo anaonekanalive akitoa command na kuhamasisha genge lake hilo wawauwe hao mabaunsa angalauhata mmoja siku hiyo. Na kweli mabaunsa wawili walikufa bila hatia yoyote kwanihawakupiga wala kujeruhi mtu yeyote siku hiyo.

Sera ya bomoa bomoa Manispaa ya Kinondoni ambayo inayoongozwa na Meya wa CCM sasa imehamia kwenye Jimbo la Uchaguzi la Kinondoni kwa Mh. Iddi Azzan baada ya kutoka Jimbo la Kawe.

Jana wakazi wa Sinza Mori na Bamaga walibomolewa nyumba zao. Zoezi hilo lililoacha simanzi, majonzi na vilio kwa wakazi hao, limefanyika jana na kushuhudiwa na kamera ya mwandishi
attachment.php

Greda likijiandaa kuanza kazi!

4.JPG

Wananchi wa Sinza wakijaribu kuokoa mali zao kabla Greda halijapitia

11.jpg

Wanamgambo wa Halmashauri wakisimamia zoezi
attachment.php

Greda likivunja Geti la Nyumba

(Habari /Picha : Haruni Sanchawa, GPL)

Tutaona kama watamwandama mbunge wa CCM wa Kinondoni kama wanavyomwandama Mdee.
 
Fikiria jinsi ya kutatua matatizo yako kabla ya kumtafuta Halima Mdee,haiwezekani kila mwananchi mwenye shida
aanze kufikiria mbunge yuko wapi,mbunge si dawa ya matatizo yetu.
 
mm nafikiri kama wananchi tunapaswa kuwa makini. haiwezekani ww ukauziwa na mtu anayedai mmiliki pasipo ushahidi usio na shaka. ukinunua kiwanja kwa mwizi huwezi kuwa mmiliki halali kwani aliyekuuzia hana umiliki halali

wakati mwingine tulaumiane wananchi, mm mwenyewe nina viwanja maeneo yasiyo rasmi, nilifanya yafuatayo-
1. nilifuatilia kujua uhalali wa mmiliki
2. nilihakikisha tunasainiana mkataba kuwa kama amenificha basi atanirudishia gharma zangu na za maendelezo
3. nilifuatilia kujua nyumba yake binafsi anayoishi, siyo ya kupanga
4. nilisaini mkataba na mmiliki kwa wakili

pia ni vizuri kujua ramani ya jiji na mpango wa serikali. usipojua hata kama CUF itaingia madarakani hata baada ya miaka 50 au 100 watakaokuwa hai serikali itatekeleza mpango wake

hata mbunge akitaka kutoa kauli ktk mazingira haya sio salama kwake kwani anaweza kuzushiwa na kucafuliwa kuwa anahimiza wananchi kukiuka sheria. sheria ni kwa wananchi wote
 
ACHA UJINGA WEWE,uvamie maeneo ya watu kwa ujinga wako alafu umlalamikie halima?usitegemee msaada kwa ujinga wako na halima hayuko kutetea maovu na kura usimpe kama unatabia ya kuiba vya watu ukitegemea kuna mtu wa kukutetea,usipoteze muda wako kumsubili mbuge kwa upuuzi wako na ukome maana uko mmezidi kuvamia maeneo ya watu,ulivamia ukisubili hiyo sheria ya mwaka 47 pole na umkome mbunge wetu na uvae gamba tuje tukuchome moto

wataje unaosema watu halali mbona hawawekwi hadharani inaonyesha unawajua kwa kina na umiliki wao halali
 
Halima ni very bogus
anariinga utasema haihitaji tena kura

wenzie kina Zitto na Mnyika wako humu
ukiwa na shida nao una wa pm tu
yeye hata ukim add facebook full maringo
mimi nakaa tegeta
nalazimika kumtuma Zitto au Ester Bulaya
wampe ujumbe Halima
simpi kura yangu tena
 
f
mm nafikiri kama wananchi tunapaswa kuwa makini. haiwezekani ww ukauziwa na mtu anayedai mmiliki pasipo ushahidi usio na shaka. ukinunua kiwanja kwa mwizi huwezi kuwa mmiliki halali kwani aliyekuuzia hana umiliki halali

wakati mwingine tulaumiane wananchi, mm mwenyewe nina viwanja maeneo yasiyo rasmi, nilifanya yafuatayo-
1. nilifuatilia kujua uhalali wa mmiliki
2. nilihakikisha tunasainiana mkataba kuwa kama amenificha basi atanirudishia gharma zangu na za maendelezo
3. nilifuatilia kujua nyumba yake binafsi anayoishi, siyo ya kupanga
4. nilisaini mkataba na mmiliki kwa wakili

pia ni vizuri kujua ramani ya jiji na mpango wa serikali. usipojua hata kama CUF itaingia madarakani hata baada ya miaka 50 au 100 watakaokuwa hai serikali itatekeleza mpango wake

hata mbunge akitaka kutoa kauli ktk mazingira haya sio salama kwake kwani anaweza kuzushiwa na kucafuliwa kuwa anahimiza wananchi kukiuka sheria. sheria ni kwa wananchi wote

hatusemi halima aje kutengua maamuzi ya bomoa bomoa bali aje kutusikiliza hata mahakamani wahalifu husikilizwa na wakati mwingine wanashinda kesi dhidi ya dhuluma
 
f

hatusemi halima aje kutengua maamuzi ya bomoa bomoa bali aje kutusikiliza hata mahakamani wahalifu husikilizwa na wakati mwingine wanashinda kesi dhidi ya dhuluma
MAMA POROJO:

Operesheni ya kuwaondoa wavamizi wa mashamba iliyoanza jana saa 12 asubuhi, ilifanywa na Serikali ya Wilaya ya Kinondoni chini ya ulinzi mkali wa askari polisi waliokuwa na magari yapatayo 30 yakiwamo matingatinga manne na gari la wagonjwa. Jumla ya nyumba 300 zabomolewa Mabwepande. | Dullonet Tanzania

Mmebomolewa na Halmashauri inayoongozwa na Meya wa CCM na madiwani wa CCM ndio majority!
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema wametumia nguvu ya wastani katika kusimamia operesheni hiyo na watu takribani 20 wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kuanzisha vurugu. "Tulipata upinzani kidogo wakati tunaanza, jambo ambalo tulilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya na kuendelea na kazi hiyo. Kazi imefanyika vizuri na hakuna askari wala raia yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa," alisema Kamanda Kenyela ambaye katika awamu ya pili ya bomoabomoa, alitaka kusiwapo na uchomaji moyo nyumba zilizobomolewa. Source Habari Leo Jumla ya nyumba 300 zabomolewa Mabwepande. | Dullonet Tanzania

Wakati wa bomoa bomoa policcm walikuwepo kusimamia!

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alisema eneo hilo limekuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na kuwa kazi waliyoifanya ni kuwaondoa wavamizi wapya katika eneo hilo lililovamiwa la kata za Mabwepande na Madale.
"Mgogoro wa hapa ni tofauti, zamani kulikuwa na tatizo la umilikaji wa watu zaidi ya mmoja katika eneo moja, lakini sasa kuna kundi la vijana ambao wanavamia maeneo ya watu na baadaye wanayauza, wengi wa waliobomolewa ni wale waliouziwa na wavamizi," alisema Rugimbana.

Na Mkuu wa Wilaya, ambaye ni mwakilishi wa Rais eneo hilo aliafiki.

Hivi kwa nini hauoni role ya CCM katika kitu chote hiki unatafuta mbuzi wa kafara (scapegoat) in Halima Mdee?
 
MAMA POROJO,

Maneno yako mekundu hayakutoka moyoni, ni unafiki.
Nilikuwa na imani kuwa wabunge wa upinzani ni wabunge mbadala. Mimi ni mmoja wa waathirika wa bomoa bomoa ya Madale ambayo kuna kila aina ya ujanja ujanja lakini tangu tupate matatizo hayo sijawahi kuona mbunge wangu HALIMA MDEE akisema lolote au hata kuwatembelea waathirika kujua shida zao na namna ya kuwasaidia kwani ni wapiga kura wake.

wapo wanaolala nje hadi sasa, wapo walionyang'angwa ardhi kwa nguvu ya fedha lakini Halima ambaye ni mjumbe wa baraza la madiwani la Kinondoni nilitegemea angekuwa na kauli ya kutueleza wananchi tulioathirika na bomoa bomoa hiyo katika eneo la Madale nakalekwa, madale tuaroho na madale nakasangwe. Ni zaidi ya mwezi sasa tangu kupita kwa bomoa bomoa hiyo.

Halima anajua ukweli kwa sababu yuko kwenye vikao vya manispaa ya kinondoni lakini pia niliambiwa kasomea sheria ( i stand to be corrected) ni sheria ipi inaruhusu kumnyang'anya mwananchi aliyekaa eneo kwa miaka kumi bila kuendelezwa hao wamiliki halali akina Michael Chacha na wenzake walikuwa wapi miaka yote. Sheria inatoa miaka mitatu tu kwa ardhi ambayo haijaendelezwa kunyang'anywa au kuwa mali ya yule anayelindwa na sheria hiyo kwa maana kwamba kama mwananchi ameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu bila mmiliki halali kutokea sheria inatambua na kumpa umiliki yule aliyopo kwa wakati huo.

My take: Halima Mdee acha kukimbilia kigamboni kuwalilia wananchi wake kutokakana na hofu ya mji mpya anza na jimbo lako. Bado tunakusubiri uje kuongea na sisi wananchi wa Madale ingawa umechelewa.

source: Mimi mwenyewe nilikuwa na kiwanja cha nusu heka Madale.

Nimechukua muda kidogo kuangalia posts zako za zamani. Baadhi ya nilizoona ni hizi:

mtabeba na makapi mwaka huu katika 22 mmewachuja kuona wanafaa???? kisa kuikomoa CCM.

Huu ndio msimamao wa chama chako hata CCM ikifanya zuri ndio jukumu la upinzani wala haishangazi.

Tupe ushahidi kwamba wamelipwa????????????? unaweza kuficha fidia ya watu wengi kiasi hicho!!!! ni siri gani hiyo ya watu wengi hivyo???

bad language.... uko upande wa chadema na ndio maana unasilikiza na kuamini ya upande mmoja tu

Mimi naona ccm na nuru tororo ..... Ni mtazamo wangu tu.

Nimefurahishwa na bango lako la wino wa kijani ni rangi ya CCM

Nimeelewa kwa nini lawama zote unamtupia Halima Mdee, na huoni kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda CCM, kuwa ndiye aliyetuma wabomoaji na askari.

Ndio maana kwenye thread hii umekazana kujaza lawama dhidi ya Halima Mdee.

Siasa za kupakana matope hazilipi MAMA POROJO!
 
Safi sana mkuu naona sasa nilichokuwa nasema kimeeleweka na watu wameona kuwa porojo zake zinasababishwa na nini?

Nilikuwa na tafuta post moja hivi aliweka kipindi cha vurugu za sindiga kwenye mkutano wa cdm zina ushahidi wa unafiki wake ngoja nizitafute.
MAMA POROJO,

Maneno yako mekundu hayakutoka moyoni, ni unafiki.

Nimechukua muda kidogo kuangalia posts zako za zamani. Baadhi ya nilizoona ni hizi:

Nimeelewa kwa nini lawama zote unamtupia Halima Mdee, na huoni kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda CCM, kuwa ndiye aliyetuma wabomoaji na askari.

Ndio maana kwenye thread hii umekazana kujaza lawama dhidi ya Halima Mdee.

Siasa za kupakana matope hazilipi MAMA POROJO!
 
nyie hamjajua tu, ila ukweli ni kwamba wabunge wanawake hawana uwezo wa kuwakilisha jimbo. Nafasi sahihi kwa wanawawe ni ubunge wa viti maalum. Mdee alikuwa viti maalum ghafla mkamkabidhi jimbo kitu ambacho yeye haoni kama ni dili sana kwake. Yeye kugombea kawe ilikuwa shinikizi la chama chake na walikuwa hawategemei ushindi ndio maana walikuwa wamesha mtengea nafasi yake ya viti maalum aliyoizoea na ambayo yeye anaimudu kwani anakuwa hana majukum kijimbo ila kichama tu.

nani kakwambia jinsia ndiyo inaongoza jimbo?
Watu tunaangalia huwezo wa mtu sio jinsia! Kumbe kuna watu bado mnaitaji elimu kuondokana na mawazo mgando kama hayo.
Jaribu kufikiri kwa kina.
 
nani kakwambia jinsia ndiyo inaongoza jimbo?
Watu tunaangalia huwezo wa mtu sio jinsia! Kumbe kuna watu bado mnaitaji elimu kuondokana na mawazo mgando kama hayo.
Jaribu kufikiri kwa kina.
Sawa Mr Bright, Mie naona kama kuna mtu anahitaji kufundishwa udhaifu wa mwanamke katika nyadhifa za uongozi ni wewe. Mwanamke ameubwa kutoka ubavuni mwa mwanaume. Mwanamke ana kazi anazoziweza na si zote. Ebu kwa uelewa wako nitajie mbunge yeyote wa chama chochote hapa bongo mwanamke unayeona ana qualify kuwa kiongozi.
 
mm nafikiri kama wananchi tunapaswa kuwa makini. haiwezekani ww ukauziwa na mtu anayedai mmiliki pasipo ushahidi usio na shaka. ukinunua kiwanja kwa mwizi huwezi kuwa mmiliki halali kwani aliyekuuzia hana umiliki halali

wakati mwingine tulaumiane wananchi, mm mwenyewe nina viwanja maeneo yasiyo rasmi, nilifanya yafuatayo-
1. nilifuatilia kujua uhalali wa mmiliki
2. nilihakikisha tunasainiana mkataba kuwa kama amenificha basi atanirudishia gharma zangu na za maendelezo
3. nilifuatilia kujua nyumba yake binafsi anayoishi, siyo ya kupanga
4. nilisaini mkataba na mmiliki kwa wakili

pia ni vizuri kujua ramani ya jiji na mpango wa serikali. usipojua hata kama CUF itaingia madarakani hata baada ya miaka 50 au 100 watakaokuwa hai serikali itatekeleza mpango wake

hata mbunge akitaka kutoa kauli ktk mazingira haya sio salama kwake kwani anaweza kuzushiwa na kucafuliwa kuwa anahimiza wananchi kukiuka sheria. sheria ni kwa wananchi wote

Ni kuanzia lini wabomoaji ndio wanathibitisha umiliki au wewe hapa JF ndiye unathibitisha umiliki??????????

Je wewe hujawahi kuona au kusikia mahala popote ambapo wananchi waliobomolewa walionewa?????

kwa nini hutaki Halima Mdee akutane na wapiga kura wake ama kwa kuwaeleza kosa lao au umiliki wao???

Kimya cha Mdee kinaashiria jambo moja tu ana jibu la bomoa bomoa kwa nini hajaenda hata kuwapa pole????

Wananchi wanamtaka mbunge je ni kosa??
 
Halima Mdee ni mmoja wa wabunge vijana na wasomi ni kwa nini hajiungi JF kama wengine kutuma majibu ya haya malalamiko???? Je haoni thamani ya mitandao ya kijamii kwa maendeleo ya ubunge wake????
 
Tunajuaje pengine wakazi waliobomolewa wana imani na Mdee hata kama waliobomoa ni viongozi????

Imani kwa kiongozi sio lazima iwe ni imani kwa chama anachotoka.

Dk. Mwakyembe, Hamis Kagasheki na Pombe Magufulu kuna watu nje ya CCM wanafutiwa na utendaji wao.

Sio jambo la ajabu kwa wakazi walioathirika kumtaka Mdee.
 
Mwanaukweli,

Kumbuka hata Dk. SLAA alikuwa CCM na Wassira alikuwa CCM akaenda NCCR na kurudi CCM unataka kusema msimamo wa namna huo hatuhitaji kuwasikiliza viongozi hao ni wanafiki na waongo????

Msimamo wa mtu kwenye jambo moja hauwezi kuathiri jambo la pili kama msimamo huo unajengwa kwenye hoja mbili tofauti na zisizolingana.

Tazama hoja..... naweza kusema vizuri juu ya kiongozi leo lakini naweza kusema vibaya kwa kiongozi huyo huyo siku za mbele kutokana na hoja iliyoko mbele yetu. Historia ya kiongozi haiwezi kuwa kigezo pekee kinachotuongoza kumchambua kiongozi kama tunavyofanya kwa Mdee na jinsi alivyowatosa wakazi wa madale
 
Back
Top Bottom