What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

Mkuu unamaana kile kighorofa alichootesha amepora kiwanja?
baada ya kile kigorofa kuna uwanja wa mpira. Familia ya diria ilijaribu kusema kile kiwanja ni chao ikashinda. Wkend iliyopita akishirikiana na ffu alizungushia uzio ule uwanja wote kwa siku moja, kama alivyofanya yule jamaa wa kituo cha bus pulm beach
 
Kawe ni jimbo lenye matatizo mengi hasa ya ARDHI..mdee amejitahidi kushirikiana na watu wa mazingira kulinda fukwe na wavamizi wa mito maeneo ya beach na pia anaendelea kuhamasisha mipango ya maendeleo mingi tu...
 
Labda wabomoaji wa madale wakishamaliza kule,breki ni huo uwanja wa jogoo,let us wait and see!
 
Mara ya mwisho nilimuona Halima Mdee, kwenye maandamano ya Mwanza amejipamba utadhani anakwend kwenye harusi, unaenda salon kusuka rasta unapaka na rangi ya mdomo halafu unaingia kwenye maandamano, halafu unasema unataka kuwakomboa wana Kawe.

Mkuu Ritz,
Hao ndio makamanda wanaongoza vita wakati makamanda wengine kina molemo hata deodorant za kupaka kwenye kwapa hawana makamanda wanaopigania usawa wakati hata ndani ya Chadema yenyewe usawa hakuna!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mh mbunge wetu wa wa jimbo la kawe Halima Mdee, tafadhali sikia kilio chetu cha upatikanaji wa maji huku Bunju B viwanja vya mradi 20,000.

Jitahidi kuacha porojo zilizo na maneno mengi mno na kuandika makala na majibu marefu, "your actions should speak louder than empty words...."
 
tunakuomba mheshimiwa mbunge kupitia tiketi ya CHADEMA katika jimbo la KAWE HALIMA MDEE timiza ahadi kwanza zako katika jimbo la kawe kwani matatizo ni mengi mno kuliko hayo unayokomalia . hivi nyumba zinazokufanya ukutane na matajiri wenye hizo nyumba zinawasidia nini wananchi masikini wa kawe wenye matatizo kibao maana umekomalia kwenye hizo nyumba as if zitahama leo au kesho . nyumba zipo wala hazihami maliza kwanza matatizo makubwa ya wananchi wa jimbo lako . shule ,shida, maji ,umasikini, uwanja wa tanganyika packers . tulikuchagua sio kwa ajili ya nyumba ya nyumba zilizojengwa ufukweni mwa bahari ingawa tunajua huko utafaidika kuliko kwa wananchi masikini. lakini maliza kwanza matatizo yao harafu hizo nyumba zito tu utaendelea nazo baadae wewe si mbunge au una wasiwasi na uchaguzi ujao ukitoka na deal litakuwa limeyeyuka ?
 
Nilikuwa na imani kuwa wabunge wa upinzani ni wabunge mbadala. Mimi ni mmoja wa waathirika wa bomoa bomoa ya Madale ambayo kuna kila aina ya ujanja ujanja lakini tangu tupate matatizo hayo sijawahi kuona mbunge wangu HALIMA MDEE akisema lolote au hata kuwatembelea waathirika kujua shida zao na namna ya kuwasaidia kwani ni wapiga kura wake.

wapo wanaolala nje hadi sasa, wapo walionyang'angwa ardhi kwa nguvu ya fedha lakini Halima ambaye ni mjumbe wa baraza la madiwani la Kinondoni nilitegemea angekuwa na kauli ya kutueleza wananchi tulioathirika na bomoa bomoa hiyo katika eneo la Madale nakalekwa, madale tuaroho na madale nakasangwe. Ni zaidi ya mwezi sasa tangu kupita kwa bomoa bomoa hiyo.

Halima anajua ukweli kwa sababu yuko kwenye vikao vya manispaa ya kinondoni lakini pia niliambiwa kasomea sheria ( i stand to be corrected) ni sheria ipi inaruhusu kumnyang'anya mwananchi aliyekaa eneo kwa miaka kumi bila kuendelezwa hao wamiliki halali akina Michael Chacha na wenzake walikuwa wapi miaka yote. Sheria inatoa miaka mitatu tu kwa ardhi ambayo haijaendelezwa kunyang'anywa au kuwa mali ya yule anayelindwa na sheria hiyo kwa maana kwamba kama mwananchi ameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu bila mmiliki halali kutokea sheria inatambua na kumpa umiliki yule aliyopo kwa wakati huo.

My take: Halima Mdee acha kukimbilia kigamboni kuwalilia wananchi wake kutokakana na hofu ya mji mpya anza na jimbo lako. Bado tunakusubiri uje kuongea na sisi wananchi wa Madale ingawa umechelewa.

source: Mimi mwenyewe nilikuwa na kiwanja cha nusu heka Madale.
 
Bado Kesi iko mahakamani lakini tumebomolewa nyumba na kunyang'anywa ardhi tulitegemea mbunge ungekuja kusaidia namna ya kutafuta haki mahakamani lakini uko kimya. Wananchi masikini wamefungua kesi lakini kabla ya hukumu tumeondolewa kwa nguvu.
 
Bado Kesi iko mahakamani lakini tumebomolewa nyumba na kunyang'anywa ardhi tulitegemea mbunge ungekuja kusaidia namna ya kutafuta haki mahakamani lakini uko kimya. Wananchi masikini wamefungua kesi lakini kabla ya hukumu tumeondolewa kwa nguvu.

Anza na CCM kwanza kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kua atakapotoa kauli tu, Bunge litasimama na kusema suala liko mahakamani......
 
Wakati mwingine tunafikiri wapinzani ni dawa ya matizo yetu kumbe si kweli ukimya wa Halima Mdee kwenye tatizo letu la Madale hakika nimeushangaa sana.
 
Wavunje CCM halafu wana CCM wadai Chadema iwatete...siasa hizi za masiku haya,khaaa!Kwani walijenga kwa vibali vya manispaa?
 
Wakati mwingine tunafikiri wapinzani ni dawa ya matizo yetu kumbe si kweli ukimya wa Halima Mdee kwenye tatizo letu la Madale hakika nimeushangaa sana.

Dawa ya matatizo yetu haiko kwa chama tawala pia....let alone wapinzani. Tunayo wenyewe as individuals kama tutaamua.
 
MAMA POROJO, ni vema ukarekebisha jina la mbunge wako, km inawezekana. Ni Halima, si Harima. Na naona siku hizi punctuation marks hazina maana tena, au ndio dotcom world!? Compare: Halima Mdee na halima mdee.
 
Last edited by a moderator:
Nusu heka madale ndio unalalamika njoo Mpiji Majoe tukupe 1 heka.

kama unaweza kunirudishia fedha yangu ndio inafanya niseme hayo ardhi naweza kupata popote lakini hakuna fidia kwa ujanja janja. Kauli ya Halima Mdee ingekuwa na mwongozo yeye ni mbunge wa wote bila kujali chama so far sheria inamtambua hivyo.
 
Back
Top Bottom