Madiwani 22 CCM Misungwi wajiandikisha kuhamia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani 22 CCM Misungwi wajiandikisha kuhamia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Jul 11, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Madiwani 22 wa CCM wa wilaya ya Misungwi (mkoa wa Mwanza) wamejiorodhesha na kutishia kutaka kuhamia CHADEMA kutokana mgogoro uliopo kati yao na viongozi wa CCM wilaya, Tanzania daima leo limeripoti. Uamuzi huo unatokana na Kamati ya siasa ya Mkoa na wilaya kumshinikiza Mkiti wa Halmashauri hiyo Mr Benard Policarp kujivua gamba kutokana na tuhuma za ufisadi wa fedha umma.

  Hata hivyo, madiwani 22 kati ya 36 hawakubaliani na kamati hizo za siasa kwa madai kuwa uchunguzi wa kina ufanyike kwanza, ndipo uamuzi wa kumshinikiza M/kiti wao ajiuzulu ufuate, kwa kuwa hakuna uthibitisho uliopatikana dhidi yake hadi sasa. kwa mujibu wa taarifa hizo, ambazo zimethibitishwa na baadhi ya madiwani hao, tayari wamekwishajiorodhesha na kata wanazotoka na wamedhamiria kuipeleka majina yao makao makuu ya CCM.

  Leo (jana) madiwani hao walitaka kuandamana kudai mali zao walizokuwa wakichangia Chama hicho lakini walikwama baada ya magari ya FFU kuzagaa kwa lengo la kupambana nao.

  Mmoja wa madiwani hao (gazeti laficha jina) alisema muda wo wote watahamia Chadema kuanzia sasa.

  Chanzo cha mtifuano.
  Ripoti ya CAG ilionesha kuwa halmashauri hiyo ilikuwa na ripoti mbaya ikionesha ufisadi wa Bil 5. Waziri mkuu Pinda aliagiza mkurugenzi ashushwe ( + jirani wa sengerema) wote wameshushwa vyeo.

  Baada ya hapo viongozi wa CCM (wilaya + mkoa) kupitia kamati za siasa wakahamisha bifu kwa m/kiti wa Halmashauri hiyo bila ushahidi wo wote, hata hivyo madiwani 22 kati ya 36 wakaamua kumkingia kifua ikibidi kwa gharama ya kuhama naye kwenda CHADEMA kutetea haki yao mpaka uchunguzi wa kina ufanyike kwanza.

  My take;
  Kama bifu linaanza mapema namna hii, kura ya maoni ya ndani ya CCM 2015 itakuwaje?
  Pili, hivi Chadema isingekuwa na nguvu wangeweza kuwa na ujasiri huo walio nao sasa?
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  still puzzle....
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu rebebisha hapo "mwanzo"sijui ulimaniisha nini
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Bado ni tetesi tu hizo
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Hali ndiyo hii, lakini watu wenye akili ndogo wanafikiri suluhisho ni kumuua Dr Slaa!
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mtabeba na makapi mwaka huu katika 22 mmewachuja kuona wanafaa???? kisa kuikomoa CCM.
   
 7. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tulia hapo hapo penye red, ndio patamu.
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  tetesi tu.
   
 9. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wasitumie CDM kama kichaka chao cha kutishiana. Kama wanataka kuhama, wahame, sio kuitumia CDM kutishia... pambaf
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Taarifa ya Tanzania daima.... gazeti la chama kilekile wanachodai kutaka kuhamia tunahitaji chanzo kingine zaidi ya hicho kimoja
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nashauri tuache kupokea hawa wanafiki kutoka CCM, ndio wanatusumbua kama Mzee wa ujira wa mwiha.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  well said,

  chadema wanapiga vita ufisadi na madiwani hao wanamtetea mtuhumiwa wa ufisadi,,,,, wao (CDM) wanafurahi kupata kundi kubwa la madiwani hao...... siasa bana.
   
 13. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Mkuu ahsante kwa taarifa, kwa vile siasa za CCM ni kulinda mafisadi, huko tuendako tutaona mengi kwa maaana watu wamechoka kudhulumiwa!!!!

   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  madiwani wanaowapokea chadema wanamtetea fisadi anayefukuzwa na CCM
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  john shibuda = madiwani 22
   
 16. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ugomvi ukiisha je? Hawana dhamira hao!
   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180

  Kwani CDM wamewaita si wanataka wenyewe kuhamia CDM, KWA VILE WAMEISHA ONA CHAMA CHENYE MWELEKEO WA KUIKOMBOA TANZANIA NI CHADEMA!!!VIVA CDM VIVA UKOMBOZI WA MTANZANAI!!!!

   
 18. h

  hans79 JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Mwenye dhambi husamehewa na pia chema hujiuza.Refa anapeta tu go on CHADEMA.Utabaki pekee kwenye tanuli la moto.
   
 19. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Habari za kutungwa.
   
 20. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mamaporojo naona umechangia sasa, inatosha, hebu tuwasikie na wengine kama hutajali.
   
Loading...