What do you wish for 2019 Christmas?

I like your spirit Homie, hapo tuko pamoja bin bega kwa bega.

Mahaba robo tatu kwako vile wewe ni binamu yangu.... Ila shemeji yako Babu Asprin asisikie eehehehehe
Mimi nshakuwa kiziwi, sijasikia.

Wivu sina ila roho imeuma sana yani
 
Upendo, Amani na Pesa.

Nakuombea upate yote hayo kwa kadiri ya uhitaji wako...
Kwa asilimia kadhaa yako ndani ya uwezo wako kwa kuweka Kia na bidii kwenye shughuli zako ili zilete matokeo ya matamanio yako.
 
Mimi nshakuwa kiziwi, sijasikia.

Wivu sina ila roho imeuma sana yani


Aahahahahhahaaa Babu big Sam, nataka ku book seccond sleeping TRC twende zetu milimani kwa style yetu safari hii, tukishuka natema mate kwa kushiba mikate inayojazwa kwenye shimo la panya.....aaahhahahahahahahahahahaaaaa

Waalah hizi bangi kanivutisha Mentor sijui yuko wapi eehehehehehheeee.

Wajua vile nakumahaba na kukumalabuku hakuna kati michepuko yako unakaribia kwa haba na haba nnalokupa...

Mmuaahh!!
 
Ooh Nkundwe, polee umenifanya nisikitike nawe. Usijali kama hutawahi mwaka mpya basi natumai panapo uzima utajumuika na mama msimu wa Pasaka.

Umenifanya nikumbuke wakati niko chuo safari moja nikaenda kula Xmas na boifrendi ndo ilikuwa Xmas yangu ya kwanza kuwa mbali na nyumbani.... Na tulisafiri masafa marefu mbali na bongo nilikiwa naogopa... What if tukitekwa, tukipata ajali... Nilikiwa kadogoo halafu very innocent yaani.

Though niliinjoi sana kumbe boifrend alikuwa ananipa bata la kuniaga anaenda kuoa looh sina hamu wanaume nyie....
😄😄😄 Wanaume sisi wabaya sana.
 
Holla,

Msimu wa sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya ndo umeingia.

Sijajiunga na kifurushi chochote cha kimiminika ila nasikia tuu ulimi unataka kutereza kimalkia. Ngoja nishindane nao, ila kichwa cha uzi kitabaki hivyo hivyo, laah nikifika mwisho naweza kubadili lugha.

Haya twende pamoja...

Utamaduni wa kimagharibi leo tarehe 23 November wanaita Black Friday yaani Ijumaa Nyeusi. Hii ni mahsusi kwa wafanyabiashara wanaouza vitu kushusha bei ya bidhaa zao ili kuwapa nafasi watu wenye uwezo wa chini/ mdogo kununua vitu kwa ajili ya wapendwa wao kama zawadi ya Christmas.

Akina sie tuliobahatika kuishia modern nursery school za wakati ule wa mkoloni tunafundishwa na Waingereza wenyewe, hadi lafudhi tuliipata ya Kiingereza sema baada ya darasa la nne ndo ikawa basi tena shule ikaishia hapo ila si haba ulimi bado unatereza utasema nimepitia Cambridge kumbe grade four, aahahahahaaa!

Tulishasikia kuhusu hii Black Friday yote ikiwa na lengo la kusambaza upendo during the Festive Season.

Kasie Matata mie maneno mengii ngoja nipunguze, turejee kwenye lengo la uzi.

Sasa leo nilienda duka moja hivi nao walikuwa na punguzo la bei za bidhaa zao si haba nikapata wasaa wa kujinunulia vitu ntavyovihitaji wakati wa Christmas.

Nikiwa nazunguka kwenye mashelf ya hizo bidhaa nikakumbuka wana JF, siko tajiri, sina uwezo sanaa wala sina pesa ya ziada ambayo haina matumizi ila, ningependa pale ulipo unaposoma uzi huu useme...

Ni kitu gani unatamani ungekipata au ungekuwa nacho kipindi cha Christmas ya mwaka huu 2019, ambacho kiko nje ya uwezo wako kukipata?! Huwezi jua naweza kuwa Granny Christmas to you au memba yeyote humu JF...

Taja kile kitu kweli unahitaji na si kuwa ni mie tuu ndo ntakupatia hicho kitu, kupitia huu uzi anaweza akaja mtu mwingine ana hivyo vitu vya ziada akagawana na wewe au akavinunua mahsusi kwa ajili ya uhitaji wako na wote tukajikuta tunasherehekea Christmas kwa tabasamu.

Sambaza upendo, eneza amani kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya.

Mie nshapamba mti wa Christmas, wewe je?

Wishing all MMU members a Merry Christmas and Happy New Year 2020 mmuuah!!

Mahaba matata kwa Captain.

Kasinde.
I wish you kasie ,nakupenda hadi naugua

USSR
 
I wish you kasie ,nakupenda hadi naugua

USSR


Aahahahhaaa woow, what should I say in return....

Your wish is granted....!!

Just give me the codes USSR....and don't get sick...
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom