Buy it for Life: Tujuzane brand ama model za bidhaa zinazodumu kwa muda mrefu ili tuepukane na usumbufu wa kununua upya

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Uzi huu tujuzane bidhaa zenye viwango vya juu hasa kwa wale wasio na pesa za ziada za kununua upya kitu kile kile ama wanaopenda kukaa na vitu vinavyodumu.

Tujadiliane brand ama model za bidhaa zenye kutumika muda mrefu bila kuchoka ama kufubaa haraka, durable vyenye uwezo mkubwa wa kuhimili mazingira mengi, yaani ukinunua ni mpaka uje ukichoke mwenyewe ama kikiharibika huna cha kudai.

Pasi ya uhakika ambayo haijachuja kwa ubora wake hapa kwetu ni phillips, Binafsi niliwahi kununua pasi yenye manjonjo ya kutoa mvuke na kumwaga maji ila nililazimika kurudi phillips.

1704997265240.png



Furniture zako jipinde chonga za mbao ya Mninga, utazitumia miaka nenda rudi hata wajukuu wanaweza zikuta

1704980822505.png


Laptop inayodumu nunua Chapa ya LENOVO THINKPAD, hili dude utalitumia mpaka uchoke mwenyewe, zimetengenezwa kwajili ya kudumu.

1704980661007.png


Jeans - chapa ya Levis ukiikuta hata mtumbani ibebe haraka, utaivaa sana ukifulia sabuni ya kipande

1704988137737.png
 
Simu: iPhone,
Gari: Any Japanese especially Toyota, Honda, Nissan,
TV/Radio: Sony, LG,
Home Appliances: LG, Sony, Kenwood,
Hio iphone ni gereza la kifahari inapewa wa promo tu, simu battery inakaa kidogo, haina radio, system yake inakuwa obselete ndani ya miaka michahche, earphone zake mpaka uchaji huwezi tumia kawaida, kuhamisha mafaili kwenye computer ni shughuli pevu, apps zake ni chache, bando likiisha huwezi tumia internet bure kwa vpn, n.k.

Leo hii wamezitosa usb cable zao kwa kukubali ukweli zilikuwa hazina nguvu na speed, wanatumia usb c za android ila bado wana jeuri kuwakataza wateja wao wasitumie usb za android wakati zinapiga kazi fresh na ni wao wameiga teknolojia, sio wao waliozibuni hizo cable, ni sawa na mwanafunzi kutaka kumfundisha mwalimu.
 
Wewe ni tajiri!

Mleta mada amesema vile vitu ambavyo kwa hali zetu wabongo hatuwezi kuvinunua mara mbili mbili yaani mtu akinunua amenunua sasa ukibadilisha kitanda kila feshen nani anaiweza hiyo?
Kitanda godoro lazima nibadili haimaanishi kuwa mimi ni tajiri
 
Kitanda godoro lazima nibadili haimaanishi kuwa mimi ni tajiri
Labda kama huwa unanunua vile wanavyopanga pembezoni mwa barabara visivyojulikana vimetengenezwa kwa mbao gani na kununua haya magodoro inch 4&5 but kama unaingia karakana kwenda kutoa order ya kuchongewa kitanda wewe ni tajiri

Last time kuchonga kitanda 6x6 ilikuwa 2021 mbao Mninga nililipishwa 1.2mill mattress nikaenda Tanfoam pale Vingunguti 8 inches nikanunua 485K useme unafanya hivi kila baada ya miaka mitatu ujiite siyo tajiri?mimi navyoona ni tajiri mkubwa hata ninaowajua sijawahi kuona wakifanya hivi.
 
Back
Top Bottom