ropam
Senior Member
- Aug 11, 2010
- 173
- 35
Natanguliza shukrani zangu wana-jukwaa...mimi ni kijana ambaye nimemaliza chuo kikuu mwaka huu. Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimesoma elimu yangu yote mpaka hapa nilipofika kwa jina la upande wa mama (babu yangu upande wa mama), sasa mimi nataka kubadili hili jina nianze kutumia jina langu halisi lakini kuna maswali najiuliza nashindwa kuelewa itakuwaje...maswali kuhusu vyeti vyangu ambavyo kuna vingine ni certifications za kimataifa! Naomba msaada wenu wana-jukwaa, nahitaji kujua kama kuna uwezekano wa kutambulika kwa jina langu halisi (hili jipya ninalolitaka) huku vyeti vilivyo na ubini tofauti vikiendelea kutambulika kama vyeti vyangu halali stil! Akhsante.