puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 1,047
- 2,167
Habari, za muda huu ndugu zangu wana JF.
Kwenye maisha, kuna mambo mengi tunapitia mazuri na mabaya. Naamini sio wote tumewahi pitia mambo magumu kiasi cha kutamani kufa au Dunia ifike mwisho kulingana na sittuation ya wakati huo.
Binafsi nimewahi pitia vipindi viwili vingumu sana kwenye maisha yangu kiasi cha kutamani kujitoa uhai, lakini Mungu ni mwema nilivuka salama.
Sababu ya kwanza ilikuwa ni mapenzi, nilikuwa na mahusiano na dada mmoja nilimpenda sana, mno mno, hii ni kutokana na tabia na upole wake, ni msikivu kiufupi ni mwanamke nilietokea kumpenda na kumwamini. Tumuite Monica (sio jina lake halisi).
Tulipanga mengi ikiwemo swala la kufunga ndoa, wakati mimi nimemaliza chuo nilikaa mtaani kama miaka miwili nikafanikiwa kupata kazi katika kampuni fulani, binafsi kidogo maisha yalibadilika hapo ndio wazo la kumuoa monica likaingia...alikubaliana na mimi ila kwa sharti moja, nisubir amalize chuo (Alikuwa anasomea nursing kibamba) Mimi sikuona shida kwakuwa muda uliobaki haukuwa mwingi, nikamwahid kuvumilia.
Kumbe nyuma ya pazia Monica ameshakuja kutolewa posa na kigogo mmoja serikalini, kwa nilivyo ambiwa na dada yake baadae, ni kwamba Ilikuwa ni vita kubwa Monica hakuwa anampenda jamaa ila tamaa za fedha zikaifunika familia kiasi cha kumlazimisha Monica kukubali kuolewa na jamaa ili kuendelea kula vinono kutoka kwa kigogo.
Nakumbuka dakika za mwisho kabla ya ndoa, nikiwa sifaham chochote Monica alikuwa mtu wa mawazo sana nikimuuliza nini shida anasema yupo sawa. Kuna siku alikuwa analia sana kila nikimuuliza nini shida ndio anazidi kuangua kilio, nakumbuka aliniuliza nini kitakuumiza zaidi katika hivi viwili, Mimi nikifa au siku ikitokea mapenzi yetu kuwa historia, nilistuka sana nikamgombeza kwa nini anamawazo mabaya kiasi hicho, hakuna cha maanza alicho nijibu usiku huo ndio ulikuwa wa mwisho kuonana nae, nikipiga simu haipokelewi sms hazijibiwi, nikitumia namba nyingine akisikia sauti yangu anakata simu.
Nikawa nimebaki njia panda nisijue cha kufanya kwao, kaka zake ni watata sana hivyo siku thubutu kusogea. Ila anarafiki yake anaitwa Sophia, alikuwa ananipenda sana mpaka kufikia hatua ya kunitamkia wazi yuko radhi niwe nae kwenye mahusiano kwa siri bila monica kujua lakini sikuthubutu kufanya hivyo sikutamani kumkosea monica ndio mwanamke niliewahi kumpenda na nikajisikia toka moyoni tangu nimezaliwa kwenye ulimwengu huu.
Siku moja nikampigia simu sophia na kumueleza kuhusu mambo anayonifanyia rafiki yake, sophia aliniambia hata yeye hamuelewi monica, ila akanitoa hofu kuwa monica ni mtu ambae akiwa ana mambo yanamchanganya ni mtu anaependa utulivu binafsi hivyo nimpe muda atakaa sawa.
Nilikubali kishingo upande lakini nilikuwa najiuliza maswali mengi, nimekuwa nae kwenye mahusiano zaidi ya miaka miwili sijawahi ona hizo tabia iweje kipindi hichi....nilibaki na maswali mengi yasiyo na majibu..
Siku moja asubuhi, Sophia alinipigia simu, akaniomba nimkapani kwenye kwenye harusi amealikwa na ana kadi ya double hivyo ananiomba sana maana ndio mtu pekee ananiamini, mwanzoni nilikataa ila baada ya kuniomba sana nikamkubali.
Jioni nikampitia alipo, nilikuwa na kagari kangu kabovu bovu hao mpaka mahala husika, nikiwa sielew hili wala lile, sijui ni namna ma bibi harusi hulembwa na kubadilika...nilianza kuingia hofu baada ya kuona family members wa Monica, nilikuja kupata mshangao mkubwa MC alipokuwa anatoa utambulisho kwa wageni waalikwa.
Sitakaa niisahau hiyo siku, nilihisi naota Monica niliemwamini na kumpenda kwa moyo wangu wote leo, namshuhudia amesimama mbele ya umati mkubwa anaolewa na mwanaume mwingine🥲🥵😢😭
Sophia alijuta kunileta eneo lile, sikujali uanaume wangu nilikuwa mithili ya mtu aliyechanganyikiwa, sijui nilifikaje pale mbele nikama akili iliniambia sio kwenye hebu sogea ukahakikishe...sikujali umati, sikumjali yeyote, nilipomsogelea nikabaini sio naota nipo kwenye maisha halisi, nilipoteza faham sikujua ni kipi kiliendelea nilikuja kuzinduka nipo hospitali, na drip mkononi, pembeni yupo dada yake Monica, sophia na wengine siwafaham, dada yake Monica alikuwa anaujua vyema uhusiano wangu na monica na namna nilivyokuwa najitoa kwa ajili ya mdogo wangu, nilivyomtazama usoni alishindwa kuniangalia machoni akatazama chini kwa aibu ni kama ananionea huruma sana, ila hana cha kufanya imeshatokea.
Ninachokumbuka, baada yakutoka pale hospitalini, niliwaambia nipo sawa naweza kwenda nyumbani sikuhitaji kuambatana na mtu yoyote, ile wiki niliishi kama mfu, nilizima simu nimejifungia ndani, sili, ninywi chochote zaidi ya kulia tu...nilitamani kujiuwa sikuona thamani tena ya haya maisha. Namshukuru sana Mama yangu kuna maneno alinitamkia...nikajisemea nutakuwa hai kwa sababu ya furaha ya mama yangu.
Niseme wazi, tangu Monica aolewe sijawahi amini tena kwenye mapenzi wala kutamani kuoa. Ingawa nasikia mumewe anamnyanyasa mno ameshaniomba msamaha mara kadhaa anatamani kuachika hata tutoweke tukaishi mbali, lakini mimi moyo wangu umeshakufa ganzi, hiki ni kisa cha kwanza, kisa cha pili kitafwata nipumzike kidogo.
ITAENDELEA...........