Ndugu, bongo
Hakuna mtu angependa kuwa na mashaka na JK kwa sasa, lkn kama yeye ni kiongozi anatamka nini kwa haya yanayo endelea? Kama unavyo onyesha upendo na kumshiba JK basi na kama uko jirani naye mwambie arekebishe haya mambo! Watendaji wake wanamharibia sana kama hawa kina Hosea, Chenge, Mustafa etc
festog naona hujaisoma post ya mbangaizaji hapo juu, naona ungali-isoma usingeuliza JK anatamka nini, naomba isome halafu utaona JK anatamka nini na hatua zipi alizochukua mpaka sasa.
festog naona hujaisoma post ya mbangaizaji hapo juu, naona ungali-isoma usingeuliza JK anatamka nini, naomba isome halafu utaona JK anatamka nini na hatua zipi alizochukua mpaka sasa.
Ndugu zangu,
Hili kosa si la Kikwete wala si la serikali yake wala si la Chama chake cha CCM. Hili ni kosa letu na upumbavu wetu wa kukiweka chama hiki cha CCM (TANU/ASP) madarakani kwa miaka yote hii (1961-2008). Tunakubali kiini macho cha kubadilishiwa sura ya mtu kila baada ya miaka 10.
Asilaumiwe mtu wala kitu hapa. Ni sisi wenyewe na ujinga na uwoga wetu. Tunavuna tulichopanda.
Mapinduzi na mageuzi ya nchi yetu yataletwa na sisi wananchi wenyewe. Si CCM si CUF si CHADEMA si TPL si UDP si NCCR-Mageuzi ni Wananchi wenyewe, hizo ni platforms tu tunazoweza kuzitumia kujiletea Mapinduzi na Mageuzi.
Kama tumekasirika kikweli kweli, tu-organize na ku-moblize tufanye kweli 2010.
mbangaizaji ahsante sana kwa kubandika hiyo post, watu wengine humu JF huwa wanabwabwaja tu. kwa wale wanaobwabwaja kama hampati jibu katika hiyo post ya mbangaizaji ndio muanze kuleta hoja, la sivyo fanyeni subra kazi inafanyika, muda wa tume ukiisha na kama hakuna action yeyote kutoka kwa waliokabidhiwa hiyo kazi na JK akikaa kimya tu, hapo ndio tuandamane, tuchukuwe sheria mkononi, tufanye kila tuwezalo kuhakikisha mambo yanakwisha kwa faida yetu walipa kodi, au mnasemaje?
.
WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.
Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.
Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.
Katika harakati za kupambana na rushwa yapo mambo mawili mengine ambayo tutayaangalia kwa karibu. La kwanza ni mikataba. Tutaangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na Serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji. Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa hasa zile kubwa kubwa za wanaotafuta utajiri.
Kadhalika, hatuna budi kuchukua hatua thabiti za kuzuia watumishi wa umma kutumia nafasi zao kujitajirisha na kujilimbikizia mali. Sisemi kwamba ni haramu mtu kuwa tajiri au kuwa na mali. Ninachosema mimi kuwa ni haramu ni kutumia nafasi yako ya utumishi au uongozi wa umma kujipatia manufaa ya kujitajirisha au kujilimbikizia mali.
So tunapenda kuona Details za fedha zilizorudishwa. Ikumbukwe Tume ya BoT ilisema 70% ya hela zilipelekwa nje ya nchi hivyo tunapenda kujua Jina la Mrudishaji, account yake au Banker wake, Kiasi kilichorudishwa na account iliyotumika kupokea marejesho(tarehe, siku na saa ni muhimu)na 70% ya marejesho yatoke nje ya nchi. Kama hizi taarifa hazitawekwa hazarani kama mafisadi na wamiiliki wa makampuni walivyowekwa hadharani, basi JK, na serikali yake yoote iwajibishwe kama alivyofanywa Lowassa.Maana tunaamini fedha zaidi za walalahoi zinaidi kufujwa kufukia za mafisadi.
Hii hotuba JK alisoma kama ilivyoandikwa,kwa hiyo yeye kama jk hakuandika hayo aliyoyasoma.ndio maana hata utekelezaji wake unakuwa wa shida sana, kama angejua kuwa itatuwa hivyo basi nafikiri angeruka baadhi ya maneno.
Kama wanaosema kuwa pesa zinarudishwa ndio wale wale waliosema kuwa hakuna wizi au upotevu wowote umefanyika in the first place basi inabidi uchukue muda kidogo kuamini maneno yao.