Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.
Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.
Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.
Hapa bado tunachezewa tu. Swali ni kwanini hawatajwi? Au ndio hawatajiki? inaonekana hiyo ni trick, au naye Mkullo ni waziri wa fedha jina, kuna mwenyewe anayeoperate under the carpet.
Kama wanaosema kuwa pesa zinarudishwa ndio wale wale waliosema kuwa hakuna wizi au upotevu wowote umefanyika in the first place basi inabidi uchukue muda kidogo kuamini maneno yao.
Ebu tujikumbushe kidogo hotuba aliyoitoa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Bungeni tarehe 30 Desemba, 2005 kuhusu Rushwa (ufisadi):
"Tutaongeza kasi ya kupambana na rushwa kisayansi kwa kushambulia kiini chake, na kuziba mianya yake. Tutajitahidi kuongeza mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ili kupunguza vishawishi vya rushwa. Tutaendelea pia kuongeza uwazi katika maamuzi ya Serikali hasa katika manunuzi na mikataba. Tutaimarisha uwezo wa kifedha na kiutendaji wa taasisi zilizo mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya rushwa, hususan Taasisi ya Kuzuia Rushwa, Jeshi la Polisi na Mahakama. Lakini yote hayo ni bure iwapo wananchi hawatajitokeza kusaidia vyombo hivyo. Naomba ushirikiano huo kutoka kwa wananchi.
Katika harakati za kupambana na rushwa yapo mambo mawili mengine ambayo tutayaangalia kwa karibu. La kwanza ni mikataba. Tutaangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na Serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji. Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa hasa zile kubwa kubwa za wanaotafuta utajiri.
Kadhalika, hatuna budi kuchukua hatua thabiti za kuzuia watumishi wa umma kutumia nafasi zao kujitajirisha na kujilimbikizia mali. Sisemi kwamba ni haramu mtu kuwa tajiri au kuwa na mali. Ninachosema mimi kuwa ni haramu ni kutumia nafasi yako ya utumishi au uongozi wa umma kujipatia manufaa ya kujitajirisha au kujilimbikizia mali.
Jambo hili ndilo linalokera sana watu kuona mtu ambaye hana chochote lakini miezi michache tu baada ya kupata cheo anakuwa tajiri mkubwa. Ona majumba ya fahari, ona madaladala, teksi bubu, anaishi maisha ya kifahari na kadhalika. Wananchi wanayo haki kuhoji, na wanayo haki kupata majibu. Ndugu zangu, naomba tuwe waadilifu. Tusilaumiane. Nataka Tume ya Maadili ya Viongozi isione haya kutuuliza jinsi tulivyozipata mali tunazosema tunazo. Nitawasaidia kujenga uwezo wa kufanya hivyo kama tatizo lenu ni hilo".
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete...ulisema mwenyewe....sasa tunataka majibu sahihi ni akina nani hao wanaorejesha hizo pesa na kwanini hadi sasa hawapo Keko au Segerea...ulituambia mwenyewe kwamba tunayo haki ya kuhoji...sasa twambie tuwajue wezi wetu ni akina nani?
Hebu tukumbushe ndio kina nani hao, majina ya waliosema hayo? you mean Mkullo? na lini alisema? any proof? au ndio nanihii tena?
Hii hotuba JK alisoma kama ilivyoandikwa,kwa hiyo yeye kama jk hakuandika hayo aliyoyasoma.ndio maana hata utekelezaji wake unakuwa wa shida sana, kama angejua kuwa itatuwa hivyo basi nafikiri angeruka baadhi ya maneno.
kikwete inchi kama imekushinda si uachie ngazi?????
Imemshinda wakati unaona anavyijituma mpaka fedha zilizolambwa zinarudi, unanishangaza sana.
Naomba kuuliza wakongwe wa JF, hivi hizi fedha za EPA zilichukuliwa awamu ipi na zilikuwa zirudi lini? naomba mnisaidie kwa hilo.
soma post iliyoanzisha thread hii halafu muulize huyo, hizo billioni 50 zimerudi wapi? ukiniuliza mimi unanionea kwani nimechangia mada tu na nimeona hapo mwanzoni kuwa billioni 50 zimerudi. Au umekurupuka tu, hukusoma mwanzo wa thread? kwa kukusaidia tu nabandika hapa kipande cha hiyo post:zimerudi wapi?
soma post iliyoanzisha thread hii halafu muulize huyo, hizo billioni 50 zimerudi wapi? ukiniuliza mimi unanionea kwani nimechangia mada tu na nimeona hapo mwanzoni kuwa billioni 50 zimerudi. Au umekurupuka tu, hukusoma mwanzo wa thread? kwa kukusaidia tu nabandika hapa kipande cha hiyo post:
...bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania...
Ndugu zangu,
Hili kosa si la Kikwete wala si la serikali yake wala si la Chama chake cha CCM. Hili ni kosa letu na upumbavu wetu wa kukiweka chama hiki cha CCM (TANU/ASP) madarakani kwa miaka yote hii (1961-2008). Tunakubali kiini macho cha kubadilishiwa sura ya mtu kila baada ya miaka 10.
Asilaumiwe mtu wala kitu hapa. Ni sisi wenyewe na ujinga na uwoga wetu. Tunavuna tulichopanda.
Mapinduzi na mageuzi ya nchi yetu yataletwa na sisi wananchi wenyewe. Si CCM si CUF si CHADEMA si TPL si UDP si NCCR-Mageuzi ni Wananchi wenyewe, hizo ni platforms tu tunazoweza kuzitumia kujiletea Mapinduzi na Mageuzi.
Kama tumekasirika kikweli kweli, tu-organize na ku-moblize tufanye kweli 2010.
Ndugu zangu,
Hili kosa si la Kikwete wala si la serikali yake wala si la Chama chake cha CCM. Hili ni kosa letu na upumbavu wetu wa kukiweka chama hiki cha CCM (TANU/ASP) madarakani kwa miaka yote hii (1961-2008). Tunakubali kiini macho cha kubadilishiwa sura ya mtu kila baada ya miaka 10.
Asilaumiwe mtu wala kitu hapa. Ni sisi wenyewe na ujinga na uwoga wetu. Tunavuna tulichopanda.
Mapinduzi na mageuzi ya nchi yetu yataletwa na sisi wananchi wenyewe. Si CCM si CUF si CHADEMA si TPL si UDP si NCCR-Mageuzi ni Wananchi wenyewe, hizo ni platforms tu tunazoweza kuzitumia kujiletea Mapinduzi na Mageuzi.Kama tumekasirika kikweli kweli, tu-organize na ku-moblize tufanye kweli 2010.
Imemshinda wakati unaona anavyijituma mpaka fedha zilizolambwa zinarudi, unanishangaza sana.
Ili iweje?