Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Fundi Mchundo,
Imebidi nirudi tena kukufahamisha kile nilichokuwa nikisema toka mwanzo... Kuwa sanctions zote ni siasa za Biashara!.. toka mwanzo nimelisema hili sijui unatazama wapi mkuu... hukutaka kunielewa bali kila wakati huongeza maswali tu kwa kila nilichoandika badala ya kutazama the big picture.
Ni hivi pamoja na kwamba vikwazo vinajieleza wazi katika nchi tofauti ukweli wa hali halisi sivyo kama ilivyoandikwa...Hizi ni siasa za nchi za magharibi siku zote..
Nikatoa mfano wa Cuba, Iran na kadhalika.. hata Mugabe kuwepo New York na majuzi Italia bado hukujibu kitu ila kutafuta njia ya kutokea.. Sheria zinasema tofauti na vile vinavyoendelea humo. Vitu vinaingia pamoja na vikwazo vyote as a fact Canada wapo wafanya biashara wamewekesha Cuba na dunia haitambui kisheria ushirikiano kama huo ambao upo..best destination ya Wa -Canada ktk tourism ni Cuba.. na kwa mwaka mmoja tu Cuba inapata zaidi ya watalii 500,000 toka North America peke yake... hawa wote wanaingia Marekani na kutoka bila kufuata hizo sheria za sanction unazozizungumzia. Cigar za Cuba hadi kesho zinaingia Marekani kinyume cha sheria hizo unazozungumzia...Hii ndio hali halisi mkuu, sio kilichoandikwa.

Kitu kingine labda nikwambie tena kuwa kama wewe ni Muislaam na jina lako lina majina yote matatu ya Kiarabu basi mkuu huwezi kutuma fedha hata iwe Africa kirahisi fedha hizo zinarudishwa! Je, ipo sheria ya namna hiyo!.. Mimi nafikiria tunachozungumza hapa ni kile kinachotendeka na sio sheria! Mugabe anayoyafanya sidhani kama yamo ktk katiba ya Zimbabwe ama yanatambuliwa kisheria!..tunachozungumzia ni ubabe wa Mugabe na huo wa wazungu hasa Waingereza..na binafsi nafikiria hofu yao kubwa ni MCHINA ambaye anaingia Afrika kwa kasi ya ajabu.
Mugabe kasimamiwa na wahuni ambao hawajali sheria inasema nini! wao upinzani hukumu yake ni kifo tu yaani unauza nchi.. Huu ni uharamia kama alioufanya Saadam Hussein wakati wale Ma Qurdish walipotumiwa na Marekani...Na siku Saadam alipokianzisha kwa hao Qurdish - Wamarekani waliingia mitini, waliwaacha Qurdish ktk mataa wakauawa kama ndama. hiki ndicho nachozungumzia kuwa wazungu wanafiki, washenzi na siku zote watu kama Morgan ambao wanataka kubebwa na mzungu ni hatari sana...

Leo hii Iraq nchi nzima wanalipa kosa la uongozi wa Saadam as a fact sababu kubwa ni Marekani na uongoi wa Bush hata kama tunaweza kusema Saadam was brutal and he had to go!.Hii ndio hofu yangu kubwa na nawaomba tujihadhali nayo zaidi ktk kila tunapojaribu kulitazama swala la Zimbabwe!
Sheria zilizoandikwa kuhusiana na Zimbabwe ni kama ulivyozieleza na kama unakumbuka niliwahi kuyasema haya toka mwaka 2004 ktk ubishi kama huu...Na nyie kwa kutofikiria mnakubali kabisa kwamba Wa - Zimbabwe hawajui kulima isipokuwa mzungu..Na inazidi kunishangaza unapotumia vigezo zvizito kama Utaalam wa ujenzi wa nyumba ktk kilimo ambacho ni jadi ya Mbantu. yaani wazungu ndio wametufundisha kweli kulima ati wao ni architectures wa ukulima!..kiasi kwamba Wazimbabwe washindwe kujua la kufanya hata chakula chao wenyewe washindwe kulima!..
Pengine msichoweza kufahamu ni impact ya kufungiwa kiuchumi, wazungu ni zuga wakubwa sana inapofikia maslahi ya nchi zao ama haki ya mwafrika..

Well, nitarudia kusema kwamba siwezi kuendelea kubishana..kwani nakumbuka wakati wa kuivamia Iraq nilisema wazi ktk kijiwe hiki (Bcstimes) kuwa Marekani wamevamia nchi hiyo kwa sababu ya Mafuta (OIL)mkanibishia sana na kusema yote mabaya ya Saadam including WMD kama ndio sababu kubwa..lakini mkashindwa kuelewa kwamba sikubisha kabisa mabaya ya Saadam isipokuwa kuwashutumu Westerners ktk hatma ya Iraq ni ukweli usiofichika!..
Leo tena najikuta ktk mjadala kama ule ule ambao baada ya miaka mtakuja kaa kimyaaaa msikubali makosa yenu ya kutoona mbali.

Nimesema tunaongea lugha tofauti. Nimekujibu hoja zako lakini pengine kwa vile majibu yangu hayakuendana na uliyoyataka unakazania kuwa sikukujibu! Mfano wako wa Cuba nimeujibu na kukuelezea kuwa hata wakati wa mapambano dhidi ya utawala wa makaburu Afrika Kusini, wanafunzi na makanisa huko Marekani(na wengine) walisusia bidhaa za Afrika Kusini wakati nchi yao ilikuwa haijaweka vikwazo! Nikakueleza kuwa hata sisi tulipofunga mpaka na Kenya, bidhaa kutoka Kenya ziliendelea kupatikana. Hivyo hivyo hakuna kitu kinachomzuia mCuba kwenda Brazil au China, kuingia dukani, kununua jozi mia za Nike na kwenda kuziuza dukani kwake Havana. Hii haimaanishi kuwa Nike wana uhusiano wa kibiashara na Cuba. Kwa kifupi, matendo ya watu binafsi, mashirika binafsi n.k. si msimamo wa serikali.

Huop mfano wako wa Canada nao batili. Nitakusaidia. Kuna wanafunzi wengi wa kimarekani wanasomea udaktari Cuba, lakini hii haina maana kuwa sanctions hazipo! Watu kulazimika kwupitia Canada au Mexico ili waende Cuba ni ishara kuwa hizo sanctions zipo. Kupatikana kwa Cuban cigars, mwenyewe unakiri illegally, si dalili kuwa sanctions hazipo. Kupatikana kwa crack katika mitaa ya New York hakuhalalishi matumizi yake. Wakati tumefunga mpaka na Kenya, watu walikuwa wakienda kenya kwa kupitia Addis. Hii haikuwa na maana kuwa mipaka imefunguliwa? Na kama nilivyokueleza, sabuni za Imperial zilikuwa zinapatikana kama kazi kwenye mitaa ya Darisalama.

Haya,Mkuu, haya ya uislaamu nayo yametokea wapi. Kuna watu wataapa kuwa kama wewe si mchaga hupati kazi TRA lakini hii haimaanishi kuwa ni msimamo wa TRA kuajiri wachaga tu! Unfortunately, racial, ethnic profiling zipo kila mahali. Hata kwetu.Ukiingia kwenye supamaketi Dar umevaa ndala, utakuta unamsindikizaji lakini akiingia mzungu amevaa hivyo hivyo anachangamkiwa. Kinachoendelea kwa wenye majina ya kiislamu ni hivyo hivyo. Uamuzi wa benki binafsi au Western Union kukataa au kukusumbua kwa vile tu wewe ni mwislamu au una jina linalodhaniwa ni la kiislamu, ni wao na si wa serikali. Kuna avenues za kufuata kama unaona haukutendewa haki.

Mugabe si mhudumu wa benki, ni rais wa nchi. Yeye ameonyesha kuwa ana utter contempt na whatever passes as a constitution. Amesimama kwenye kadamnasi na kuwa'mock' kwa kusema anayeweza kumtoa pale ni Mungu tu. Huyu ni mhuni. Na ndicho tunachokisema lakini hutaki kuelewa. sasa kwa vile George Bush senior aliwatosa waKurd, leo anayoyasema mwanae kuhusu huyu mhuni yanakuwa hayana ukweli? Kuna tofauti gani na sisi ambao tulisimama tukiangalia wakati jirani zetu Rwanda wakiuana kikatili? Ambao tunaendelea kuikumbatia serikali ya Sudan wakati ikiendelea na mauaji na unyama huko Darfur? Wakati Bush ameishayaita yanayoendelea huko kuwa ni genocide, nani katika sisi REAL Africans ametoa tamko kulani yanayoendelea? Badala yake tulitaka kuwatuza kwa kuwapa uenyekiti wa AU! Toa kibanzi katika jicho lako kwanza. Sisi hatumkemei Mugabe kwa vile wamarekani na wazungu wanafanya hivyo. La, hasha, tunamkemea kwa sababu aliyowafanyia wazimbabwe ( kuanzia wa matebele, na ndio hata wale Wazimbabwe weupe n.k) goes beyond the pale. Huyu bwana ni muovu, period. Kama wananchi wa Zimbabwe wakiamua kumchagua Morgan wewe una tatizo gani? Akiendeleza hayo ya Mugabe, nae atakemewa na hopefully atatemwa na watu wake. Kama ilivyotokea kwa Chiluba.

Nani amesema waZimbabwe weusi (inaelekea mwenzangu waZimbabwe weupe wewe huwahesabu kama ni raia wa nchi ile) hawajui kulima? On the contrary, mara baada ya zoezi la kwanza la kuwagawia wakulima mashamba ya waZimbabwe weupe, uzalishaji ulipanda. Tatizo ni hapo alipoamua kuwapa kmakada na cronies wake ambao hawajui lolote kuhusu kilimo. Wale wanachi waliokuwa wakifanya kazi katika mashamba ya wazimbabwe weupe walionekana kuwa ni potential wasaliti, wakatemwa. Uendeshaji wa mashamba makubwa unahitaji expertise ambayo si wote waliyokuwa nao. Nilikueleza kuwa, Fundi mchundo au Fundi muashi si sawa sawa na Mhandisi ingawa inawezekana kabisa kuwa wanamzidi katika upangaji wa matofali! Sisi wenyewe tulinyang'anya plantations na ranchi kutoka kwa wale tuliowaita makabaila na tumeshindwa kuyaendesha. Mbona wamasai wako kibao , kwa nini basi tumeshindwa kuendesha ranchi za Kongwa n.k.? Si tungewapa wakina Ole ? Naam, kilimo ni jadi ya mbantu. Ndio maana kila kukicha tuna kibakuli tukiganga njaa! Kilimo cha kiamba si sawa na kilimo cha plantation. Ndiyo maana Nyerere alipoenda Marekani kama mgeni wa Carter, alitembelea Georgia, kuangalia wenzetu wanalimaje. Ukisikia kuwa Carter alikuwa analima karanga si sawa na mkulima wetu wa zao hilo hilo kule Dodoma. Kila utaalamu una kikomo chake. Mkandarasi wa Class 5 haruhusiwi kujenga jengo lenye ghorofa kumi. Matokeo yake tumeyaona. Wengi wetu tunaweza kujenga kibanda lakini inapokuja kaghorofa tunawaachia wataalamu. Ndivyo inavyotakiwa.

Tusiopendana ni sisi. Muuaji mkubwa wa mtu mweusi ni mtu mweusi mwenzake. Wazungu wana mchango wao lakini kwanza inabidi tubanane wenyewe kwa wenyewe ama sivyo hatutajikomboa. Hakuna mtu anayemheshimu mtu asiyejiheshimu. Tutamtegemeaje mzungu atujali wakati wenyewe hatujijali?

Sasa unaondoka Somalia unakimbilia Iraq! Wakati huo huo ukinishutumu kwa kusogeza magoli!!!!! Mimi sikuweko Bcstimes ( nimegundua kitu kinachoitwa internet mwaka jana tu) kwa hiyo nisingeweza kukubishia. Lakini kama ningekuweko, ningekubishia. Sio kwa sababu ulizoziweka bali kwa vile hoja yako ilikuwa simplistic na kwa msamiati wako, ya kutoka kwa kinyozi.

Mkandara, arguments zako ni convoluted bila sababu. Kama nilivyosema awali, naona tunaongea lugha tofauti.

Amandla.......
 
Jana Mandela, ametoa maneno mazito sana kumsema Mugabe kwa mara ya kwanza, lakini ninashangaa kuwa kwa nini ameenda kuyasemea majuu badala ya Afrika, tena akiwa amezungukwa na wazungu why? Wakuu naomba kueleweshwa?

Mkuu Thabo Mbeki, nasikia Muagbe anamuita ni play boy, na kwamba anamdharau sana kuwa ni kibaraka wa wazungu na ameshamwabia hivyo mara nyingi usoni kwake, na pia nasikia na sisi bongo anatuona ni a big joke hasa baada ya Joji Kichaka kuja kwetu, nasikia anatudharau sana,

Hapa ndio tunamkumbuka Mwalimu, yule mzee alikuwa na something sijui ni kile kifimbo au tunguli, maana angekwenda kwa huyu Mugabe na angemshikisha adabu, muulize Buyoya wa Burundi!

Huyu mzee anajua dili lote!
ANAWAFAHAMU WACHINA VIZURI SANA KAMA WENGINE WANAVYOWAFAHAMU!

HUYU MZEE ANGEKUWA HAONI MBELE...ASINGEKUBALI KUKAA JELA KWA MIAKA 27!

FROM THE BOTTOM(JAIL) TO THE TOP(STATE HOUSE)

MADIBA...WALIMPA MASHARTI NA KUMWAMBIA KUWA ILI WAMTOE JELA..NI LAZIMA AKUBALI KUTOSHIRIKI KWENYE MAMBO YA SIASA.

AKASEMA NABAKI JELA!
RESOLVE YA KIZALENDO!

UKISHAKUWA FISADI...UKIPIGWA JAMBA JAMBA KIDOGO TU UNAUZA NCHI.

MCHINA HAKUKUBALIWA NA KIKWETE KWANI BALLALI HAKUWA HUKO!

MAMBO HAYA NI TOOO MIXED!

NA NDIO MAANA KUNA TETESI ZA JESHI KUGAWANYIKA KUHUSU EITHER KUMSAPOTI MCHINA AMA MMAREKANI.

MADIBA ANAJUA KUWA HAWA MAREKANI WAKO KWENYE HALI NGUMU SASA HIVI!

KIUCHUMI NA KILA KITU!

KWASABABU YA VITA YA IRAQ NA KICHAKA!

ANAJUA KICHAKA NI KICHAA NA ANAWEZA KU COMMIT TROOPS!
AT THE SAME TIME ANAJUA INTELLIGENCE YA HUO MTENENGE WA MCHINA AMBAO UNAMPA MUGABE KIBRI!

HUYU MZEE ANJAUA MAISHA YAKE SASA NDIYO HIVYO TENA...UMRI!

HIVI MAREKANI NA UK WAKITOLEWA NISHAI NANI WA KWANZA ATAKAYEFUNGUA CHAMPAGNE KAMA SI DIBAS?
 
Kitu kingine labda nikwambie tena kuwa kama wewe ni Muislaam na jina lako lina majina yote matatu ya Kiarabu basi mkuu huwezi kutuma fedha hata iwe Africa kirahisi fedha hizo zinarudishwa!

Si kweli...

Kuna vitu tukisema jamani tujue tunaongea mbele ya halaiki ya watu wenye experiences za kila aina.
 
ndugu Yangu Mushi, Hivi Uchaguzi Wa Zimbabwe Ulipangwa Na Uk Na Us? Kama Uchaguzi Ulikuwa Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Zimbabwe Na Wapiga Kura Walikuwa Ni Wazimbabwe Wenyewe Ni Kwa Nini Walaumiwe Uk Na Us? Kama Kweli Mugabe Alikuwa Na Nia Ya Dhati Kuwa Na Uchaguzi Huru Na Wa Haki, Ni Kwa Nini Aue Watu Waliopiga Kura Kumkataa?

Watu Wa Zimbabwe Wanaijua Hali Ya Zimbabwe Kuliko Wapiga Debe Wa Mugabe Wasio Wazimbabwe Na Ndio Maana Walipiga Kura Ya Kumkataa Mugabe Na Kumkataa Na Kumtaka Morgan Awe Rais Wao. Wazimbabwe Sio Wajinga Kumpigia Kura Morgan Eti Kwa Sababu Tu Amewekwa Na Uk Na Us. Kama Morgan Angekuwa Na Madaraka Serikalini Tungefikiri Kuwa Labda Aliwahonga Wazimbabwe Na Ndio Maana Alipigiwa Kura Ya Kukubaliwa, Lakini Hivyo Sivyo. Mimi Ninaamini Kuwa Wazimbabwe Walimpigia Kura Morgani Kwa Sababu Waliona Kuwa Ni Kiongozi Bora Kuliko Mugabe Na Si Kwa Sababu Ya Madai Kuwa Ni Kibaraka Wa Uk Na Us.

Saddam Walimwekea Vikwazo Sana Tuu!
Wananchi Wakateseka Sana!

Lakini Kwa Undava Wa Kichaka...wakawa Bado Wanamrudisha Madarakani Saddam Kwani Alikuwa Na Beef Na Hao Vichaka Kuanzia Kichaka Senior!

Wairaki Wakawa Wanaandamana Kila Siku!
Dunia Nzima Ikaandamana!

Kumbe Kuna Watu Wana Yao Na Walishapanga Vita Loong Time Kwenye G8 Summit Na Kukubaliana Kuhusu Dili La Zimbawe,iraqi!

Dili Likishapangwa Na Masaini Kuangushwa Ni Vigumu Kulivuruga!
Dunia Nzima Iliandamana Kupinga Vita Ya Iraqi!
Blair Akapoteza Umaarufu Wake Na Hata Kuhusishwa Na Ushoga Yeye Na Bush!

Sasa Ni Zamu Ya Bush Kulipa Fadhila!
Atamsikiliza Nani?
Mandela Ambaye Alikataa Kumsikiliza Alipomwambia Asivamie Iraqi?

Walipovamia Iraqi..waligawana Hivi...jimbo La Kusini La Shiite Lenye Mafuta Mengi Walipewa Uk.

Huko North Kwa Kurdish..ndio Kama Taifa Jingine Kabisa Kwani Wanajitegemea Kama Serikali Tofauti Kabisa!

Hawakukaa Sana Majimbo Ya Sunni ALMAARUFU "THE SUNNI TRIANGLE"
Kwani Hayana Mafuta!

Hilo Likawa Kosa Kwani Alkaeda Kwa Kumtumia Al Zarqawi Walikuwa Wanaiongoza Irqi Kigaidi kwenye ukanda huo wa SUNNI TRIANGLE ambao unaweza kuona ilkuwa ni mpango wa SADDAM..Kwani kwenye hiyo triangle yao wanauwezo wa kuwatandika wamarekani na shiite pande zote za IRAQI kwani hiyo triangle imeunganisha sehemu kidogo ya Northern side, maeneo ya kati kusini pamoja na east and west!

MARK MA WORDS...SUNNI WATALIRUDISHA TAIFA LA IRAQI!
Remember The Battle For Falluja Etc Etc!

Sasa Baada Ya Kugundua Kuwa Sunni Ni Noma..wakawaingiza Kwenye Dili Kwani Hatua Yao Ya Debaathification Haikuwa Nzuri Kwani Waliwafukuza Polisi Wote Na Kila Mtu Na Wakaweka Kila Polisi Wapya
.
Ambao Maandalizi Yao Ya Zima Moto Huko Jordan Yaliwafanya Kitoweo Kwa Maofisa Wa Saddam Waliofukuzwa Kazi!

Hivi Unawajua Hao Walionyang'anywa Mashamba HUKO ZIMBABWE?!
Hawa Walienda Kulia Lia Kwa Malkia!

Na Familia Hiyo Wana Uhusiano Wa Damu Na Bush!

CONNECTION YA ROYAL FAMILY NA BUSH IKO KWENYE KING HENRY THE SOMETHING!
Kaazi Kweli Kweli!
 
Wakina MADIBA WANAJUA ZIMBABWE WAKISHINDA BASI NI AFRIKA IMESHINDA!

WATU WANATEGWA!

MANDELA SI KICHAA AKATAE MAREKANI NA UK KUIVAMIA IRAQI HALAFU AKUBALI WAIVAMIE ZIMBABWE!

MWACHENI MZEE WA WATU!

SI MJINGA HUYU MTU!

WE SUBIRI KICHAKA ATIE TIMU HUKO...ATAKUTANA LIVE NA HU JINTAO!
 
Kichaka Atajiuliza!
Ala!
Inakuwa Vipi Huyu Mtu Aliniita Kichaa Nipokwenda Iraqi Na Sasa Haoni Noma USA Kwenda Zimbabwe?

Yani Kweli Mandela Aliwaonea Huruma Wairaqi NA SADDAM Kuliko Mugabe Na Zimbabwe?
 
Fundi Mchundo...hayo Hapo Juu Maoni Yangu Kwa Sasa..sasa Leta Mambo Na Ukae Kwenye Hoja!
Ni Maoni Tuu!
 
Nchi Ya Iraqi Ni Zaidi Ya Asiliamia 70 Shiite,NA kurdish na other ethnic groups ni the remaider(10%)

Sunni Ni Kama 20% Lakini Position Yao Ya Makazi Yao Ni Mpango Kamili!
Maana Saddam Alikuwa Akipewa Sapoti Na Mmarekani Yeye Kama Sunni!
Silaha,pesa Kumlinda Nk.

Ila SADDAM na yeye hakuwa mjinga..kwani aliwaposition SUNNI kitaalam sana.

Na ndio maana MADIBA AKAMUONYA KICHAKA!

HAKUSIKILIZA! NA KWASABABU ANAJUA USA WANAWEZA KUWA WANAPALILIA ANGUKO LAO..KAJIFANYA KICHAA KWENYE ISSUE YA ZIMBABWE!


Wamarekani Walichukua Uamuzi Huo Mara Baada Ya Mapinduzi Ya Kiislam Ya Iran!

Mapinduzi ambayo yalitokana na uamuzi wa marekani kuwawekea wairani mtawala wa kifalme.."SHAH"
Irani Ni Shiite!

Na Iraqi Ni Nchi Yao Takatifu Kama Ilivyo Kwa Saudi Arabia Na Sunni.

Given The Fact That Iraqi Ni More Than 70% Irani(shiite=irani) Marekani Wailiogopa Kuwa Mapinduzi Hayo Ya Ayatollah..yataamia Iraqi Kwani Ni Nchi Yao Takatifu!

Madhambi Waliyomuua Nayo Saddam Si Madhambi Ya Saddam Ni Ya Marekani!
Wao Ndio Walimpa Silaha Za Kina Aina!

Irani Naye Akawa anapigwa Sapoti Na Russia Etc Etc!
Saddam Ilibidi Apewe Msaada Na Usa Ili Kuweza Kuwadhibiti Shiite Kote Kote...iran Na Ndani Ya Iraqi!

Mmarekani alikuwa akipambana pia na MRUSI KABLA HAJAANGUSHWA NA REAGAN.

ZIMBABWE NI MCHINA!

Mpambano Uliendelea Kwa Miaka Nane Na Matokea Yake Mnayajua!
Bush Si Binadamu Kabisa...!

This Is Why...watu Aliowasapoti..kina Chalabi Na Wenzake Waliopewa Nchi...walikuwa Irani!

Irani..nchi Ambayo Bush Anataka Kuivamia!

Sasa Utawapa Vipi Nguvu Irani...huko Iraqi Na Kuwasapoti Wairani Hao Na Huku Akitaka Kuanzisha Vita Nyingine dhidi yao!?

BE WARE WITH WAR MONGERS!

Kwanini anataka kuivamia IRANI WAO NA ISRAEL?

NA WAKATI WAO NDIO WAMEWAPA NGUVU IRANI KWA KUWATOLEA SADDAM?

Vita Ni Biashara Kubwa Sana Kwa Bush Na Marafiki Zake Kwani Wanauza Silaha Kama Njugu!

Sasa Hivi Muirani Anasikilizwa Zaidi Na Serikali Ya Iraqi Iliyowekwa Na Bush More Than Jinsi Wanavyomsikiliza Bush!

Hawa Wanataka Dunia Iwake Moto Ili Wauze Silaha Na Kupora Mali!
Bush Anataka Sapoti Ya Israel Kuwachapa Iran...irani Sasa Ni Kubwa Sana...!

Kwani Iraqi Sasa Ni Technically Irani Kwa Msaada Wa Bush Mara Baada Ya Kuwaondolea Adui Yao Mkubwa Saddam!

Kuivamia Iraqi Ni Mbinu Ya Bush Kuanzisha Moto Huko Middle East Kwani Hapataka Kalika!
Wao Wamekuwa Sasa Ndio Saddam Wa Iran!

Wasingeweza Kufanya Hivyo Kama Saddam Angekuwa Hai!
Wamejisogeza Karibu!

Subiri Uone!

Majeshi Ya Marekani Yameizunguka Dunia Na Bahari Zote!
Hakuna Mahali Ambapo Hawana Jeshi Na Miltary Bases.
Bush Alishasema You Are Either With Him Or Not!

Kumbuka Axis Of Evil...iraq,iran Na North Korea!

Yangu Macho!
 
Wachina nao si wajinga!
Sasa nani asiyejua kuwa NORTH KOREA NA CHINA NI KITU MOJA?

NA SASA BUSH ANAFANYA JUU CHINI KUWAONDOA NORTH KOREA KWENYE AXIS OF EVIL KWASABABU THE CHINA CONNECTION IS VERY CLEAR!

NI VITA YA SUPERPOWERS!

MCHINA ANATAWALA DUNIA NA MAREKANI PIA KWA KIASI KIKUBWA WAKIKATA MAWASILIANO NA MCHINA..BASI MWENYE HASARA NI MMAREKANI NA MARK MA WORDS..THEY WILL GO DOWN!

MABENKI YAO WANAMILIKI WAO!
BIDHAA ZOTE ZA MAREKANI HUTENGENEZWA CHINA!
HAKUNA KITU MADE IN USA HAPA...NI CHINA!
MAREKANI ANADAIWA NA MCHINA KULIKO ANAVYODAIWA NA TAIFA LOLOTE HAPA DUNIANI!

KICHAKA AKIKOMAA KWENDA HUKO ZIMBAWE..ASISHANGAE AKIKUTA NA HU JINTAO AMBAYE ATAMKWIDA SHATI ARUDISHE PESA WANAZOKOPA!

PESA AMBAZO HAWAWEZI KULIPA KWA SASA KWANI NI NYINGI MNO!

MCHINA SI MJINGA!
NDIYE SUPERPOWER!

PESA YOTE YA VITA VYA IRAQI...USA WANAKOPA KUTOKA CHINA!
WAENDE HUKO ZIMBAWE WAONE KAMA MCHINA ATAENDELEA KUWAKOPA!

NA SASA MUGABE MJANJA...!

BAADA YA YEYE KUSOMA DILI LOTE..KAMPIGA BAO BUSH KWA KWENDA KWA JINTAO!

KAMA KWELI MCHINA YUKO NYUMA YA MUGABE..BASI MAREKANI IKIENDA HUKO..ULE USEMI WA MADIBA WA KUWA KICHAKA NI KICHAA UTATIMIA!
 
Mkuu,JMushi1.
Kwanza unaniambia nichangie mada lakini nisitoke nje ya hoja. Nilipokuuliza hoja yenyewe ni ipi (ili nisije toka nje yake kama ulivyonishauri) unaniambia haujui!

Are you for real au unataka ku'yank my chain'?
 
Mkuu,JMushi1.
Kwanza unaniambia nichangie mada lakini nisitoke nje ya hoja. Nilipokuuliza hoja yenyewe ni ipi (ili nisije toka nje yake kama ulivyonishauri) unaniambia haujui!

Are you for real au unataka ku'yank my chain'?

Marekani hawezi mwambia mchina kitu!
Kama Mchina ni kweli Yuko nyuma ya MUGABE!
BASI WASHAPIGWA BAO NA MADIBA WALA HANA HAJA KUWAKATAZA TENA.
Pia nimekuonyesha uhusiano kati ya TSIVANGIRAI NA SADDAM!
KWAMBA KAMA UKIMSIKILIZA BUSH NA WEWE NI MWENDAWAZIMU!
BISHA?
DIVIDE AND RULE ETC ETC!
MIFANO YOTE NILIYOKUPA INAONYESHA KWAMBA SI KWELI BLAIR NA BUSH WANA NIA NZURI NA AFRIKA NA DUNIA KWA UJUMLA?
MADIBA KESHA MWITA KICHAA!
NA UKIMSAPOTI KICHAA..NA WEWE NI KICHAA!
SITAKI KUAMINI MANDELA NIKICHAA!

HAPA ISSUE NI KUWA HATUTAKI VITA!
 
Madiba Anajua Wanataka Kuzitumia Damu Za Waafrika Kwa Malengo Yao Wenyewe!
Aligundua Dili Lote Na Ndio Maana Wakam Isolate Kikwete Na Huku Wakitoa Kauli Ili Wazungu Hao Wasije Wakahisi Ni Influence Yake Madiba Kumsideline Kikwete!
Kwani Anajua Hii Ni Proxy War Na Usa Hawatathubutu Kupigana Na Mchina Hata Siku Moja!
KWANI HII THREAD SI INAHUSU WESTERN PROPAGANDA?
SASA UK NA USA NI EAST?
 
Kama hujui michezo ya west basi hapa unaleta ushabiki tu!
FYI....Wakimpa Tsivangirai silaha...Halafu wakagundua kuwa hawezi kumwondoa Mugabe...Then watamsikiliza Mugabe.
Mugabe na yeye anaweza kunegotiate na USA KIDOGO HALAFU TSIVANGIRAI AKANYONGWA KAMA SADDAM KWA MAUWAJI WATAKAYOYAFANYA KWA KUTUMIA SILAHA HIZO HIZO WALIZOMPA!
KUWENI MACHO NA MJIFUNZE HISTORIA NA KUFANYA TAFITI NA SI KUKUBALI KILA KITU CHA BUSH NA BLAIR.
HAKIWEZI KUWA NA NIA NZURI KABISA!
TENA HAO NDIO WAMEHARIBU KABISA!
TSIVANGIRAI ANGEPATA SAPOTI KAMA SI KINA KICHAKA!
 
MtuMungu,
Haya yanayotokea Zimbabwe unashangaa kitu gani hali yameshatoikea Tanzania..Mara umesha sahau ya Pemba na ule uchaguzi mdogo vijana wa Chadema walikipata cha mtema kuni!...au kwa sababu hawa ni CCM wajomba zetu, mama zetu na baba zetu?

Pengine yaliyokwisha tokea sii kwa kwa kiwango cha Zimbabwe lakini hakuna geni kabisa kwa nchi zetu -Yanatokea ktk nchi karibu zote za Kiafrika.. Mkuu -Ndivyo tulivyo, ajabu tunashangaa leo ya Zimbabwe hali sisi wenyewe tayari tumeisha weka maji kichwani...ZANU PF haina tofauti kabisa na CCM ktk swala la kura na nadhani katika malengo ya chama cha CCM ushindi wa kura ndio umepewa kipaumbele katika katiba yao.. Ushindi ni lazima..

Mimi nafikir mada hii ilikuwa inazungumzia zaidi kuhusika kwa wazungu na propaganda zao dhidi ya Mugabe na kwamba wanajaribu kila njia kuepusha ukweli kuwa wao ndio kichombezo kikubwa cha maafa yote..
Fundi mchundo,
Mkuu ile habari ulosema hapo nyuma nadhani hukuelewa kwamba mfanyabiashara unayemzungumzia ni Mimi mwenyewe! Mimi ndiye nilikwqenda bank kujaribu kunua kitu Zimbabwe na kikampuni changu uchwara. Nilikataliwa na maelezo ya mhudumu wa bank alisema Zimbabwe ipo ktk sanction sasa wewe unachotaka kusema bila kuonyesha jinsi wewe ulivyojaribu na kufanikiwa ni maneno ya mgahawani...
Werwe kama upo nje iwe Marekani ama Uingereza naokuomba nenda bank yako na wambie unataka kufanya kununua kitu Zimbabwe ambacho unahitaji kutuma hizo fedha kwa kampuni X... kihsa sikia majibu yao.
Halafu swala la Pamba ni jamaa yangu kabisa anayeshughulika na ununuzi wa Pamba Zimbabwe hivyo huwezi kunambia kitu ambacho binafsi nakifahamu vizuri..
Mugabe ni kiongozi mbaya kama alivyokuwa Saadam hHussein na alitakiwa kuondolewa lakini inapotumika swala la WMD kuwa ndio sababu ya uabya wake hapo ndipo napopinga mimi na kusema hawa wazungu washenzi tu. Mugabe ana ubaya wake lakini mengi wanayoyafanya hayamuumizi Mugabe isipokuwa wananchi wa Zimbabwe kama walivyoumia Wa Iran enzi zile walipowekewa vikwazo.. Kama wanavyoumia Wa Cuba kwa sababu tu wao ni Wajamaa!... Cuba hata sikui moja haijawahi kuitishia Marekani kiuchumi wala kisiasa na kusema kweli sioni kabisa sababu ya kuwawekea vikwazo...wanaoumia ni wananchi sio Castrol na utawala wake...
Hii ndio point yangu na hakuna mahala nimempongeza Mugabe kwa ubabe wake wala sinyta mpongeza Morgan kwa kutumiwa na hawa wazungu...
Mwisho, maamuzi yangu yote yametazama Zimbabwe ya kesho baada ya Mugabe na hakika kama Morgan atakuja kuchukua nchio basi tumejivunmia Somalia nyingine!...
Mtakuja nambia.....nakomea hapo ktk mjadala huu..

Mkuu,
Ewaaa...asante sana kwa maelezo yako sasa naona ndugu zangu hapa labda wataelewa kama siyo kupata ka-mwanga kidogo.
Waarabu wameshashtukia suala zima la western propaganda ndiyo maana wanayo El-Jazeera na Latin America nao wanayo Telesur,tumebakia sisi tu waafrika kumeza kila kitu wanachosema BBC ,CNN,Fox,Deuchevelle .. amkeni ndugu zangu....
 
Mwanatanu,
Mifano ni mingi sana yaani hata haina idadi... tazama kina Mobutu wa Zaire...walisifiwa sana, Lumumba akapewa matusi yote hata kabla hajatawala..Wazungu walipomchoka Mobutu ndipo kila mwafrika alipomwona ubaya wake.. Baada ya mzungu kusema! na wakaingizwa mjini bila kufahamu kwamba hatua watakazo chukua dhidi ya Mobutu zitakuja kuwaangamiza zaidi..

Ndio maana nawauliza Waingereza ilikuwaje kwa miaka 17 Mugabe alikuwa kiongozi shujaa na kapewa sifa zote! Tazama kina Mubarak huyu katawala toka Zimbabwe haijapata Uhuru wake hadi leo anapeta pamoja na kwamba kairudisha Egypt nyuma kishenzi nchi imegeuka kuwa na Utawala wa Kijeshi na Kidikteta wanakufa watu kila siku hakuna anayesema kitu sii Muingereza wala America, wapinzani wote wa Mubarak wanaitwa Terrorist pamoja na kwamba wamejiandikisha kisheria kama vyama vya Upinzani.
Kila kona ya Afrika mchezo ni huo huo na hakuna hata siku moja tumejifunza kutokana na yale yaliyotangulia.... Bila shaka nakubaliana na Nyani Ngabu -NDIVYO TULIVYO!

Mkuu,
Ngoja tuongezee list uone jinsi UK na Marekani walivyondumila kuwili Omar Bongo wa Gabon yuko madarakani tangu 1967,Theodore Obiang Nguema wa Equatorial Guinnea naye yuko madarakani tangu 1979,Museveni tangu 1986 na katiba kaibadili ili atawale kipindi cha tatu! na wazungu hawa hawa wako kimyaaa na wala hakuna cha economic sanctions wala nini ..wanaona Zimbabwe tu!
 
Mkuu,
Ngoja tuongezee list uone jinsi UK na Marekani walivyondumila kuwili Omar Bongo wa Gabon yuko madarakani tangu 1967,Theodore Obiang Nguema wa Equatorial Guinnea naye yuko madarakani tangu 1979,Museveni tangu 1986 na katiba kaibadili ili atawale kipindi cha tatu! na wazungu hawa hawa wako kimyaaa na wala hakuna cha economic sanctions wala nini ..wanaona Zimbabwe tu!
This sounds interesting buddy. Let's start with Mu7, Omar Bongo and Nguema!

I know, Mugabe is the subject currently, but what are we doing against these other 'tyrants'?
 
And people, why do you defend G.W.B? Cause he is a better leader? Remember Mugabe is a leader of a liberation movement... The situation in Zimbabwe has 2 sides to blame - 1. Mugabe's intelligence and 2. the Wests ignorance!

Remember, whats happening in Zimbabwe is civilian and not military, as a matter of fact Mugabe is not in control of the military... We all know the economical sanctions by the West to Zimbabwe has absolutely NOTHING to do with the Zimbabwean peoples will - Zimbabwean people never begged for the western imperialists to drag their own economy into a loophole - this situation between the west and Zimbabwe is personal, believe me if it wasn't the British would not have banned the Zimbabwean Cricket Team from playing any matches in England... If there was black farmers involved the west would not have taken such harsh, pointless and drastic measures!

Tsvangarai is a western appeaser, he must never rule Zimbabwe, the last thing we want for a stable Africa is a western puppet.

In other words the fundamental inequity at the rock bottom of this unfolding disaster-the theft of what is now Zimbabwe by the racist British colonials from her black indigenous rightful owners-has NOT been put right.

Do not depend on the BBC and other western media for their news over Zimbabwe. You should find out who gave Nelson Mandela hope while he was incarcerated - Comrade Robert Gabriel Mugabe!

While Mugabe was leading the valiant guerrilla resistance against the racist white government, Tsvangarai was working a job for the racist white regime!
 
Back
Top Bottom