Ndo maana Africa hatuendelei. Mtu tunayetarajia atusaidie na awe msitari wa mbele katika kuandaa katiba mpya, anaanza kusema haoni sababu ya kuibadili katiba iliyopo. Bado hata bosi wake anaposema kuna umuhimu wa kutoa katiba mpya, yeye anasema haoni sababu ya kujiuzulu. Hii ni akili au ni matope?
Wapo watu wengi kweli wanafaongoza wenzao kufanya kazi ambazo hata wenyewe hawazijui. Ninakumbuka siku moja tukiwa chuoni tukamwita dean wetu wa faculty. Tukamweleza kuwa hatufanyi practical na madarasani hamna viti. Alitujibu kuwa tujifunze kuzoea matatizo kwani hata yeye ni mwenyekiti wa bodi ya shule moja ya kata na wanafunzi wa hiyo shule wanakalia ndoo. Tulimzomea kweli huyo mama lakini hata hivyo tulimaliza chuo bila kufanya practical.
Kwa mfano huo Huyu Dean Werema na Kombani, wanajua kuwa watanzania waendelee na matatizo yaliyopo maadam wao wanapata Mshahara. Wakiulizwa tufanye mabadiliko gani watakuambia tulinganishe katiba yetu na ya DRC, Lyibia, Uganda tuone na wao wanafanyaje. Ukiwaambia kwa nini tusiandike ya kwetu wenyewe au tuchukuae ya kenya au ya Amerca watakuambia Kenya na Amerca ziko juu kiuchumi au hali ya hewa ya kule haifanani na ya hapa.
Umefikia wakati wa watanzania haswa Watanganyika kuanza kumkataa kila mtu aliyekabidhiwa madaraka akiwa bado mvivu wa kufikiri.
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ametetea kauli yake ya hivi karibuni iliyotaka Katiba iliyopo ifanyiwe marekebisho badala ya kuandikwa upya na kusema, yalikuwa ni maoni yake binafsi na si msimamo wa serikali.
Katika mazungumzo yake na gazeti hili Werema alisema, sikuzungumza kwa kificho na kila mtu alinisikia nikitoa maoni yangu, sielewi ni kwa nini jambo hili linakuzwa, sasa hao wanaotaka nijiuzulu nao wajiulize, ina maana mwanafunzi akiwa wa mwisho kwenye mtihani darasani watamwambia ajiuzulu kusoma?
Wewe ni Jaji Mkuu usiwabembeleze hawa wana chadema.
Luteni said:"sasa hao wanaotaka nijiuzulu nao wajiulize, ina maana mwanafunzi akiwa wa mwisho kwenye mtihani darasani watamwambia ajiuzulu kusoma?"Ivi hawa waandishi wa habari wa kibongo wakoje? Yani AG anajifananisha na mwanafunzi afu haulizwi maswali?! Kujiuzulu kwa mwanafunzi aliekua wa mwisho ktk mtihani ni kuachishwa shule au kurudia darasa. Sasa taaata mura werema asubiri aidha kurudia darasa au kuachishwa masomo sasa.
sijui atajibuje akiulizwa hilo swaliJe ile ya Dowans nayo ni maoni yake au msimamo wa Serikali?