Werema: Nilichoongea ni maoni yangu si msimamo wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Werema: Nilichoongea ni maoni yangu si msimamo wa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jan 4, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ametetea kauli yake ya hivi karibuni iliyotaka Katiba iliyopo ifanyiwe marekebisho badala ya kuandikwa upya na kusema, yalikuwa ni maoni yake binafsi na si msimamo wa serikali.

  Katika mazungumzo yake na gazeti hili Werema alisema, "sikuzungumza kwa kificho na kila mtu alinisikia nikitoa maoni yangu, sielewi ni kwa nini jambo hili linakuzwa, sasa hao wanaotaka nijiuzulu nao wajiulize, ina maana mwanafunzi akiwa wa mwisho kwenye mtihani darasani watamwambia ajiuzulu kusoma?
   
 2. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  maoni yako uwe unaongea kwa Mkeo.
  But ukija kwa waandishi wa habari unatakiwa uwe unayasema yale yaliopelekea uajiriwe....sawa?
   
 3. k

  kingmaker Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hawa viongozi sijui kwanini hawajui maadili ya uongozi.....hivi kweli wewe AG unaweza kutuambia maoni unayotoa ni yako binafsi....aliyekuambia tunataka maoni yako nani?? Unapofungua domo lako ujue unaongea kwa niaba ya mwajiri wako na usitake kujifanya ni maoni yako binafsi...subiri ustaafu ndio uwe unatoa maoni yako kwa vitukuuu vyako na vijukuu!! Eboo
   
 4. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe ni Jaji Mkuu usiwabembeleze hawa wana chadema.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  mkuu,

  Werema hana cheo cha jaji mkuu....kama umesoma mada vizuri inataja cheo chake.
  karibu jamvini, umeingia kwa mwendo mdundo!
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi kama chenge aliweza kuchomoa kwa vijisenti na rada ni mtu gani anaweza kuwajibika au kujiwajibisha.

  Ndio Maana hata Lowasa mpaka leo ana ujasiri wa kusema alionewa saabu anajua anajua michezo kama hii ni ya kawaida tu. ni modulus operandi ya CCm
   
 7. shejele

  shejele Senior Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mi nilidhani Werema ni mwanasheria mkuu wa serikali,kumbe ni jaji wa chama fulani!!

  Werema tunategema out put yako iwe genuine, usijifananishe na mwanafunzi bwana.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Why did he have to wait for this long kusema hili? Kwa nini wakati ule hakusema in bolds kwamba this is my own opinion. Yoote hii inatokana na uchanganyaji wa siasa na taaluma. Nadhani alijibu vile akidhani anawafurahishwa wanasiasa hasa bosi wake JK. Anapoona upepo umebadilika naye anataka kubadilika. Shame on ths guy!!!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tunakipawa cha kutoa majibu mepesi kwenye masuala mazito! Nakumbuka Kauli tata za Kikwete Mimba na Ukimwi ni vihere here, wakina mama zaeni watoto wa kike wengi kuna mashindano ya urembo...kitu kama hicho, wanafunzi wenye watoto maziwa kutiririka etc etc.....akibanwa basi husingizia waandishi hawakumwelewa ama alikuwa anatania tu.

  Werema naye yuko kama bosi wake!
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni mkuu wao hana uwezo wa kukemea wanaotoa kauli tatanishi ndio maana mawaziri huwa wanakurupuka kusema chochote wakijua hakuna wa kuwakemea. Subiri uone Kombani atakavyojitetea atasema niliposema serikali haina hela za kuandika katiba mpya yalikuwa maoni binafsi.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Werema, huu ufafanuzi wote wa kazi gani?

  Kama ni watu kuuaua kutokana na kauli yako hiyo iliyopungua busara mpaka leo hii siku nyingi tungekuwa tumeshazika na kusahau machungu.

  Cha msingi wewe jipime tu kwamba baada ya kupingana na kauli ya bosi wako ambaye ni rais na pia kutuita sisi waajiri wako MA-BATA tunaobwatuka ovyo bila kufahamu kitu juu ya katiba, uone kama bado huduma zako kwetu ni muhimu.

  Hata hivyo usichelewe sana katika kumpitia na yule mwenzio Celina Kombani pale wizarani.
   
 12. Wameiba Kura

  Wameiba Kura JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aibuuuuu, AG mzima ana ongopa, eti self opinion, maoni binafsi ni kwake na familia yake si kwa Public, ananza spinning hana lolote
   
 13. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Mama tartibu! kawa jaji mkuu lini tena?
   
 14. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 135
  Kwa nafasi yake hapaswi kuwa "mwanafunzi wa mwisho" bado yule mwenzie Kombani hovyooo!
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Unamdanganya mwayego..huyu ni wa kumrudisha kulekule Mirembe alipokuepo.
   
 16. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,871
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Waziri mzima kujilinganisha na mwanafunzi wa mwisho ni ujinga mwingine anauonyesha ina maana yeye amekuwa wa mwisho wapi kati ya mawaziri wenye busara au? Nikiunganisha dots kuna lecturer wake aliwahi kusema hata darasani Werema alikuwa dully sana.
   
 17. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nonsense Werema!!!
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Huku ni kukosa miiko ya uongozi na kutokuwa na maadili ya kazi. Huwezi kuwa kiongozi mkubwa serikalini ukasema utaoa maoni yako na si maoni ya serikali, kama serikali ikitekeleza maoni tofauti na yako ina maana wewe uko pale kama picha una imani na fikira tofauti, kwa hiyo hufai kuwepo pale.

  Tunarudi kulekule, sasa hivi serikali haina msemaji kila mtu anasema hovyo tu kila mtu akikutana na waandishi wa habari anasema analopenda, akichemka anaita tena waandishi wa habari, ni upuuzi na uozo serikali.
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi Jk kwenye hotuba yake angesema haoni umuhimu wa katiba mpya na iliyopo inafaa, huyu jamaa angeibuka na anachokisema hivi sasa?
   
 20. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwenye tume ya katiba mwanasheria mkuu wa serikali lazima awemo sasa kama yeye binafsi haoni umuhimu wa katiba mpya atakuwa akifanya nini.
   
Loading...