Werema: Nilichoongea ni maoni yangu si msimamo wa serikali

Halafu Celiina Kombani naye akija aseme kuwa ni maoni yake hayakuwa ya Waziri wa Sheria na Katiba.. hawa watu huwa wanapoitwa kutoa maoni kwa vyombo vya habari wanajisahau kuwa wana nyadhifa fulani? Tukiwaendekeza hata shetani atajitokeza na kudai kuwa hajawahi kuisikia Jehanamu! na atasema hayo ni maoni yake binafsi!
 
Halafu Celiina Kombani naye akija aseme kuwa ni maoni yake hayakuwa ya Waziri wa Sheria na Katiba.. hawa watu huwa wanapoitwa kutoa maoni kwa vyombo vya habari wanajisahau kuwa wana nyadhifa fulani? Tukiwaendekeza hata shetani atajitokeza na kudai kuwa hajawahi kuisikia Jehanamu! na atasema hayo ni maoni yake binafsi!

The funny thing ni kwamba hivi hawajiulizi na kwa nini hayo wanayoita maoni binafsi huwekwa kurasa za kwanza za magazeti?
 
Mwisho na JK naye atatuambia alichosema juzi ilikuwa ni maoni yake binafsi na si kama raisi.
 
Nilikuwa sijawahi kuona serikali ya aina hii, hakyanani tembea uone. Yaani kila mtu anaamka na kusema kivyakevyake vyake tu!?? Akiulizwa, nilikuwa natoa maoni yangu. Labda JK naye atabanwa kwenye chama chao aje aseme alikuwa anatoa maoni yake binafsi. Nadhani haya ni ya Musa tu, Mpaka miaka mitano iishe tutayaona na filauni!
 
Hivi Jk kwenye hotuba yake angesema haoni umuhimu wa katiba mpya na iliyopo inafaa, huyu jamaa angeibuka na anachokisema hivi sasa?

Hii serikali yetu ni ya kuchora tena kwa penseli, hawa jamaa wameshawadharau sana waTZ na ndio maana hawajali umakini wa wanachosema ama fanya.
 
Werema angeamua kufunga domo lake kila akiongea ni pumba tu....sasa yeye mwansheria mkuu wa nchi....anajifananisha na mwanafunzi...wa mwisho???ahahhaa kwelii mwanasheria tunaye mwaka huu.....hana subira wala busara...
 
Wewe ni Jaji Mkuu usiwabembeleze hawa wana chadema.

ushabiki shabiki tu hata kuelewa hamuelewi ndo maana mnabuluzwa sasa unaleta ushabiki wa vyama mpaka kwenye mambo muhimu ya kitaifa hapa sio jangwani na msimbazi! You deserve to be a great sinker and not a great thinker.
 
MWANASHERIA Katika mazungumzo yake na gazeti hili Werema alisema, "sikuzungumza kwa kificho na kila mtu alinisikia nikitoa maoni yangu, sielewi ni kwa nini jambo hili linakuzwa, sasa hao wanaotaka nijiuzulu nao wajiulize, ina maana mwanafunzi akiwa wa mwisho kwenye mtihani darasani watamwambia ajiuzulu kusoma?

Kwa manenoyake kama yanavyosomeka amekiri kuwa ni mwanafunzi wa mwisho darasani na tumwache tu.
Werema si wewe ulifunga mjadala, sasa ulifunga mjada kwa mkeo au kwa umma, maana sasa unasema ni maoni binafsi.
Ulipoongelea Ikulu hukujua kuwa hiyo tu ilitosha kuwa kauli ya serikali licha ya wewe kuwa AG.
Werema umejidhalilisha sana.
 
Kama yalikuwa ni maoni yake angesema toka mwanzo kwamba ni maoni yake binafsi badala ya kuleta taharuki na mkanganyiko usio na sababu. lakini pia lugha yake imekuwa ya kibabe utadhani ni mwanajeshi!
 
Halafu Celiina Kombani naye akija aseme kuwa ni maoni yake hayakuwa ya Waziri wa Sheria na Katiba.. hawa watu huwa wanapoitwa kutoa maoni kwa vyombo vya habari wanajisahau kuwa wana nyadhifa fulani? Tukiwaendekeza hata shetani atajitokeza na kudai kuwa hajawahi kuisikia Jehanamu! na atasema hayo ni maoni yake binafsi!


(hapo kwenye red & bold)

mithili ya kuku mwenye kiu ya maji. ukitia maji kwa bakuli ukamuwekea, hukanyaga kingo za bakuli na kumwaga maji yote kabla hata ya kuyanywa.

hizi ndiyo akili za viongozi wetu.

wanakuwa na kiherehere cha kurekodiwa ili jioni wakiwa kwenye mahekalu yao wajione kwenye Tivi.
 
Na angesemaje kama Rais wake angekataa suala la katiba? Werema angejiita kuwa ni mwanafunzi wa kwanza kwenye mtihani?
 
Wewe ni Jaji Mkuu usiwabembeleze hawa wana chadema.



Nadhani ulienda sisiemu kuongeza idadi ya mbumbumbu na hukustahili kuwa among great thinkers. Hujui tofauti ya Jaji mkuu na Mwanasheria mkuu wa Serikali!
 
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ametetea kauli yake KUWA sasa hao wanaotaka nijiuzulu nao wajiulize, ina maana mwanafunzi akiwa wa mwisho kwenye mtihani darasani watamwambia ajiuzulu kusoma?

Mwanafunzi akiwa wa mwisho kwa maana ya kufeli, hufukuzwa; tatizo wewe huna wa kukufukuza ingawa ni kweli ulivyojilinganisha na mwanafunzi wa mwisho labda ndivyo ulivyo.
Hivi JK, hatuna wanafunzi wa kwanza wanaofaa kushika nafasi hiyo?
 
du kazi ipo waziri anajilinganisha na mwanafunzi anayekuwa wa mwisho darasani!! sijui hii katiba itakuwaje maana huyu jamaa naye atakuwepo sasa kama yeye ni mvivu kufikiri ataweza kweli kushauri yalio mema?
 
Hii ni "pressure" ina mount katika serikali... safi sana people should exert more pressure mpaka wakome. Nadhani watanzania hawa sio wa miaka ya 80, these are people wanaotaka kwenda kwenye next level... wakulu wamekuwa-pressured mpaka sasa wanatapatapa.
 
Back
Top Bottom