Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,234
- 1,503
Sisi hapa Mwanza sidhani hata kama zimefika bar 7. Maana ikifika asubuhi tu wamekata na kuurudisha ni mpaka saa kumi na mbili jioni. Nasikia Dar zimefika bar 52, hivi ni kweli? Maana bwana .....Dar ndiyo kilakitu. Isije ikawa kelele zimepungua kwasababu Dar zimefika bar 52, kumbe sisi huku 'mikoani' bado tunaumia. Naomba tujulishane......hapo ulipo zimefika bar ngapi. Ili nijifariji na kauli ya wahenga "kifo cha wengi harusi".