Morgan Fisherman
JF-Expert Member
- Dec 10, 2017
- 1,933
- 2,329
soma kitabu kinaitwa power of subconscious mind
hama na mji ikiwezekana kupata exposure mpya
hama na mji ikiwezekana kupata exposure mpya
Achana hao wasiojua chochote na hawajawahi kukutana hayo matatizo , utasaidiwa tu mimi nataka nikusaidie bure bila hata mia .Hii yakutojishughulisha imetoka wap?? wap umetuona hatujishughulishi?? Ndugu umetumwa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu huyu umelogwa yeye na familia yake staili ya kuwaua huku wakiwa hai , sawa na injini inatolewa inabaki housing tu .![]()
Kuna familia zina laana ya asili
Hili naliandika kwa uchungu mno kwakuwa waathirika ni wengi na hata pengine baadhi ya wana JF ni wahanga. Maisha yanatufunza mengi yanatuonyesha mengi na yanatufunulia mengi Kuna familia zimebarikiwa, hawa maisha yao ni full shangwe mafanikio na baraka kwao si kitu cha kuuliza , kwao ishu za...www.jamiiforums.com
Kuna familia zina laana ya asili
Sent using Jamii Forums mobile app
Hao ni watoto hawajui chochote mkuu na dunia hawaijui haipo Kama wanavyodhani na kudanganyana huko kwa walokole uchwara .Thanks bro.. Kuna wanaofanya mdhaa wakidhani ninayo yaongea ni just a talk.. kwa kuwa hawajakutana na Watu wagiza kwenye familia zao.. hawamuona shetani anavyotesa live .... ila nimeshughudia mengine hata siku yaweka kwenye andiko langu maana akina tomaso ni wengi na wanajua kukejeli sana.. Ipo siku Mungu ata waonyesha kwa vitendo ili wapate kujua uhalisia Giza na Nuru.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Haya Maumivu ya Moyo na Msongo wa Mawazo.. Na Taarifa za Mateso ya Ndugu zangu yanavyo nitesa akili.. maana Degree niliyosoma haina samani vyeti viko kabatini.. Siiajiriki.. Biashara nilizo fanya zote zimekufa.
Alafu kila siku unauza vitu vya ndani ili upate kula .. Ukijaribu kusema usamehe ili Mungu afanye kazi yake, Ghafla unapokea Simu ya Ndugu flani kawa kichaa mara kesho Mama tatizo hili mara kesho kutwa Unaambiwa Walio wazulumu wanauza nyumba yenu Mara ghafla Ndugu yako mwingine Ameacha kazi anakunywa tu pombe mpaka ana lala mitaroni. Ghafla unaambiwa ndugu mwingine Kachanganyikiwa ameonekana ana ongea mwenyewe njiani.. ukimfuatilia unaambiwa Ana lala kwenye Mito maporini..
AJABU WATOTO WOTE TULIZALIWA KWENYE FAMILIA BORA BABA ALIKUWA BOSS MKUBWA SABA BANK KUKU(BOT) TULIZALIWA WAZIMA WOTE MPAKA WATU WANAFIKIA MIAKA 30 WENGINE 35 GHAFLA WOTE WANACHANGANYIKIWA ALAFU WANO TUFANYIA WANA TAMBA KABISA MITAANI KUWA WATA TUMALIZAA.. Hivi unadhani kama yote haya yanatoke Je Hayo maandiko yako yangekuwa yana wezekana yasinge tekelezeka ?
Unajua haya ya Ayubu ni wakati Mungu anaongea na wanadamu ana kwa ana, ni wakati binadamu alihitaji kumwaga damu ya wanyama kwenye madhabu ili kuutafuta upatanisho na mungu, ila baada ya Mungu kuimwaga damu ya mwanaye Yesu kristo kwa ajili ya upatanisho wa kudumu, Hata Majaribu ya mateso kwa mwanadamu aliye achiwa Roho mtakatifu ambao ni sisi wa kizazi hichi.. hatufanyiwi mateso ya aina ya Ayubu kamwe.. haya yanayotokea katika Familia yangu ni nguvu za giza na mikono ya wanadamu wenye Hila.. Ipo siku nitazishusha hila zao kuzimu ili iwe fundisho kwa vizazi vyao vitakavyo bakia hapa duniani. Haijalishi kama hii itakua ndio dhambi yangu kuu katika maisha yangu ila Naamini Mungu huyo huyo aliye wabeba miaka yote wakatutendea haya yote ndio Mungu huyo huyo atakaye ni beba na Mm nitende hayo hayo..Kumbuka kua na Imani ndugu yangu, kama wewe ni mkristo kumbuka mateso ya Ayubu hakuna gumu lisilokua na mlango wa kutokea.. mshinde shetani usilipize kisasi endelea kumuomba Mungu ombea ndugu zako peleka nguo zao kwa wachungaji huenda wewe ndo utakaekuja kuvunja hiyo mikosi na laana katika familia yenu
Sina kitu mkononi nimefilisika kabisa, ila naomba kama unaweza niondolea hawa watu wawili wanao itesa familia yangu. Nitakupa Hekari 3.5. zipo Morogoro hichi ndicho nilichofanikiwa kumiliki kwa mkono wangu na jasho langu maishani mwangu.
Nimefilisika hakuna hata senti ya kula, ila Kama una njia ya kuwaondoa hawa watu wawili ili ndungu zangu watoke kwenye mateso wanayofanyiwa basi ntakupa hizi ekari3 na nusu.. zipo Mbele kidogo ya Chalinze eneo linaitwa Bwawani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,Andiko lina sadifu kilichopo katika mindset yako.Unataka NINI?Unataka kuandamwa na mikosi na Balaa?Untaka kuandamwa na Baraka na Neema?Mungu yupo na I Assure you anaweza.Sitaki kukupa faraja nataka nikupe changa moto.Mjaribu Mungu.Badala ya kufocus kutatua shida zako embu mwachie yeye then focus on helping wale ambao wanashida zaidi yako.najua wapo wengi.MUNGU AKUPE NGUVUMaumivu yangu katika maandishi
Unaweza zoea "ukiwa" katika maisha yako kiasi kwamba ukiona mtu anacheka unajiuliza hivi huyu yupo dunia ipi?
Guys, kuna maisha na kuna mapito. Kuna laana na kuna kuchukiwa. Siku zote usiombe Mungu akachukia familia yako wala asitie laana kwenye familia yako maana
Kuna kusaga meno na kuna kulia machozi ya damu
Kuna kudharauliwa na kutemwa mate
Kuna kushushwa kabla huja jishusha
Balaa zaidi nikukutana na watumishi fake wanao taka kutumia mateso yako kukutoa hela kwa kivuli cha mungu kawaagiza utoe sadaka flani ili akusamehe. Amini nakuambia usiombe usiombee!
Utashughudia hatua za maendeleo ya wenzako na wewe utakuwa ngazi ya kukanyagiwa wawo wafike juu. Ogopa sana hasira za Mungu. Ogopa sana maana hata usali na kutubu vipi kama asha piga muhuri wa mateso katika uzao wenu utaomba aridhi ipasuke.
Kuna wakati huwa najiuliza mara yangu ya mwisho kuwa na tabasamu la kweli usoni mwangu ni lini, wala sikumbuki nalitafuta sana jibu katika kipindi cha miaka mingi nyuma silioni, kile ninaweza kiona kwangu ni huzuni, ukiwa, maumivu ya moyo, maisha ya siyo na ladha, kutengwa, kufungiwa gereza kuu la ajira, mikono yangu kuwa locked na pingu isifanye biashara.
Mifuko yangu imetobolewa isikae na hela, hisia zangu zime kuwa diluted na chuki usipende wala kupendwa. Macho yangu yamekuzwa nishughudie maendeleo ya wengine na akili yangu imefungwa isifanye chochote katika dunia.
Kila nisalipo naona kabisa sala zangu hazina nguvu wala hazi mfikii muumba. Nikiwaza ukiwa wangu tangu nikiwa na miaka 3 mpaka nafikia utu uzima huu, najiuliza ikiwa tuna ambiwa mungu halali wala hafungi macho ilikuwaje mimi na ndugu zangu tukayapitia yote yale na mpaka sasa nayapitia haya yote?
Huwa najiuliza maswali ya wapi jicho lake lilipo kuwa hata mimi na ndugu zangu tuka yapitia yote haya? Najiuliza ule mpango wa wenye hila kutudhulumu haki yetu ya amani hapa duniani na kumuuwa baba na kaka yangu mkubwa, na bado wameendelea kuangamiza ukoo wa baba yangu, je! Mungu hakuona? Bila shaka aliona je! Ukimnya wake kwa miaka yote hii 30 ni kwamba haoini mateso yetu?
Je, yanayoendelea mpaka sasa hayaja mguswa kutoa adhabu yake kwa wahusika? Je, kama kuna kisasi cha Mungu cha adhabu kwetu, let' say kwamba mababu zetu wali muudhi akaachia laana ikaja kwetu sisi wa kizazi cha 4, je katika kulia kwetu na kuomboleza bado adhabu hizo za mababu hazi sameheki kwetu?
Je, hawa wanao tumia uchawi kutesa familia nzima na bado wana raha katika maisha yao na bila aibu wana jisema wazi wazi kuwa wata mmaliza yeyote atakaye inua mdomo kudai haki au kuulizia kifo cha baba mzazi, je hawa wame mpa nini mungu ata awafanye watabasamu na kuishi katika nyumba yetu?
Je, inatupasa tuishi kwa kulipiziana kisasi kwa kuwa haki kwa mungu haipatikani? Je, na mimi nikibuni mbinu yangu ya kuwaangamiza wale wanao wafanya ndugu zangu kuwa vichaa na kuuwa wengine, mungu ata nilinda kama anavyo walinda wale? Je huu uchawi unao tumika kuuwa wasio na hatia umepewa baraka na maandiko? Kama jibu ni hapana mbona maandiko yana sema usimuache mchawi aishi ila hawa wanaishi na kila mwaka wanauwa na kutesa watu kwa magonjwa, je hayo maandiko hayatendi kazi kwa ulimwengu wa sasa?
Kuna mengi sana nimejiuliza bila kupata majibu sana sana naogopa kuishia kumkufuru mungu wangu, ila naamini sistahili haya nipitiayo sasa, kwa kuwa nimeshughudia baadhi ya watu mbali mbali wakifanya kufuru na ushirikina mkubwa ambao mm sikusubutu hata kuya waza ila wao wana ishi kwa mafanikio na baraka za kila wafanyacho, ila uzao wa mama yangu umekuwa na mateso makali tangu utotoni mwao na bado wanataabika mpaka leo hii, na ukitafuta kikubwa walicho mkosea mungu hukioni.
Namuomba mungu sana kabla ya kufa kwangu angalao anifungulie kosa langu na ndugu zangu ni nini nipate amani maana nimetafuta tangu tukiwa na miaka mi3 ni mateso katika hii dunia, najaribu kuwaza ndugu zangu kwa mri ule walimkosea nini mungu hata aruhusu wawe mateka wa nguvu za giza, mateso yao kwa miaka yao yote mpaka sasa! Sina maana ya kupinga kazi ya mungu ila nautafuta ukweli wa fedhea hizi katika familia mauwaji, dhuluma na kusoma na kukosa kazi, biashara haziendi, kuchukiwa kwetu na kudharaulika.
Natamani siku moja niandike kitabu cha mapito yangu ya adhabu ya laana za mababu zinavyo ni andama mm wa kizazi cha 4.
Watu wajifunze kuwa hata ukiwa mwema kwa Mungu kama kuna muhuri wake ulifanyika juu ya kizazi chenu huta epuka muhuri huo.
Sina kitu mkononi nimefilisika kabisa, ila naomba kama unaweza niondolea hawa watu wawili wanao itesa familia yangu. Nitakupa Hekari 3.5. zipo Morogoro hichi ndicho nilichofanikiwa kumiliki kwa mkono wangu na jasho langu maishani mwangu.
Nimefilisika hakuna hata senti ya kula, ila Kama una njia ya kuwaondoa hawa watu wawili ili ndungu zangu watoke kwenye mateso wanayofanyiwa basi ntakupa hizi ekari3 na nusu.. zipo Mbele kidogo ya Chalinze eneo linaitwa Bwawani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Matazi ya Familia yangu ni muhimu kutatuliwa kuliko Aridhi nisiyoweza ilima wala nisiyoweza iuza kwa kufungwa na Watu hoa hoa wanao zuia nisifanye chochote. Kuangamia kwao ni bora kwangu kuliko hiyo Aridh.. Maana hata ninge angaikia vipi kulima hakuna kitu nitapata kwa kuwa wanapambana na njia zangu zote kama ni biashara nisha hangaika kwa miaka zote zina kufa ajira zote zinakufa .. ikiwa nitafanikiwa maishani mwangu kwa wao kuangamia na kama ninacho weza kutoa ili niwe huru nianze upya bila wao wanao nifuatilia ni hiyo aridhi.. bora itoke, ili familia yangu nikombolewe kwenye nguvu zao za giza.
Asante kwa Ushauri kaka! lakini Embu niambie nitateseka hivi mpaka mwisho wangu wa maisha? Maana kwa Mungu nime mtafuta makanisa karibi yote makubwa na kwa watumishi wakubwa ila wote wameshindwa.. Sasa Nikaamua mwenyewe kumpigia Mungu Goti.. ila ndio Kwanza nikama Sifanyi kitu hakuna jibu kwenye mateso yetu.. Je unadhani unaacheaje kuwaza kujaribu upande mwingine.. Hivi ninavyo ongea nan wewe simjui mganga wala sija wahi enda kwa mganga.. pamoja na mateso yote miaka yote sikuenda kwa Mganga .. nimemkimbilia Mungu ila bado Mungu haja itoa familia kwenye mateso hayo.. Je unadhani Leo hii nikiwaza kufanya haya niwazayo.. ninakosea kweli??
Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka nimekuja Dm.. sija kukuta.. ukija naomba upitie Dm yakoJaribu upande wa pili ndugu yangu kama makanisani wsmeshindwa, kama kweli umechoka hilo Tatizo lako huwez kuangalia wapi pa kupata msaada popote tu utaenda
Pole snNisaidie bro.. nina hali mbaya sana! Kaka njoo Dm kama kuna mbinu yoyote sita jali .. nimechoka sana.. Mama yetu katulea kwa Hekima na busara katufunza kumcha Mungu.. na tume kuwa hivyo.. Ila Dunia haitupi amani.. Dunia inatutesa kwa upole wetu.. Nataka Niwe Katili kuliko Osama Biladen.. I got no other choice... Nimekuwa mwema sana ila wema wangu umezaa Maumivu makali sana.. NJOO INBOX PLS
Sent using Jamii Forums mobile app
Sikweli napingana na wewe 100%. Roho mbaya haijengi siku zote na daima.Simu yangu hainiruhusu kusoma uzi mzima ila ushauri niliogewa ni hauwezi kufanikiwa kama hauna roho mbaya.
Najisogeza kwa speed kwenye hii mantra.