Wenye miaka zaidi ya 30, kitu gani unajutia kufanya/kutofanya kabla ya kufikisha miaka 30?

Nafurahia zaidi nimekwepa mambo yanayowakumba vijana wenye 20s
  • Nimelala kituo cha polisi ila nashukuru siijui jela (vijana wengi kwenye 20s huishia jela kwa tamaa, makundi, vurudugu za damu kuchemka, n.k.
  • nilichukua tahadhari kukwepa magonjwa ya ngono
  • nimewahi kujaribu bangi ila niliacha (bangi ya Tz ni 50/50 waweza kudata)
  • sina mtoto wa nje ya ndoa
  • n.k.

Nachojutia zaidi nimewahi kupoteza muda kumpenda mwanamke ambae hanithamini,

Wengi sana wanaharibu maisha wakiwa kweny
 
Kutokuoa aisee maana nimetimiza 30 juzi tareh 26.4. Nina nyumba ila now ninaumwa basi nyumba nzima nipo peke yangu baba mzazi amefariki nina mama na babamdogo tu nao wanamajukumu yao basi dah nawaza ningekuwa na mke angenipa kampani kubwa sana.
Hapo huna cha kujutia mzee. Ungekua na mke ndo angeuza na hyo nyumba afu anakimbia kabisa!!
 
Kutokuoa aisee maana nimetimiza 30 juzi tareh 26.4. Nina nyumba ila now ninaumwa basi nyumba nzima nipo peke yangu baba mzazi amefariki nina mama na babamdogo tu nao wanamajukumu yao basi dah nawaza ningekuwa na mke angenipa kampani kubwa sana.
Mshukuru sana Mungu kwa uamuzi huo wa kutooa mapema. Ungekuwa na huyo mke huenda mpaka sasa usingekuwa mgonjwa tu ila marehemu kwa hayo maudhi ambayo ungepitia katika hali hiyo ya ugonjwa.
Uhuru ulionao una thamani, Furahia maisha kwa namna upendavyo.
 
Ni kuchelewa kupata mtoto ..

Nimepata mwanangu wa kwanza nikiwa na 30 kamili

Nilitamani kuwa na mtoto tuliepishana hata miaka 25

Lakini sijui nilichelewa wapi?

Yaani sinui kwakweli nilikuwa nafanya nini huo umri
Umri waemiaka 24-35 unakatika mapema sana

Kwasababu ratiba ya kijana hapo inakuwa imejaa kuanzi asubuhi hadi jioni
Dah nmejenga mapema aisee mpk ss nina miaka 30 nina nyumba tatu halaf sina msingi wa biashara ndo ilo nalo jutia
 
Kitu pekee nachojutia ni kuwaajir ndugu miaka hiyo. Cntakuja kurudia huo ujinga
 
Sina cha kunifanya nijute sana, nilivyonavyo havitoshi ila kuna watu hawana kabisa.
 
Back
Top Bottom