Wenye miaka zaidi ya 30, kitu gani unajutia kufanya/kutofanya kabla ya kufikisha miaka 30?

Nafurahia zaidi nimekwepa mambo yanayowakumba vijana wenye 20s
  • Nimelala kituo cha polisi ila nashukuru siijui jela (vijana wengi kwenye 20s huishia jela kwa tamaa, makundi, vurugu za kutaka kuonekana miamba, n.k.
  • nilipenda ngono kwenye 20s umri wenye matamanio na nguvu zaidi ila nashukuru nilijitahidi kujilinda (vijana wenye 20s huishia kuungua na uti, magono, ukimwi, n.k. kwa kusukumwa zaidi na miili kuzidi akili)
  • nimewahi kujaribu bangi nikiwa natamani kwa muda mrefu kuyajua yaliyomo ila nashukuru niliacha (bangi ya Tz ni 50/50 waweza kuwehuka, huogi, hujijali, n.k.)
  • sina mtoto wa nje ya ndoa
  • n.k.

Nachojutia zaidi nimewahi kuwe kwenye mahusiano ya kumpenda mtu ambae hanithamini (kufosi), kuwa na marafiki wa ovyo, kupoteza muda mwingi mitandaoni bila faida, n.k.

Wengi sana wanaharibu maisha wakiwa kwenye 20s sababu ya ugeni wa mapenzi, ugeni wa uhuru, kutaka vitu wasivyoweza kuvimudu (tamaa) , n.k.
 
Back
Top Bottom