DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Usiongee kama umekatwa kichwa nikupe mfano mdogo. Wilaya ya Ubungo ina Zahanati,Vituo vya afya na hospital 261 hiyo ilikua mwaka 2023 kati ya hizo hospital,vituo vya afya na zahanati za serikali hazizidi 35 sasa jiulize wakiamua kufunga watu watatibiwa wapi. Kama ungewahi kuhudhuria mikutano ya Aphtar hata mmoja ungeelewa umuhimu wa sekta binafsi kwenye afya nchi hii vingenevyo watu wangekufa kama kuku
Kwahiyo ndiyo serikali ifanye wanavyotaka wao! Si wagome tu.
 
Kwa kweli tuombe Mungu atusaidie hawa Private hospitals na NHIF wafikie muafaka

Wagonjwa wenye Bima ya Afya ya NHIF wanataabika sana

Mungu wa Mbinguni utusaidie!
Yap..
Kuna wagonjwa wamelazwa wanaendelea na tiba muda huu kwa kutegemea hiyo hiyo NHiF, imagine waambiwe kuwa kuanzia kesho huduma hakuna!
 
Safi sana,

Hii wizara kwa sasa inaongozwa kwa propaganda mtupu.

NHIF ipo taabani kila siku na jumbe za kuhuisha uanachama hata kama expiry date kwenye card bado miaka miwili.

Ni ubabaishaji tu na kusumbua watu zoezi lenyewe ni makao makuu ya mikoa tu.
 
Hao wanaokataa na wafanye kama hao wahindi sijui kelele za nini kwanza kila hospital inaingia mkataba kivyake na NHIF kwahiyo anayetaka kufanya kazi na NHIF afanye anayekataa akatae.
Kila hospitali inaingia mkataba kivyake ila zote zinakuwa chini ya Umoja wao..

Na hivyo hivyo hata kila daktari anasoma kivyake na anafaulu kivyake ila wote wanakuwa Chini ya Baraza la madaktari nchini na ndo wanaotoa leseni..

Sasa mantiki yako sijaielewa tangu mwanzo..
Nini hasa Hoja yako?
Kwamba watu waendelee kuface unyanyasaji wanaofanyiwa?
Kwamba wenyewe wapate hasara kwa kuifaidisha serikali?

Kwa mujibu wa Takwimu zangu za Haraka Hospitali 80% ni za Private na Serkali ina 20% tu ya Hospitali zote..

Sasa sijajua kwako wewe unatetea nini Hasa kwamba Wakubali unyanyasaji kwa manufaa ya nani hasa?

Nipo tayari kuweka mjadala na wewe wa wazi kama uko tayari kutumia takwimu na facts
 
Kwahiyo ndiyo serikali ifanye wanavyotaka wao! Si wagome tu.
Hapana ila serikali hii katili haijali kuhusu maisha ya watu. Mkuu kuendesha hospital ,zahanati au kituo cha afya si lelemama ni gaharama kubwa naweza sema biashara ya afya ina kodi nyingi na running cost kubwa..
1.TRA
2.Kibali cha wizara kwa mwaka
3.Kibali cha maabara kwa mwaka
4.Osha
5.Fire
6.Kodi ya manispaa ya leseni.
7.Kodi ya jengo ya TRA
8.Kodi ya mwenye nyumba kama umepanga.
9.Tozo mbali mbali za mtaa/ Kata au halmashauri
10.Mishahara ya wafanyakazi tena hapa wanataka kila kada uwe na watu angalau wa tatu wakati wao hospital zao unaweza kuta hata mtoa dawa hamna au zahanat haina daktari na safi tu.

Hapo bado hujanunua vifaa tiba na dawa.
 
Wizara ya afya inafanya kazi kubwa sana kusaidia Wanachama wa Mfuko wa Bima ya afya unakua na manufaa kwao bila kuasiri uhai wa Mfuko. Maboredho hayo yameongeza huduma nyingi Muhimu na dawa ambazo hazikuepo awali.
Kumbuka hao wanachama wanakatwa hela zao.
 
Kila hospitali inaingia mkataba kivyake ila zote zinakuwa chini ya Umoja wao..

Na hivyo hivyo hata kila daktari anasoma kivyake na anafaulu kivyake ila wote wanakuwa Chini ya Baraza la madaktari nchini na ndo wanaotoa leseni..

Sasa mantiki yako sijaielewa tangu mwanzo..
Nini hasa Hoja yako?
Kwamba watu waendelee kuface unyanyasaji wanaofanyiwa?
Kwamba wenyewe wapate hasara kwa kuifaidisha serikali?

Kwa mujibu wa Takwimu zangu za Haraka Hospitali 80% ni za Private na Serkali ina 20% tu ya Hospitali zote..

Sasa sijajua kwako wewe unatetea nini Hasa kwamba Wakubali unyanyasaji kwa manufaa ya nani hasa?

Nipo tayari kuweka mjadala na wewe wa wazi kama uko tayari kutumia takwimu na facts
Unyanyasaji gani unaozungumzia wewe! NHIF wao wanalipa kulingana na bei ya soko lakini nyie kina bwana tamaa na msio na utu mnataka malipo mara dufu.
Unasema sekta binafsi wanamiliki 80% ya hospitali nchini sawa lakini kumbuka zaidi ya 80% hizo hospital zimeanzishwa baada ya kuanzishwa NHIF ili wajipigie pesa na utajiri wa haraka haraka sasa wao wakubaliane na NHIF wasitishe watu kwa sababu manufaa zaidi wanayapata wao kuliko hicho mnachokisema eti wananchi ndiyo watateseka,kwanza jiulize hao wanaotumia bima ya afya ni asilimia ngapi kati ya mamilioni ya Watanzania.
Hawa watu wanatetea matumbo yao na wala hawatetei wananchi.
 
Samahani sana kwa majibu nitakayotoa mbele....

Kama wewe ni msomi..
Nakuhakilishia kabisa Waliokusomesha wamepoteza pakubwa sana..

Sasa nisililize kwa makini sana..
Nakujibu vizuri sana..

Hoja ya kwanza umesema Uanzishwaji wa Hospitali Nyingi ulitegemea NHIF

Sijui umri wako..

Ila ngoja nikupe kidogo Historia mwaka 2001 Tanzania Rasmi ilianzisha sheria ya Bima ya Taifa na ikaanza implementation yake mwaka 2002..
Na ilikuwa Lazma kwa Watumishi wa Serikali mwaka 2003..

Malipo ya Bima kwa Private sector yalianza Rasmi mwaka 2004 bila kusua sua...

Sasa Takwimu za kipindi hicho Serkali ilikuwa chini sana kwa Kuwa na Vituo vyake vya afya na hospitali walikuwa wanamiliki chini ya 30% ya Vituo vyote na hospitali..

Na ndo maana Hospitali nyingi Za private na FBO zilipewa hadhi ya Hospitali za Mkoa na hospitali za wilaya Zikiitwa DDH na DRH..
(designated District hospital na Designated Regional Hospital)

Miaka Ya nyuma Kipindi bima hakuna ndo miaka Vituo vya serkali vilikuwa vichache sana..
sasa sjui wewe Takwimu zako unazipata wapi au ni umri wako ulikuwa mdogo pengine..
Vituo vingi vya afya na Hospitali vilijengwa kipindi.cha Kikwete na Magufuli..

Hoja ya pili umesema kuwa Hospitali inapata Mapato kupitia NHIF na wanatajirika kupitia hayo.

Katika Taasisi inayoongoza kwa kudaiwa na kukata Madeni ya watu nafikiri ni Moja ya Taasisi ambayo ingechukua Tuzo..
Chukua mfano hospitali hutuma madai ya 12 Mil ila inalipwa 3mil na kubaki inadai 9 Mil..

Visingizio vimekuwa Vingi sana kuhusu malipo sasa wameamua kabisa na bei wazishushe..

Ingekuwa inafaidika unafikiri wangegoma kuchukua pesa zao wasitishe matibabu ya wagonjwa?

Ni taahira peke yake anayeweza kudhania kila kitu kipo kisiasa

Hoja yangu:Kuhusu Kitita

Tudiscuss Bei za Dawa na Huduma Kwa Kitita cha mwaka 2016, January 2024 na hiki kipya cha March 2024..
Kipi kimefanya washushe gharama za bei wakati Soko la bidhaa bado liko juu?

Ulitaka tujikite hapo kama wasomi na sio kama waropokaji ..
 
Hapana ila serikali hii katili haijali kuhusu maisha ya watu. Mkuu kuendesha hospital ,zahanati au kituo cha afya si lelemama ni gaharama kubwa naweza sema biashara ya afya ina kodi nyingi na running cost kubwa..
1.TRA
2.Kibali cha wizara kwa mwaka
3.Kibali cha maabara kwa mwaka
4.Osha
5.Fire
6.Kodi ya manispaa ya leseni.
7.Kodi ya jengo ya TRA
8.Kodi ya mwenye nyumba kama umepanga.
9.Tozo mbali mbali za mtaa/ Kata au halmashauri
10.Mishahara ya wafanyakazi tena hapa wanataka kila kada uwe na watu angalau wa tatu wakati wao hospital zao unaweza kuta hata mtoa dawa hamna au zahanat haina daktari na safi tu.

Hapo bado hujanunua vifaa tiba na dawa.
Umenifurahisha hapo,Kwamba kila kitengo kinatakiwa kuwa na mtaalam husika, ila wao Wana upungufu. Ole wako private hospital ikose hata mtaalam mmoja, inakuwa balaa.

Ndiyo maana ni nadra sana Mfanyabishara kuamua kuwa na Hospitali.
 
Mimi ni moja ya watu ambao wame experience vitu vya kushangaza sana nilipokuwa mwanachama wa NHIF ( kupata huduma hafifu) na baadae nikawa mtoa huduma ( nikihudumia wateja wa NHIF) kila nikitumia wastani wa Milioni 1 kuhudumia wateja wao, jamaa wananilipa wastani wa laki 4 hivyo nakuwa nishapoteza laki 6 ambazo nilikuwa nazo mfukoni kabla ya kuhudumia wanachama wao.

Hiyo ni sawa na kusema kila nikitumia 10M kuhudumia wanachama wao, automatically ningekuwa na uhakika wa kupoteza 6M ( confirmed)

Inashangaza sana wa kweli.
 
Serikali imehujumu watoto wa nchi hii, imefuta BIMA toto. Mamilioni ya watoto wanapata tabu.

Rudisha Bima toto NHIF
 
Samahani sana kwa majibu nitakayotoa mbele....

Kama wewe ni msomi..
Nakuhakilishia kabisa Waliokusomesha wamepoteza pakubwa sana..

Sasa nisililize kwa makini sana..
Nakujibu vizuri sana..

Hoja ya kwanza umesema Uanzishwaji wa Hospitali Nyingi ulitegemea NHIF

Sijui umri wako..

Ila ngoja nikupe kidogo Historia mwaka 2001 Tanzania Rasmi ilianzisha sheria ya Bima ya Taifa na ikaanza implementation yake mwaka 2002..
Na ilikuwa Lazma kwa Watumishi wa Serikali mwaka 2003..

Malipo ya Bima kwa Private sector yalianza Rasmi mwaka 2004 bila kusua sua...

Sasa Takwimu za kipindi hicho Serkali ilikuwa chini sana kwa Kuwa na Vituo vyake vya afya na hospitali walikuwa wanamiliki chini ya 30% ya Vituo vyote na hospitali..

Na ndo maana Hospitali nyingi Za private na FBO zilipewa hadhi ya Hospitali za Mkoa na hospitali za wilaya Zikiitwa DDH na DRH..
(designated District hospital na Designated Regional Hospital)

Miaka Ya nyuma Kipindi bima hakuna ndo miaka Vituo vya serkali vilikuwa vichache sana..
sasa sjui wewe Takwimu zako unazipata wapi au ni umri wako ulikuwa mdogo pengine..
Vituo vingi vya afya na Hospitali vilijengwa kipindi.cha Kikwete na Magufuli..

Hoja ya pili umesema kuwa Hospitali inapata Mapato kupitia NHIF na wanatajirika kupitia hayo.

Katika Taasisi inayoongoza kwa kudaiwa na kukata Madeni ya watu nafikiri ni Moja ya Taasisi ambayo ingechukua Tuzo..
Chukua mfano hospitali hutuma madai ya 12 Mil ila inalipwa 3mil na kubaki inadai 9 Mil..

Visingizio vimekuwa Vingi sana kuhusu malipo sasa wameamua kabisa na bei wazishushe..

Ingekuwa inafaidika unafikiri wangegoma kuchukua pesa zao wasitishe matibabu ya wagonjwa?

Ni taahira peke yake anayeweza kudhania kila kitu kipo kisiasa

Hoja yangu:Kuhusu Kitita

Tudiscuss Bei za Dawa na Huduma Kwa Kitita cha mwaka 2016, January 2024 na hiki kipya cha March 2024..
Kipi kimefanya washushe gharama za bei wakati Soko la bidhaa bado liko juu?

Ulitaka tujikite hapo kama wasomi na sio kama waropokaji ..
Jibu refu na zuri, tatizo unamuelewesha akili yake tu haimtoshi unadhani atakuelewa?
 
Tegeta 😂

Labda Tegeta ya Dareda:

GHf87HBW0AANomp.jpeg
 
Hapo ilitakiwa mkurugenzi mkuu wa NHIF na waziri wa afya wajiuzulu mara moja kwa kuwachanganya watanznia na kumchosesha kura rais kwenye uchanguzi wa mwara 2025
 
Sawa ngoja tukajipange huko Mwananyamala, Temeke, Mabwepande na Palestina hospitals tukisubiri Huduma za X-ray, Usb, echo, ECG, holter monitor, trademill, MRI, ctscan, dialysis, physiotherapy n.k
 
Umenifurahisha hapo,Kwamba kila kitengo kinatakiwa kuwa na mtaalam husika, ila wao Wana upungufu. Ole wako private hospital ikose hata mtaalam mmoja, inakuwa balaa.

Ndiyo maana ni nadra sana Mfanyabishara kuamua kuwa na Hospitali.
Yaani mkuu tena wanakua wakali kishenzi ,imagine kizahanati wanataka uwe na CO watatu wakati wao mmoja tu

Biashara ya afya kwasasa ina mikono mingi ngumu sana utatoboa kwa kupambana mno.
 
Back
Top Bottom