Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
WIZARA YA AFYA
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA
TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZINAZOSAMBAA KUHUSU KUTOKUTUMIKA KWA KADI ZA WANACHAMA KATIKA VITUO BINAFSI
Januari 07, 2024 Dar Es Salaam,
- Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF), unakanusha taarifa za upotoshaji zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikielezea kuzuiwa kwa kadi za wanancham kupata huduma ama kupewa rufaa kwenye hospitali za binafsi zilizosajiliwa na Mfuko.
- Taarifa hizi hazina ukweli wowote na badala yake zina nia ovu ya kuleta taharuki kwa wanachama wa mfuko. Ukweli ni kwamba huduma za matibabu kwa wanachama wake zinaendelea kama kawaida kupitia vituozaidi ya 9,000 vilivyosajiliwa na Mfuko vikiwemo vya Binafsi, Madhehebu ya Dini na Serikalli.
- Kutokana na hayo, Mfuko unapenda kuwahakikishia wanachama wake kuwa huduma za matibabu zinaendelea kama kawaida katika vituo vyote vilivyosajiliwa na Mfuko na endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote taarifa rasmi itatolewa kupitia njia rasmi ikiwemo kurasa za Mfuko zilizoko kwenye mitandao ya kijamii.
- Endapo mwanachama atakutana na changamoto ya kukatliwa huduma katika kituo cha huduma atoe taarifa kupitia ofisi za Mfuko zilizo karibu au kupiga simu namba 119.
Imetolewa na;
Grace Michael
KAIMU MENEJA UHUSIANO
===Grace Michael
KAIMU MENEJA UHUSIANO
Pia soma:
Hebu tuambizane, hospitali binafsi zimeanza mgomo baridi Kwa wanaotumia Bima za NHIF?
Hospitali za private (binafsi) zatishia kutohudumia wagonjwa wanaotumia bima ya afya ya NHIF