BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Nimeangalia tena kuona kama hili swali lina chembe yoyote ya utata,
Kweli katika hayo mawili umeshindwa kupata kipi ni nambari one na kipi kinafuatia??
Mie ninavyoamini, familia ni nambari one, tena pia ni nambari mbili, tatu na hata nne!!
Kwa sababu mleta mada hajatuelza kama tuchague kuwa na kimoja peke yake, kwa hiyo unaweza kuwa na wingi wa kimoja na hilo jingine likawa kidogo. Hivyo, nikiwa na familia yangu iko stable, sitashindwa kutafuta kidogo kidogo cha kutuweka mjini!!
Kama ni kipato cha kunipa mafweza ya kumwaga (kama yale ya EPA) at the expense of my family..please hicho kipato niko tayari kukikosa!!
Babu DC!!
Nakubaliana nawe Mkuu DC. Kuna thamani kubwa sana ya kuwa pamoja na familia yako ambayo bahati mbaya hatuwezi kui-quantify thamani yake kwa kutumia currency yoyote ile duniani. Hivyo kama nilivyopiga kura chaguo la kwanza ni familia.