Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,255
1) Utendapo wema maana yake unamjali mwenzio.
Yaani maana yake umejilipa mwenyewe kabisa.
Kwani lolote tutendalo huwa tunajitenda wenyewe!
Liwe jema au la, Muumba huturudishia lile lile!
Lakini wema usiwe wa kutenganisha familia zao!
Unapoitenganisha, wewe ni mkatili na siyo mwema.
Wema wa WEMA uko wapi?
2) Kama wewe siyo mkatili basi sasa u nani wewe?
Ukimnusuru rafiki lupango na kumwacha mume!
Mume anaendelea kusota ndani hivi ukoje wewe?
Sasa hapo umeijenga familia au kuibomoa kabisa?
Si kheri wote wakaendelea kusota kule lupango tu?
Kama watoto nd'o kisingizio, lakini yakubalika kweli?
Wema wa WEMA uko wapi?
3) Kajala hamtembelei katu mzee kule korokoroni!
VISA pia imelonga haya kwa kirefu sana mmmmh!
Matanuzi yao yaendelea na huku mzee anasota!
Kipimo cha wema kiwe hakuna kubaguana katu katu.
Nguvu tuzikusanye na mzee tumwopoe kule gerezani.
Wana JF jitokezeni kumchangia Baba Kajala naye atoke.
Wema wa WEMA uko wapi?
N.B:- Inspired by VISA tabloid of may 16th -22nd, 2013 No. 108.....ISSN 0821-584.