Weka wazo lako la kuishauri serikali kuhusu kuboresha usafi wa mazingira

maramojatu

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
1,175
1,542
Habari ya jioni wanaJF,

Mimi kama mkazi wa DSM nimeona niweke hii thread hapa ili tuwe tunaishauri serikali jinsi ya kuboresha usafi wa mazingira tunayoishi. Ushauri serikali ifanye haya.

1. Kuongeza kodi maradufu kwenye nepi za watoto wanaoziita baby diapers... Hizi zimekuwa uchafu maeneo mengi. Kuna wakati mtu mmoja alijaza mfuko wa sulfate na kuniwekea kwenye eneo langu. Watu washauriwe kutumia nepi ambazo zilotimika miaka ya 1970.

2. Chupa za plastiki nyeusi zinazoweka vinywaji kama Azam kola sijui nini... Hizi waokota makopo hawaziokoti sijui haziwezi kuwa recycled au vipi. Kwa hiyo watumiaji na watengenezaji wa vinywaji hawa wanatakiwa waongezewe kodi au walazimishwe kuandaa utaratibu wa kuzikusanya na kuziteketeza kwa utaratibu unaofaa.

3. Serikali kurudisha utaratibu wa usafi wa mazingira siku ya jumamosi.

4. Mifuko laini la plastiki imerusi mitaani kwa utaratibu usiojulikana. Serikali ifuatilie hili na kuchukua hatua stahili.

Tafadhali ongezea maoni yako kwenye hili.

Usiku mwema
 
Kuna mji mmoja ulioko katikati ya nchi wamefunga madampo ya kutupia taka hadi yale yaliyojengwa masokoni na mitaani.

Badala yake wananchi wanajikusanyia taka zao na kuziweka kwenye viroba vya salfeti kisha kuvirundika kando ya barabara ili gari la kukusanya viroba hivyo lipite na kuvibeba kwenda kutupa huko nje ya mji walikopanga kutupia taka hizo.

Kero ni kwamba viroba hivi vinakuwa ni uchafu barabarani vinakaa muda mrefu kuchukuliwa. Bora yale madampo na vizimba rasmi vilivyofungwa kuliko kurundika uchafu barabarani.

Huo ubunifu ni wa kijinga sana, sijui huyo ofisa wa kusimamia usafi alisomea chuo gani hicho mpaka anashindwa kubuni namna nzuri ya kudhibiti na kukusanya taka mjini badala yake ndio anachafua mji zaidi
 
Back
Top Bottom