Stacy hata kaa asahau siku hio ya Harry kufanya ile show, imemcost vitu vingi sanaaa. Its like her life will never be the same again. Yaani hatokuja kusahau. Vile simu zinaingia mambo si mazuri, mambo si mazuri akawa anajipa moyo kuwa Mungu mwema tuuuu, mambo yatakaa vizuriii. Mwanzo huwaga mgumuuu. Akawa kidogo hii show ya Dar inampa moyo. Weeeee! Hio mvua ilio shuka huku Dar sasa, hata ilipotokea hakuna anaejuaaaaa. Ilishuka mvuaaaa, kubwaaaa ya uhakikaaaaa.
Wasanii waliolipwa wakaimba hivo hivo wakaimbia viti na majukwaa matupuuuu. Na hela za Harry ndo zikawa zimeishia hapo. Yaani kufika usiku ni simu tu za kudaiwaaa. Ikafika mda Stacy akamzimia simu, akamwambia kaa bwanaaa, utadaiwa hata kesho, deni halina haraka na mdaiwa hafungwi bwana.
Yakapita lakini, asubuhi jua likawaka, siku hazigandi wiki ikaishaaa. Harry analala tu ndani asubuhi mpaka jioni. Kuja kujua kumbe alikuwa na mkopo bank tena juuu. Mkopo mkubwa tuuu. Million 40. Yeye akajiweka pembeni bwana, ndo raha ya kuwa mchepukooo, kama ulivokuwa unakula makombo ya raha yanayobaki kwa shibe ya mke, na shida nazo unakula kidogooo, tofauti na mke ambae anasimamia show.
Baada ya wiki Harry akaondokaaa, akawa kujikosha anampigia simu mara kwa mara kumjulia hali tuuu, na kumuuliza mambo yanaendaje na kila siku anapewa habari bora hata ya janaaa. Hakutaka kujihusisha sanaaa, yeye sio mke bwanaaa. Angekufa ghafla Harry, mali zote si angepata mkewe na mtoto sasa jimsalaba hilo ahangaike nalo vipi sasa. Cha maana alitaka tu kumfanyia ubinadamu wa kawaida.
Wakawa marafiki na Gill, na urafiki wenyewe Gill alikuwa kapatikanika na Malikaa si kidogooo. Malika anavodai hana imani na Gill na Stacy, lazima wanakulana kisiri siri kama hawakulani kwanini sio marafiki? Ukiona watu wameachana wana uhasama basi ujue wanapendana. Ili Malika ajiridhiseh Gill is over Stacy basi wawe marafiki wao wa 3, Stacy, Malika na Gill.
Stacy kwanza aliona huo upumbavu mtupuuu, kama Malika is insecure, sio tatizo lake hilooo. Watajuana wenyeweee. Sema Gill akamuomba sanaaa, Stacy usinifanyie hivooo, Malika ndo kiboko yanguuuu. Meet her walau umjue, usipompenda baas. But atleast kabla hujakataa get to know her. Stacy akawa haoni logic, sema ikaja issue ya kwamba Gill ananunua pombeeee, na analula bata refuuuu sanaaa. Kufikiria kama Malika karidhia aliwe yeye Malika, bata wala wote sio kesi, not a bad idea.
Siku ya kukutana na Malika akakubali the girl is something else. Yaaaaaaaaniiii! Acha kabisaaaa. She has no limit. Kiukweli sio rahisi kutokumpendaaa. She such a lovely and babbly person, alafu too generous. Japo she is so wild! Too wild to be exact. Anakumbuka siku hio ya kwanza wanaonana akamuona kavaa LV genuine originaal ya kiatu. Akamsifia tu, LV hii ni kiboko. Akamwambia unavaa size gani? Akasema 39. Malika akasema we wear the same size. Basi akajua yameishaaa. Mda Stacy anaondoka akamvulia vile viatu kampaaaa. Just like that. Stacy akajisemea Malika we gonna be friends for life. Hana shidaaa kabisaaa, ukiongea kitu tu yeye anakusapotiii, yaani kiukweli hajawahi hata kumkrea bahati mbaya. Kazini akija kwa Gill wakiagiza chakula anamuagiziaaa. Basi Gill anamtania sasa hivi nataka kuoa wake wawili. Hahaaaaaaa.
Harry alivoondoka ukapita kama mwezi mzima, wanasalimiana tu, ila kuonana ndo hawaonani, anahangaikia mambo yake. Ila usiku wanaongea sanaaa, kilichomfanya ajue hayupo kwa mkewe. Akawa anampa moyo tu, na nini na kumtia nguvu. Sasa siku hio usiku akamuomba sina pa kukaa naomba nije nijibanze kwako kwa mda. Akawa kamkubali, si kujibanza, akajua yale mambo ya mtoto yanaweza kuendelea.
Akawa kachelewa kutoka kazini, maana alitoka na Gill na Malika. Alikuwa kasha sahau kama Harry anakuja. Saa 2 akastukaa, akasema akimbie mkuku mkukuu. Kafika saa 3. Akawa kakaa sebuleni. Akawa anaongea na dad, wageni wamekuja, dada akamjibu wamekujaa ndio. Akasema sawa. Nipakulie nionje, tumngoje mgeni kuja kula.
Akiwa anakula akaona mtu anafungua mlango wa chumbani, akajua Harry,akashangaa kumbe alikuwepo ndani mda wote. Akashangaa mwanamke ndo anatokaaa! Tobaaaaaaa! Akastuka chakula kikampaliaaa. Akawa bado kaduwaaa, ndo mwenyewe mke wa Harry. Akapigwa butwaaaa. Inamaana huyu Harry kuomba kukaa ndo kaja na mkewe na mtoto? Tumeeeeeee! Akawa kwanza kachukiaaa, kaona sasa huko kufanyana mafalaaa. Ndo nini kuhamia kwake na mke na mtoto. Huo ni upuuzi na kufanyana maboyaaaaaa.
Akawa kakerekaaa, akataka kumtimua yule dada, ila akawa kaja sebuleni na mtoto. Akasema ngoja nimuweke kiporo nimngoje huyo mume wao sasa ndo atamsulubisha vizuriii. Akawa kaja kukaa kwenye kochi, akamuamkia shikamooo. Akaitikia tu marahaba. Karibuniiiiiii. Karibu sanaa, mjisikie mko nyumbani. Muwe na amani tu. Kwa unafikiiii Stacy hana mpinzani.
Akamuuliza "Mmekula? Mtoto kashaoga? " Akaitikia tu "Ndio tunashukuru" Wakawa wamkeaa kimyaa wanaangalia Tv. Stacy analilia vitu vya Prince, inabidi sasa Sahngazi mtu amwambie Prince muachie vingine. Akawa kakaaa anamngoja kwa hamu sanaa huyo Harry. Akamuuliza unaitwa nani? Binti akase,a Imelda! Una miaka mingapi? Akasema 17. Mmmmmmh akaguna tu. Akamuuliza "Unafanya kazi?" Akasema hapana na reseat mtihani. Stacy akawa mbona mdogooo, ila akakumbuka mwenyewe by 15 ashaanza kuikalia mipini na kuikatikia kabisaaa.
Akawa kasha chefukwa, akamwambia "Naenda kulala karibu sanaa jisikie uko nyumbani". Akiwa chumbani Prince akangangania kulala kule, maana kila Ijumaa wanalala nae tangu Harry aondoke, na kile cha Kike kikawa kimekujaa. Akajisemea "Sasa huu mtihani jamani." Akamuita dada kanunue pampers. Akawa kaileta. Akakavalisha akalala nao wote. Moyoni anawaza majaribuu kweli kweli.
Mpaka asubuhi Harry hajaja. Akaamka akampikia Prince brakfast akapika na uji. Akakinywesha kile kitoto. Kiukweli yeye anapenda matoto mabongeeee. Vitoto vilivokondeana havitakagi kabisaa. Prince nae hana tu shukrani anamlisha hatari sema tu hanenepi. Ila ukimuona anangaa unajua hili toto linalishwa vizuriii. Mda wa Prince kulishwa dogo analilia basi nae analishwa. Kiko so happy. Watoto wako so inocent. Akajisemea hujui baba yako kafilisika hana hata 100. Utajuuta mwaka huu.
Akatoka kwenda kuzururaa. Akarudi jioni wakala, ashaanza kuwazoea sema ndo vile hataki kumzoea yule mwanamke. Kabisaaaaa. Ila mtoto aaaaah! Mashostiiii. Yule dada bila kuambiwa akawa kama house girl anashinda na dada jikoniii. Anasaidia vyombo, na vitu kama hivo bila kuambiwaa. Chezeaa mume ndo kafulia utasugua sufuria sanaaa.
Jumapili wamekaa akawatoa out, wote nyumba nzimaa. Mke wa Harry hana raha kabisaa, yani hana rahaaaaa. Yupo yupo. Mtoto ndo kampani ya Prince hana habariii. Wa,erudi jioni, yule mama mtu akaanza kumsuka mtoto. Stacy akamuuliza "unajua kusuka? Akjibu "Najitahidi" sema sio ya kujiamini kabisaa. Akawa anaangalia nywele moja kamboronga borongaaa, mistari imepindaa, akasema kasheshe. Akamwambia "Acha dada awapeleke saloon na Prince anaenda kunyoa kiduku chake kimeota." Yule dada akawa anasita sita, akamwambia "Acha tu nimsukeee." Stacy akamwambia mbona kusuka hujui sasa hata mi nakishindaa, watamcheka mwenzie atakuwa shabby!" Dada akakaa kimyaa baadae akajisemea "Hela hatunaaa dada" Stacy akamuhurumiaa sanaa, chezea mume kufilisikaaa. "Akamwambia nitamlipia" wakaongozana na dada, akawa kampa dada 50,000. Yule dogo asukwe nywele za 35000, Prince kunyoa 10000 na inayobaki wakililia vitu huko maana Prince kwa kulilia vitu kibokoooo
Baadae wanarudi dada kabakia nyuma nyuma Stacy akajua ana umbea, akamwambia dada njoo, nje ya geti. Dada anamwambia huyu mgeni anasikitishaaa. Stacy akamuuliza kwanini? Hana hata 100. Dada nae kwa umbeaaa. Stacy akamuuliza umejuaje? Kaniomba nimkopeshe 1000 anunue panadol anaumwa kichwa. Stacy akamuuliza wachaaa? Dada tumefika kule anataka mtoto asukwe nywele za 5000 eti hela hamna, nikamgomea nikamwambia umesema asuke za shangaaa. Akasema huyu dada ana roho nzuri Mungu amlipie tu, asije tu kutuchokaa. Afu anagombana na baba mtoto wake kwenye simu. Stacy akatega sikio. Wanagombana nini? Anamdai hela ya matumizi kwamba yeye hawana hela sahivi. Stacy akamuliza na baba wa mtoto anasemaje? Anasema mambo yake sio mazuri. Stacy akamwambia dada uendelee kunipa ubuyu.
Wakarudi ndani yule mama akasema asante dada. Stacy anamjibu usijaliii usijaliii. Katoto kakawa kamependezaaaa. Kesho mda wa shule wakaandaliwa wote wakapelekwa na Prince. Kazini anawaza hivi huyu Harris ana maana gani kunitupia mkewe na mtoto, ananiona falaaa, nitamcharuraaaa. Nitamvurugaaaaaaa.
Akawaza siku hio usiku ndo atamnyea aje achukue viumbe vyake, hataki stress mjini. Akarudi nyumbani mapemaa, wakawa wamekaa kwenye Tv. Wanaangalia hawana tabu na mtu. Wakiwa wamekaa hawana hili wala lile kina Prince na Stacy wana gombana maana ikawa kawaida wote wakorofiii, kamfokea Prince mpaka kachokaaa. Harris akaja. Stacy akasema safiii sanaaa. Finally!
Akawasalimia za hapaaa, akaitikia safiii, dada akaamkia, na mama mtoto akasalimia ila salamu yake ilimshangaza sana Stacy. Akasalimia "Shikamoo Mjomba!" Stacy akashtuka ila akachunaa, akawaza wanataka kuniletea ujanja wa kizamaniii, baada ya maisha kuwala Tigo sio mke na mume ni mtu na mjombaaa wake. Nyokooooo! Hio ilikuwa zamani, hawamfanyi mjinga ngooo. Bado sanaaaa. Katoto nacho kakamkimbiliaaaaa na kumuwaoh, nako kanaita Uncle! Akawaza hivi huyu mtoto mdogo hivi unaweza kumshikisha maneno kweli? Mmmmh! Ila hataaa sikubali kirahisiiii.
Harry akapakuliwa chakulaa akala, Stacy akaaga naenda kulala, na jeshi lake likamfata nyumaaa. Watoto wanalala vibayaaaa. Jana yenyewe ilibidi alale kati kati yao. Maana si kwa kujitandaza kule na kujibinnuaaa. Kazima taa, wamelala. Anamsikia Harry anakuja, akanyamaza kimyaaaa. Akaingia kavua nguo kabaki na bukta, anauliza mi nalala wapi sasa? Stacy akamjibu tu "Nafasi hakunaaa huku kalale na mkeo." Harry akacheka alilitarajia hilo kabisaaa. Akaanza kujikosha "Nisamehe bwana Stacy huyu mpwa wangu, we umemsahau huyu siku ile nyumbani alikuwepo, mi niliongea vile kukujambishaa tu ila sio mke wangu, hii mimba alipewa shule huko akatelekezwa sasa mjomba kamtimua ndo nakaa nae. Please dont make a fuss about it. Nakubali nilikukosea kukudanganya"
Stacy akamwambia "Harry usijishushe hivooo, kufilisika ndo umkatae mkeo? Mi sio mtu mbaya we kalale na mkeo, mi sina neno." Harry kajielezea paragraph 25. Stacy kakaza. Anambania vifungu hatari. "Kama sio mkewe mbona Gill alivomwambia siku ile usiku alishindwa kukanusha hana mke? Yule ni mkewe analeta janja ya nyani tu. Mke anaumaaaaa, kumkana mke inataka ujasiriiii. Na yeye mara kibao kashindwa kumkana mkewe." Harry anajitetea kwamba it was a Haux sio kweli awaulize watu sijui nini. Akaambiwa huku hulali bwanaaaaa. "Kalale na mkeo." Anajitetea yule mpwa wangu nitalala nae vipi? Akaambiwa ndo utajua sasa. Huku unatupigia kelele.
Harry akalala kwenye kochi mpaka asubuhi. Nyumba ina vyumba vi tatu, kimoja yuko dada na ndo cha prince, kingine yuko Imelda, na master yuko Tracy. Akalala kwenye kochi. Asubuhi mpwa wake asimuone analala kwenye kochi akaenda tena kumbembeleza Stacy, stacy akagomaaaa. Hizo janja zipo sanaa, mtu anamleta mwanamke wake afu anadanganya danganya wanakulana humo humo. Sasa yeye harry kachelewa anamjua huyo nduhu yake kama mwanamke wake kitambo. Akawa amekaa sebuleni.
Akawaandaa kina Prince wakafatwa na Schoolbus, Harry yuko busy anaangalia News, CNN, chezea kutimuliwaaaa chumbaaa. Hahaahaaa. Wakati anaondoka, Harry yuko sebuleni akamuuliza Imelda utaenda shule, akasema ndio. Akamuuliza una nauli? Akawa anamuangalia mumewe sijui mjomba wake, watajua wenyewe kwa wasiwasi, akajibu tu ndio, ila hamuangalii usoni, ile ya mashaka. Akajua hanaa. Akampa 50,000 akamwambia utaongezea nauli yako.
Kufika kazini dada Prince akamtumia sms, huwezi amani ile 50,000 uliompa mjomba wake kamuomba ampe 20,000 hana nauli ya mihangaiko yake. Stacy akawaza Tobaaaaaaaaaa!
ITAENDELEA SAA 6 USIKU.