Gill akawa anakaa anamtafakari malikaaa hammaliziii. Yaani haelewi elewi. He never though time would come when he will be a One Woman Man. Hakuwahiiii kuwazaaa. He has always been a womanizer. There was Stacy and always other women. Lot of other women. Hapendagi kujibanaaa, akimpenda mwanamke hata akimtamani tu lazima amle. He belives women were created for men. Women are a gift from God for men to enjoy themselves.
Ila tangu awe na Malika it is almost 2 month na haja mcheat hata siku moja. Yaani hajiskii kabisaaa kama ana hamu na wanawake wengine. It is as if ameacha kuwanotice wanawake. Hata akiwa na washkaji wenzie , atapita demu wooote watamsifia yule demu bombaaa, ila yeye atamuona kawaidaa. Akaanza kuhisi sio buree, huenda Malika anamfanyia mambo ya kiswahili. Yale mambo ya suicide mission, ya kuwekwa kwenye chupa ndo Malika anamfanyiaaa. Akatetemeka kwa wogaaa. Not that he is a church person ila Malika kazidiii, atleast yeye mara moja moja anaenda kubeep kanisani. Anakuta nyimbo zimebadilika, viitikio vimebadilika ila atleast. Malika hata hajui ni dini gani.
Akawa comvised Malika anamfanyia ushirikina na ndumba, anampulizia to keep him faithful. Akajiambia kama yeye mshirikina sanaa na anajua waganga basi aniongezee dose. Ujue hivi vitu vipooo, sema tu sijajaribu ukute ashaniroga jogoo langu haliganyi kazi nikiwa na mwanamke mwingine. Tumeeeeee. Aka shiver kwa woga. Mmmmmh! Hatari sanaa. Ngoja nijaribu na mwanamke mwingine ukute natembea mjini kibabe kumbe huku chini machine kushneyyyy, kwisha habari yangu.
Woga ukamzidi akajiambia hataa sijaribu na mtu nae mjua, maana kama ndo halifanyi kazi kweli si ndo atanitangazaaa, Gill siku hizi hamna kituuuuu, limesinyaa tu. Hana jipyaaa. Mmmmh! Hatari sanaaa. Akakata shauri bora amtafute mtu mtandaoni wasiejuana hata akishindwa kufanya kazi itakuwa siri yake. Akajiambia kama kanilogaa, yaani nitamuendea pembaaa kumuotesha kibushaaaa.
Akaingia Badoo, akatengeneza profile feki akatulia kwanza na kuanza kukagua kagua. Akamuona Lizzy da ass profile zinga la msambwandaaa. Akaanza kumchatishaa, mchina huo unao kweliii, isije kuwa chengaaa? Akajibu ninaoooo na najua kutumiaaa. Gill akasema mmmh hapa hapa. Akamsomeshaaa, akamwambia njoo Serenana, akampa chumba namba. Akabook chumba chake cha siku zote kama kawaidaa. Lizzy kaja, amevaa nguo wa ukweliii, msambwandaa anao wa kutoshaaa. Akaona mashine inasimama akajua inafanya kazi vizuriii. Akaamua sababu maji kashayavulia maji hana budi kuyaogaa.
Lizzy kuvua nguo, mistariiiii, michiriziiiii mwili mzimaaa. Kama ramani ya duniaa. Yaani utasema ugonjwa wa ngoziii. Gill akawaza hawa watoto wa broiler hawa, pale hajazaa michirizi namna ile, akizaa sasa si ndo balaaa kubwa. Hamu yote ikamuishaaa. Akamwambia vaa nguo zako uende. Basi anajishtukia akwanini jamaniii, mbona hivooo, basi nazima taaaa. Akampa 200,000 ya nauli. Lizzy da ass kupewa ile hela anangangania apewe namba ya Gill ili amtafute. Gill akampa namba kanyaboya.
Akampigia Malikaa aje, hela yake ya hotel isipotee bureee. Akhaaaaaaa! Malika kaja asijue kilichotokea, anamsifia babe you are so spontaneous. Wakawa wanaongeaa kwanza. Mapenzi ya kiutu uzima mnaongeaa kwanza weee, mnajadili mpaka taarifa ya habariii ndo muanze mapenzi. Malika kupiga jicho chini akaona enjoface tena hizi za bei poa za 3000 imeanguka. Akajua Gill alikuwa na mwanamke mule mda si mda. Akaipotezea na kurudi kwenye story.
Gill akaenda kuoga, Malika akaiokota ile enjoface akaitumbukiza kwenye dustbin. Akauchubuaaa, akawa busy na mambo yake. Gill kutoka bafuni ikatokea tu akapiga jicho kwenye dustbinakaiona ile enjoface wakati kabla hajainhia bafuni aliliona liko tupu. Akajua tu Lizz da Ass ndo aliidondosha na Malika ndo kaitupia mule. Akawaza tu Damn! Ila nae akauchubua kama haijaionaaa.
Wakawa wamekaa Balconny wanaongea tu. Tofauti na wanwake wengine woote hata Marrie, Gill alipenda kuongea sana na Malika, they could talk for hours haborekiii. Yani hawa,alizagi kuongeaaa. Wakiwa Balconny wanaongea na kunywa kupitisha mda, chumba kikagongwa. Malika akaenda kufungua, akarudi ndani, afu akarudi mlangoni tena akafungaaa. Gill akamuuliza nani tena? Akasema room service wamechanganya vyumba kuna mtu ameorder ametoa wrong room no. Wakaendelea kuongea.
Walivokuja kulala Gill akapiga jicho kwenye dustbin akakuta ile enjoface haipo tenaaa. Akajua tu Lizzy da ass ndo aligonga alifata enjoface yake. Moyoni akasunyaa Mxiuuuuuuuuuu, 200000 yote niliompa kashindwa kununua decent make up kairudia enjo face ya 3000. Loooh! Hawa kuku wa kienyeji tabu sanaaa. Akaendelea kujikaushaa kama hajastukia pichaaa.
Akajikuta anakumbuka walivokutana na Malika, akaghairi kutoka nae, akawa ameblock kwenye simu. Siku hio hana hili wala lile Malika akamfata ofisini. Akastukaaa, Malika akamwambia ana mualiko Ikulu sasa hana date na angependa kwenda nae kuna hafla na raisi atakuwepo. Gill couldnt resist ndo akamu unblock na kwenda hio hafla. Kwanza sababu hakuwa na political connections, so akaona sio mbaya kuanza kuzIkusanya sahivi.
Kwenye hafla hakuboreka hata kidogooo. Akaamua sababu analipa lipa ata hang out nae siku 2 tatu afu atamtelekezea huko yeye hatafuti mke. Siku mbili hizo alimfacinate sanaa. Gill anapenda sifa, sanaaaa. Akaanza kujisifia anahela ya kumuhudumia vizuri sanaa, Malika akamuuliza niambie una hela gani? Basi Gill kujisifia i am MD, Malika anamtupia shade so you still working for other people at that age, eeeh tuendelee. Gill anajisigia nina mansion Mikocheni, Malika anamjibu which your wife gets to keep it to raise the children. Gill anajisifia nina viwanja na mashamba, Malika anamwambia of which ni dormant asset, manake hazikuingizii income on daily basis, i could say you have millions burried somewhere. Gill pozi likamuishaa akaamua kusitisha kuhakiki mali zake maana alikuwa anajiaibisha kwa Malika.
Akamuuliza Malika sawa you put me down, but what do you have? Malika akamuonesha 2 appartments in Dubai, Resort in Mauritius, Lots of Stocks and Bonds. Very big liquidity in forex. Gill akamshangaa, impeccable for a woman. Akamuuliza so UN pays you all this money? Malika akamwambia mi UN navolunteer tu, sijaajiriwa nimejiajiri. Gill akasema too good to be true atakuwa wale wanwake tapeli au wapigajiiii. Akaamua tu kumchimba ili amkamate. Akamuuliza umejiajiri kwenye nini? Drugs au?
Malika akamwambia mi nadela na Foreign exchange, nafanya speculation naingia masoko yangu makubwa ya Shangai Stock exchange, Japan Exchange Group, Hokong Stock Exchange, schweni stock exchange. Nanunua $$$$ zina flactuate sanaa, nazi cross exchange na Yen na chinese Yuan. Afu nakuja kuziuza hapa bongo kwa wachina na wakinga, wachaga below market value. Rate hawapati kokote.
Nauza na hela zingine za Africa natread sana Nairobi Stock Exchange, Jobag stock exchange, na Nigeria stock exchange. Nauza sanaa Nairaa kwa wanunua mafutaa, na Rand kwa wanunua viatu South, na magari, na KSh kwa wauzaji wa vipodozi, vyakula na vitu kama hivo. Kwenye financial black market mimi ni Queen, hela zinawekewa oda, hata kabla sijatamka rate. Competitors wangu ni wasomali tu, nao wanabahatishaaa na kutakatisha hela haramuuu.
Pia nainvest sana kwenye financial instruments kama Shares na Bonds. Nilitajirika na hisa za Tbl, Umoja na Twiga. Nanunua mpaka hisa international. My filed is money. Ukiona nimeshika pc hata saa nane usiku jua kwamba kuna soko la fedha limefunguliwaaa na biashara ishaanza. Mjini ujanjaaa tu.
Gill akamwambia kwa hio wewe ni miahini, na ukibambwa na BOT utashtakiwa for treason manake unahujumu uchumi. Malikaaa akachekaa akamwambia hawa mawaziri na wabunge wateja wangu wakubwaaa. Ndo maana Ikulu mi naingia sanaaaa. Mjini mipangooo. Gill akawa hajamuamini ila akaona she is something else. Basi anavokaa nae anamuona anavoingia kwenye masoko hayo, anahangaika kutafuta rate nzuriii, unakuta ana oda kubwa afu rate zimekaa vibaya vibaya ana dataaa.
Akarudisha mawazo hapo hotelini na kuwaza ile enjoface aombe msamaha au apotezee. Akawaza demu mwenyewe sijamlaa, hata Mungu atanitetea. Wakalala wote hapo hotelini kama kawaida the packahe is always complete. Ashaacha kijaribu kwa Malika, labda useme sijui amfundishe kitu au amuelekeze thubutuuuuuu. Yuko mila 30 mbele yake kwenye kila kitu kitandaniiii. Ikafika mahala he decided to sit back and enjoy her. Akawa hajitutumui tena, walaaaaaa. Alidhani Marrie ndo kiboko yake ila Malikaa ndo mamba yake. Mmmmmmmh!
Basi akanza kuchukua finanvial advice kwa Malika, ile kuambiwa hana kitu mzee wakati watu wazima walikuwa wanamtetemekeaa wanamuona Mungu mtu ilimzindua sanaaa. Na kilichomkera kuhusu Malika kwenye insvestment she is a natural, hatumii hata nguvu. Kuna siki akasema ana bomu la 50m linatiki, Malika akamuuliza kwa hio ukizipata hizo unaweka bank unatumia mpaka ziishe? Gill akawa mbogo kupangiwa hela zake cha kufanya hapendiiii. Huko sasa kuingilia uhuru wake. Kafokaaa.
Malika akamwambia what is nikikwambia kuna njia ya kuizungusha hio 50m ikazaa 30m in 2 months? Gill akajikausha maana katoka kugoka mda si mda. Badae akajikusanya na kuuliza njia gani? Nyokoooooo! Akaambiwa ameona kwenye internent alivokuwa India stock Exchange kaona kihabari kuna upungufu wa dengu na mbaazi India. Kilo imefika $5per Kg. Wakati huku bongo dengu na mbaazi zipo kibaooo, max ni $1. So by now kama wakipeleka mbaazi na dengu India kwa Cargo plane Ukauza hata $3 tu per kg mbona unatoka sanaaa, unarudisha hela, unatoa garama na faida unapata kubwa. Wanunuzi anaweza kuwapata kabisaa humu humu online wakabook kabla ya kupeleka.
Gill akacheka sanaa, yaani Mill 50 zilivo za shidaa unaniambia niweke kwenye mbaazi na dengu, i love you baby so much but hell no. Gill ofisini akamwambia owner wa hio kampuni kuwa kuna window hio katika story tu. Owner akamwambia nikutanishe na Malika i wanna throw in 500m deep and fast. Gill akaingiwa shaka Malika akiwatapeli je itakuwajeeee. Akaenda kumuuliza Malika usije kumtapeli boss wangu, utanimalizaa. Malika akamwambia nikitaka kutapeli nitatapeli wenye hela not broke men as you. Wewe you should not focus on thinking atapoteza million 500, fikiria atazalisha 300m in matter of days bila jasho.
Boss wake akakomaa anaweka 500m, Gill nae kimashaka mashaka akaweka 50m, wakanunua mbaazi na dengue, wakatafuta transporter, fata guidelines za ku export chakula, Gill alikomda kilo 5 hahaaa, kwa woga. Zimefika kule zimegombewa mbayaaaaaaa. Wakauza zoote. Wahindi wakatoa maoda makubwa makubwaaa. Boss wa Gill alidata maana alipata 900m kwa biashara ya siku kadhaaa. Gill alipata million 90. Kurudi Bongo msimu umeishaaaaaa. Hamna dengu wala mbaazi hata moja. Ayaaaaaaa! Washachelewaaa.
Basi Boss wake anamwambia muulize Malikaa what should we do next, tuuze nini na wapi? Hata akisema chachandu zina soko Japan im putting 1b bila doubt. Gill ana mpressure Malikaaa vipiiiii, vipiii Malika anamwambia ukitaka kupiga hela vizia opportunity. Sasa sio kila siku kuna fursa, siku kama hizi unatulia kwanza. Boss nae anaona anakawizwaaa kwenye kutajirikaaaa. From that day Gill anapokea finacial advice kwa Malika vibaya mnooo. Na hela sahivi anaizungusha inazaaa.
Akaamua it is about time amkutanishe na familia yake. Akamwambia Marrie, Marrie akasema poa nitaanda dinner na Mathie atakuwepo. Gill akasema sawa. Basi akasema sawa, wakaenda wote na Malika, akamkuta Mathew na wanae wawili wote wa kike. Wadogo kwa wanae. Yeye, Malika, Marrie na wale wanae. Basi mda wa kula, Gill akimpiga jicho Rodgers anampa doleee kwamba safi sanaa Malika yuko viwangoooo. Mmmmh! Moyoni anajisemea wewe jishaue tu kama sijakupa laana. Basi dinner ilikuwa tu civilised. Wakala wakaondokaaa.
Kabla ya kuondoka akamuita Rodgers chembaa, akamuuliza what is the progress on our research, have you dug any ghosts in his past? Rodgers akasema no, i inquired from his daughters but they adore him, i asked his students he is clean dad. He is a lecturer, and a noble man. Akamwambia we shouldnt be too sure yet, your moms heart is at stake here. Keep digging, and never relax son, you never know, ill keep dighing too. No stone should be left untouched son, keep digging, ask the dughters more about their mom, where is she? Anything unusual, i noticed he doesnt speak of his wife at all. We need to know what is he hiding.
ITAENDELEA KESHO SAA TATU ASUBUHI