Stacy was confused, akazidi kuamini kweli Mungu hampendiiii. Just as soon as Gill k propose kumuoa ndo mimba yake ikatoka. Jamaniiiiiiii.Kweli hiidunia haina wema kwake. Kwa jinsi anavomjua Gill akajua tu kwamba harusi na ahadi zte zilikuwa because of the baby. Akawaza hatomuachia kirahisi.
Watu wengi ofisini wkaja kumuona, watu amabao hata hawasalimiagi, team yake wanaompelekesha kama mbwa wakawa wanakuja kumuona na kumjulia hali kwa siku hata mara 3, aka realise they are good people after all. Pamoja na yote aliowafanyia they still cared for her, cared about her loss. Aka realize she really had no friends. Akajiambia tu akipona she will work on being a better person.
Wau wengi sanaa wakaja kumuona kasoro Harris. Gill kama kawada hakumuangusha akawa anampa full attention. Akaendelea kupata nafuu na kutoka kabisaaa hospital. Mda wote hawakua wamejadili swala la harusi au yeye kumuaha mkewe mefikia wapi au kama kuna maendeleo yoyote. Akaruhusiwa kurudi nyumbani. Akarudi nyumbni kwake, akaanza kuwa mkarimu kwa mdada wake wa kazi, mpaka dada akashangaaa ndo yule yule au? Akawaza tu labda kwasababu kakichungulia kifo ndo ameamua kubadilika, kulichungulia kaburi si mchezooo.
Akaja huyo dada wa Unga limited kumleta mtoto, anaitwa Ellina, na mtoto anaitwa Babuu au Justin. Hajabatizwa wala nini yuko yuko tu, ngozi yake inaonesha ana unyafuzi kwamba halishwi vizuriii. Siku analetwa na Gill alikuwepo wakawa wamekaa kwenye makochi ya Stacy ya million 5. Kumbe mtoto hajavalishwa pampers, si akakojoa. Stacy akapanic na kuanza kufoka makochi yake. Gill akamfokea Stacy kwamba it is just a coach sio kwamba mtu kafa litafuliwa na kurudi kama zamani, the boy is just a kid hajui kama yale makochi million 5 au 10, alichojua ni kwamba mkojo umembana anachotakiwa ni akojoe. Kama ataishi na mtoto inabidi a adjust mind set yake kwamba yule mtoto.
Ellia akasema kama mdada mwenyewe ndo huyu simpi mtoto wangu, narudisha hela, atamtesa sanaaa. Mtoto anauma sanaaa. Hana roho ya uvimilivu na uelewa wa kuishi na mtoto. Basi sababu mtoto si wake ndo atamtesa mpaka basi. Kwa kwelihajashawishika kumuchia mtoto. Stacy akaanza kupanictena na kujua keshaharibu. Gill akaingilia kati kumuelewesha Ellina sawa Stacy ana mapungufu yake, lakiniukimzoea ni mtu mzuri sanaa. Na isitoshe tatizo lake limezidi, Arostooo inamelekesha vibaya sanaa, mda mwingi anakuwa anabembea kwa hio bora amuachie mtoto mapema. Akiwa arostoo mtoto anaweza kukutwa na majanga mengi na hatokuwa na uwezo wa kumsaidia. Ellina akaanza kusema naenda Rehab, nitjipanga upya, niaacha kabisa na kuanza safari zangu kama zamani, nitamlea tu huyu mtoto. Gill akamuuliza toka useme hivo mda gani umepita? Ellina akatikisa tu kichwa kukubali Arostoo haiwezi inampelekesha.
Stacy akamuone huruma akamuomba msamaha, kwa kumfokea mtoto na kumsimulia mwenyewe mimba yake imetoka juzi juzi tu akajikuta analia akikumuka na yeye mwanae anekua kufikia pale. Yaani balaaaa. Ellina akamuonea huruma waka bond, si mnajua wote mkiwa na matatizo mnaelewana automatically.
Katia story za hapa na pale, Stacy akamuuliza Ellina iliuwaje alizaa na Traves au sababu ya overdose maybe wakajikuta wamehook up one night stand thing na yeye akamuua kuzaa au ilikuaje kuwaje hasa, Stacy alijua tu it will be nothing extravagant katika hio story ya 2 addicts, a prostitute and a gay. It had to be interesting. Ellina akamwambia walaa, me nimekutana nae sijaanza kutumia.
Mi nilikuwa nasoma, sasa sekondai hzi tukitoka shule kuna shoga angu ana bwana wake alikuwa na hela hatari, tukawa tunakutana nae bar, sasa nikimsindikiza kwa yule bwana namkuta yuko na Traves amabe akasema wanafanya wote biashara baadae ndo nikajua biashara ya Unga. Wale wako wa 2 na sisi tukawa waiwili. Nikawa naogopa nikajua labda ataniomba kiboga au sijui nini, ila hela nataka shoga angu keshanirusha rohooo, nikakaza nafsi. Basi tukiiga chumbani mwenzangu anajichoma tu sindano za unga anabembeaa mpaka analalaaa. Na mmi nalala nikiamka ananipa laki naondoka. Sijatoa mzigo wala nini. Tunaenda botics nunua manguo, manywele hela zote lazima ziishe. Akili zetu tumia hela ikuzoeee.
Ile kushinda shinda nae nikaanza tu kumpenda nikata nijue kwanini yupo vile, nikaguswa na kutaka kumfahamu. Siku hio nimeenda nikamkuta na dada mwingine, roho ikaniuma hatariiii, nilifanya fujo la kufa mtu. Akajua baada ya fujo yule dada akiondoka ndo basi, we thubutuuuuu, nikamwambia twende chumbaniii. Aawa anacheka tuuu. Basi nikaanza kumwamba mi nakupenda ujue. Akawa aajibu unanipenda cause hunijui ukinijua huwezi kunipendaaa.
Akaanza kunisimulia maisha yake alivofungwa gereza la Tanga wa wizi wa magari, alivofungwa tena Pakistan. Kwamba yeye ni gay. He always liked men tangu mdogo. Na hakubakwa wala nini mwenyewe tu he had feelings for men tangia anakua. Sasa na kukaa jela ndo akajiendekeza kabisaa. Ila being gay imemkosanisha na wewe dada yake, na kumfanya aishi kwa upweke sanaaa. After verything katika maisha yake alichokitaka ni kupatana na wewe tu ndo angejisikia mkamilifu, muishi kama familia upyaaa. Being alone has been so hard, watu wanakupenda ili wakutumie kufanikisha malengo yao ila wakisha fanikisha wanakusahau wanakwend akushangilia na ndugu zao. Akasema unga pamoja na kuusfirisha mda hkuwahi kutumia, na wala yeye hakuathirika na pangusa, kwamba anaharsha njiani mpaka apanguse ndo safari ifike walaaa.
Alianza kutumia intentional tu, kupunguza mawazo na stress na ili aache ushoga, manake alijua bila kuacha ushoga kurudisha undugu ni ngumu sanaa. Sasa alijaribu kuacha mwenyewe akawa anashindwa, ndo akaamua atumie unga kama kujisahaulisha flani, akianza kuwaza tu hayo mambo anajipiga dose. And it was working hajalala na mwanaume like in 2 yrs tangu awe addict. Mi sijuinilikuwa na akili gani, nikamwambia nitamsaidia kuacha ushoga na kuwa straight again.
Sisis wahaya na dawa zipo kabisaa za kihaya, na watu kibao walianza hio michezo wamepewa dawa na wamepona kabisaa. Wanasema hauponi hauponi ila mi nilikua najua unapona kabisaaa. Watu mpaka wanaoa na kuzaa. Nikaongea na bibi kwamba raiki yangu kapata mwanaume shoga ila ana hela balaaaaa. Bibi yuko dada ikooo, namtengenezea amlete tu huyo mgonjwa na laki 5. Nikaongea nae bwana kuna dawa kuna mbibi ana dawa.Traves alifurahi sanaa akasemayuko tayari kwa hio dawa. Bibi akaambiwa akatoe tiba hoteli. Bibi kaja na chetezo, kaomba mkaa room service akabandika ndizi inaiva na mto mdogo mdogo. Traves akaanza kuogopa sasa tiba hio akajkazaaa tiba ikakamilikaaa. Aliumwaaa aliumwaa, aliumwaaa. Ila akapona kabisaaa.
Wakawa wanaishi kabisaaa, wanapendanaa hatari, mpaka akabeba mimba kabisaaa. Tatizo wote wakawa wanatumia vile vitu vya sumu, kwa hio ikawa wote wana bembea mda wote. Na yeye tamaa zake akawa ashaanza kusafirisha unga, ikawa wanaishi poa tu mpaka alivomwabia kamuona kwenye gazeti na anakuja huku kumfatilia. Yeye akaibiwa simu siku akiwa arotsoo ndo Gill kuja kumwambia kuwa Traves akafariki na ashazikwa. Ndo arostoo imemzidia kabisaaa. Niashpoteza maisha, shule nimechezea, bwana kafaaa kaniachia mtoto.
Stacy roho ikamuuma sanaaa. Ila it was too late. Yule dada akaaga akasema atakuja kumuona mtoto from time to time. Mtoto kamlilia mama yake ila ndo akaamua kumuacha kikomandoo. Gill kumfanyia mtoto shopping upya, ana google kabisa na kumuuliza Marrie mtoto wa umri ule we anapewa chakula gani kwa ratiba gani. Anamuandikia dada na kumsisitiza kwamba ile ratiba ifwatweee ooooh.
Mwanzo Stacy akaona kama usumbufu si mnajua amambo ya watoto tena, mara kashika hiki,mara kile wanaboa haoooo haswa ukiwa umezoea mambo yako na privacy yako. Ila wiki tu akawa kakazoea mpaka mda wot anatamani akae nacho. Ujjue watoto wana innocence na unconditional love. Katakupenda basi tu. Na macho yake kanakuita mmama. Katakusemesha vimaneno visivoeleweka, and the smile is pricless. Na vile alivoanza kulishwa na kuogeshwa mara 3 na nguo za bei ghali akaanza kuwa toto, toto kweliiii. Stacy akawa kama mjinga sasa, anataka amlishe yeye amuogeshe yeye akaamini kweli mtoto anaumaaa, hajmzaa ila anavokapendaa je angekazaaa.
Gill is excellent with children, sababu si tayari anao wa 2 and very experienced. Anaweza kuwa kep entertained for 2 straight hours na katoto hakaboreki. Stacy akambadilisha jina hilo la Justin akaliona baya akaamua kumuita Prince nyumbani, ila shule akakubali ataitwa hilo hilo Justin cause ndo alipewa na marehemu baba yake na Stacy hakujua why.
Akarudi kazini basi kama chizi kila mda anapiga imu nyumbani kuulizia mtoto. Wenzie akaanza kuishi nao vizuri kama kuulizia watoto hawajambo, ku take time kumjua mtu na story yake atleast akionana nao anauliza warembo wetu hawajambo, au wakaka wazima, au kama anakaa na mzazi wake anauliza bi mkubwa pressur vipi mmeamkaje huko. Watu wakasema Stacy kakua sahivi. Na watu wakanza kumzoea sasa.
Siku hio Laurent akaenda kumuomba promotion, manake legal fees zimekuwa kubwa sanaa, akamuelezea kwamba alipata kazi ingine inalipa vizuri sanaaa, sanaa sema akashindwa kuichukua sababu ya mtoto mda wa kumuangalia atakosa. Ila sahivi anahitaji helaaa, anaomba awe promoted. Akamsimulia vita vyak na mkewe n kwamba h is raising his son alone. Stacy akamshauri tuakamuome Gill, he is a nice man atamuelewa. Akamwambia na yeye ana mraise mtoto wa kaka ake maehemu peke yake. Wakakubaliana they should hook up on play dates, manake yeye Stacy hana experience hivooo. Wakabadilishana namba.
Sasa Gill wakawa wanatibuana swala la mtoto, yeye kwa mkewe kakimbia hayo hayo mambo ya watoto aje kwa Stacy wale good times, na kuspend quality tim, sasa na huku nako anajikuta anataka kukabidhiwa majukumu ya ubaba wa hiari. Heeeeeeeee.Akawa bored si kidogo. Akaanza kupnguza kuja kidogo kidogo. Stacy akimuhitaji hawezi kuja mda mwingine makususdi tu, labda amwambie wakutane hotelini.
Stacy akawa na hamu kweli ya kuwa na mtoto wake yeye kama yeye afu wa kike sasa. Akaanza kumbembeleza Gill wa try for a baby. Gill akakubali kwa roho moja manake si anapewa free match, unlimited sex hio. Hahaaaaa. Stacy akawa anamkumbushia kila siku lini unamuacha mkeo, Gill anamwambia nipe mda nipe mda. Ikapita miezi 6 tangu mimba itoke bado anadai mda tu hakuna progress.
Stacy alivoona miezi 6 hashiki mimba akaenda hospital kupima, akaambiwa hana tatizo lolote amuite mumewe aje apime. Kumwambia Gill akafurahi kinomaaa, afadhaliiiii. Akamwambia mi siwezi kwenda kupima sababu nina watoto 2 kwa mke wangu, labda Mungu hajakupangia tu. We should keep trying. Hahahahaaa.
Siku hio Stacy kambananisha kisawa sawa kuhusu Harusi, Gill akaamua kumtolea uvivu tu kwamba ASAHAU HILO. Mkewe hawezi kumuacha leo wala kesho. For what? Stacy kwanza mda wote hajamzalia chochote zaidi ya kumlia hela tu, isitosh he has a beautiful familly why would he give it up for her? Kwa uchi gani wa maana alio nao, maana wale watoto ni damu yake yeye malaya tu kama malaya wengine sema nini yeye malaya mwenye bahati. Kwanza kazeeka, na yeye Gillis seeing some one else a younger version of her, some one 23. Kwa hio it is over between them. She is on her own, atafute ustaarabu. Heeeeeeeee! Chinekeeeeeeeeeeeeee! Heyyyyyyyyyyyyyyyyyy!
Stacy alijikuta UTI inamfumuka mwilini, sio kwa kutemwa kule ghafla. Akajilaumu sanaa kwanini hakuwa na uwezo wa kushika mimbaaa. Akasikitikaaa. Akanyongeaaaaaaaaaaa. Alimkumbuka Harris siku hio. Akakumbuka alivorudi tu aliambiwa ameresign, hakujua why. Na hakutaka kufatilia sanaa manake that time alikuwa focused na Gill hatariii. Alikondaaaaa. Akataa aache kazi, ila akaona maisha yatamshinda, akaamua kukomaa.
Gill huyo mwanamke mwingine kamleta pale pale ofisini, kumkomoa tu, she was yonger, versatile and bold. Akaanza kunyanganywa gari, akanunua Rav 4 yake. Kodi ilivoisha nusra nusra almanusra akampigie magoti Gill ila akajiambia hivi wanaishi huko uswahilini si wanaishi tu akatafuta nyumba ya uwezo wake akahamia. Akasem yeye Stacy kumuangukia Gill sio yeye, boa hata afe ila sio kumuomba msamaha Gill. Sio kwa kmdharau kisa Ugumba. Sio kwa kumdanganya mambo yote yale. Akamuamisha mwanae shule. Aliyumbaaaaa sio kidogo. Watu wapo Stacy kwisha habariiii yake.
Yule dada akaanza kumchokonoa, huu mchepuko mpyaa, unajifanya nao boss wake. Gill was harsh towards her kazini, anamjoboa mbele ya watu kwnye presentations. Nyanyasika upate akili, akakomaa kumkomoa tu Gill, her presentations got better and better mpaka Gill akiwa anamjoboa watu wanamshangaaa anacho mjoboa nini mbona strategy kali sanaa. Basi anavo improve Gill anapanick hatari.
Wakawa close sanaa na Laurent sababu ya watoto na Sacy akawa bored, basi anamuuliza Laurent unafanya nini, labda nampeleka mwanangu mpirani, anamwambia nitakuja na mimi na Prince. Au weekend wana toka wote beach na dada wao wa kazi na watoto. Mpaka mtoto wa Laurent akawa anamuita Prince my brother. Mtoto akiumwa anampigia Lau ampeleke wapi, Lau ana msindikiza, shule akampeleka pale pale kwa Lau alipompeleka mwanae. Mungu mwema mlango mmoja ukifunga mwingine unafunguka. Wakawa close mpaka ofisini wakaanza kuhisi ndivo sivo.
Ule mchepuko unaendelea kumjoboa Stacy, unamuandamaa. Stacy akamwambia Lau, huyu dada nataka nimnyooshe. Yeye si anataka ligi, nitampa ligi mpaka afurahi. Hivi sahivi nieacha ushangingi nimebadilika anaona ananimudu sasa naanza nae. Nipe mwezi nitamnyoosha. Hela ya kuchezea kununua botic za mjini hana akaagiza Ali express new wardrobe kule bei poa na viatu, ma lace wig hatariiiii. Akatafuta saluni za bei poa poa, sasa clenser na facial za bi ghali hana uwezo nazo, akachukua manjano, rose water, riwa, anapaka kila siku kabla ya kulala akiwa anacheza na mwanae. Siku hio jumatatu akatupia nguo yake ya kishangingi na kiatu kirefuuuu asante Ali express. Watu wakasema mwenye kampuni yak karudiiii. Patamu hapo.
Ule mchepuko mshamba afu hauna damu ya nguo kabisaaaa. Stacy hatumii nguvu ila anampotezaa. Gill akaanza tena ku question maamuzi yake, alikosea nini mbona kama alie muacha analipa zaidi. Sasa alishakunyaaa kwa Stacy huku bora bakie kule. Kila akitaka kubakia kule roho inamuuma. Afu anavomuona yupo karibu na Laurent anahisi tu hapa lazima Laurent anamla, roho inamtokaaaa. Anajikumbusha jamni huyu demu nilimuacha mwenyeweee lakini mbona hivi. Anajikaza ila roho inamuuma sanaaa.
Stacy akawa anamsindikiza Lau mahakamani, mpaka wakajuana na mkewe. Unadhani wakikutana hivi Lau na mkewe ni maadui, walaa wanaongea kabisaaa sema ni kurushiana daggers mwanzo mwisho. Ila wanakaa wanaongea na wanacheka kabisaaa. Mke wa Lau alivomuona Stacy, na Stacy anasikia anamwambia Lau atleast ume upgrade this time, but isntshe a bit too sluty for a single a daddy? But you always liked them slutty anyway. Lau anamrushia na yeye atleast she is way cuter than you and has a nice ass, ialways liked ass. Wanachekaaa. Mkewe anamjoboa tena, i herd you are bankrupt and you cant keep up with the legal fees, and i am just getting started isnt it a bit early for you to be bankrupt i haven't sued for child support yet in $$$$. Lau anachekaa, anamwambia the way i herd you are new man is loaded im planning to sue for Alimony myself. Mkewe anamjoboa i always took are of you what will it stop me from caring for you few more years. Yani wanaongea tu poa mbona. Basi mkewe anamwambia why dont you just give me our boy and live happily ever after with miss Slutty over here, wont you love that Slutty? Keep him all for your self infinity and beyond"
Stacy akaona anapitwa akaamua kuingilia mtanange , first of all we aint dating, and you can keep him i pass. Mke wa Lau, anamjoboa really! come on if you are facking my Ex husband have the decency to look me in the eyes and admit yes i am facking your baby daddy, not that it will break my hear, but it will be a bonus to slaughter him in the trial and show what a womaniser he has always been. Wanajikuta wote wanacheka. Mke wa Lau akili zake sio nzuri kabisaaa. Mara akimuona Price awahi kumbeba na kumwambia Lau, if we kept making babies we could have had a princess too at his age, too bad you were caught ina dick show around the city. Yani unaweza shangaa hawa watu wamefikishanaje mahakamani jisni walivokuwa na matani.
Gill uvumilivu ukamshinda akaanza kujisogza kwa Stacy, akampa increament ya mshahara, bonus alikuwa anampiga mswaki akazirudishaaa, akanza kujisogezaaa,akamuachisha yule mchepukooo kazi, mara akaenda kumuona Prince shule, mwalimu a Prince akamwambia, yani anajisogezaaa kabisaaa unamuona live. Stacy akamfungia viooo. Uzalendo ukamshinda akamuita ofisni kwake.
Bila haya akaanza kuomba kurudi."aby i know i treated you badly, i want you back by my side, nimejua makosa yangu, i am changed person. Dont make me beg, you want me back tooo. Turudi kuwa Bonnie and Clyde and take over the world once again." Hana hayaaaaaaaaaaaa. Stacy akamwambia tu "Gill i ni mgumba yule yule, nimezidi kuzeeka kuliko wakati ule, your precious wife and familly ni wale wale, what has changed? Nothing! Tusipotezeane mda, thanks for everything kwa ulivonifanyia nyumaa, nikiacha kukushukuru shetani mwenyewe atakasirika ila kila mtu aendelee na maisha yake dear. I wish you all the best." Gill akaanz akupanic na kutaka kumcontrol kama zamani ile kumpangia na ku dominate , Stacy akamwambia "Gill i am not a little girl anymore" Akafungua mlango akatoka zake akaenda kumfata Prince shule.
Kwenye parking hana hili wala lile akagongana uso kwa uso na Harris akiwa na katoto kadogo kakike ka daycare center kama kana mwaka barely. Wakasalimiana, za siku, nzuri, upo nipo. Stacy uzalendo ukamshinda akamuuliza huyo mwanao? Harris akamwambia ndio huyu mwanangu. Stacy moyo ukafanya paaaaaaaaaaaaaaah! Akamuuliza anaitwa nani kujikosha tu basi. Akamjibu anaitwa Stacy. Akamjibu tu hongeraaa sanaa. Anashika kimkono Staccccy, kitoto kina smile. Akaanza kujikosha huyu mwanangu nimemzaa anaitwa Prince. Harris akachekaaa, akmwambia we Stacy huyo mtoto ana miaka 4, mi na wewe tumepotezana just 2 years na ulikuwa hujazaa au unanifanya nimekusahau? Stacy akajichekeshaaaa tu ndo kabmbwa mgumba afanyaje. Akajikosha mototo wa marehemu ndo namlea ila hajui kama mimi sio mama ake. Basi Stacy yupo na kitoto, yaani kitoto chako kizuriii, jamaniiii, hata yul mtoto wetu angekuwa mzuri hivi hivi. Harris akamjibu tu mzuri kama mama yake. Stacy akajua lile dagger karushiwa. Akanyweaaaa na kuaga fasta fasta.
ITAENDELEA SAA 5 USIKU.