Hell is state of mind.
Nikiwa pale chini bado nimefungwa kamba baada ya kukutana uso kwa uso na israel mtoa roho za watu, nikawa nimebaki nahesabu tu dakika. Nishakata tamaa. Maana pale kwangu panaweza kupita hata wiki 2 hajakatiza hata paka. Sauti haitoki, majirani wako mbali. Nikawa nimekaa tu natubu, kulichungulia kaburi sio mchezoo msomaji kuwa nikipona mimi Leila, natubu, nafanya tu Ibadaaa. Umalaya baaas, ushetani baaaass. Namwambia Mola nipe nafasi ingine, sikuangushi. Kweli kweli kabisa ukiniachia uhai, SILIPI KISASI LWA SIZA NAMSAMEHE ROHO MOJA. Hata niingiwe shetani gani silipizi kisasi. Wewe sio Mungu wa visasi. Mbele ya ubai tena nafanya bargains juu bargains
Yakapita masaa 2, nikasikia piki piki. Nikahisi tu yule Siza kaja kunimalizia. Sasa nimetupwa design nalipa geti mgongo. Siwezi hata kujigeuzaaa. Nikasikia sauti ya Mangi, Leilaaa. Nikajua baaas. Kaja kunimaliziaaa huyu. Siza kaanza Mangi anamaliza mchezooo. Nikajikausha kama nimekufaaa. Walau akate tamaa aone ashakufa mtu huyu. Kufumba macho ikawa kosaaa la jinai. Sikumbuki nini kiliendelea.
Najikuta niko hospital na Vicky. Akaniambia pole, nasikia ulivamiwa na majambazi! Mmmmmh nikawa sikumbuki chochote. Akaniambia Mangi ndo alikukuta una hali mbaya sanaa akakuleta hapa hospitali. Alivotaja Mangi picha zikaanza kuja. Sema zinakuja lwa kasi na kupotea, vipande vipande. Nikataka kunyanyuka nikaona siwezi. Vicky anasema umefungwa jiweee. Umeteguka mguu. We kojoa tu una mpiraaa.
Kila nikikaa pale nawaza Siza anakuja kunimalizia. Napanga mipango ya kutoroka. Nikawa sielewi kwanini Mangi kanileta pale, au alijua analeta maiti nini. Mchana akaja Mangi, nilivomuona tu, nikafunga macho. Amekaa amekaa mpaka kaondoka mda ulivoisha. Kesho hivo hivo akija najifanya nielala. Akaja na Vicky nikajifanya nimelala. Vicky amsha, amsha na wewe , sasa Vicky dr, najifanya muite Dr. Najisikia maumivu makali sanaa. Sasa yeye pale staff wa zamani, nakubali kuchomwa diclofenac ilimradi tu.
Siku ya tatu nikamwambia Vicky anipe simu yangu, nikaichaji na kuiwasha kuwapa watu taarifa, nilivamiwa na majambazi kidogo yaniue. Maana ishu nzima ilikuwa ya aibuui afu ningeonekana muongooo. Maana mpaka mwenyewe siielewi. Nikatolewa lile jiwe na kufungwa ogo, nikauziwa na magongo. Nimepata nafuu, sema midonda donda bado nai dress. Damu zilizovilia zikaanza kupungua.
Pata matatizo uwajue watu. Kwanza nilijua taarifa sijatoa, hata baada ya kutoa Vicky ndo alikuwa anakuja sanaa. Fupi alikuja mara moja, ndugu wa mama, ambao nao hawana uwezo. Na mama alikuja kutoka mkoani. Mangi alikuwa anakuja kila siku maskini mpaka nikaanza kumsemesha. Nikamuomba msamaha infact yale mambo ya dunia tu. Akasema nimekusamehe hata Siza hakunishirikisha hili, kwanza urafiki umekufaaa. Sema nini Mangi ,cheshi sanaa, afu si kajiajiri basi anakuja tunapiga story. Usimdharau mtu maishani iko siku thamani yake itazidi dhahabu.
Usiku bado napata night mares, naipiga miyoweee, nakufaaa, nakufaaa, ananiuaaa. Mpaka wananishtuaaa usingizini. Siku wakaniuliza we majambazi yaliokuvamia kuna mmoja unamjua jina? Nikastukaaa, hapana kwanini? Wakasema unamtajaga mtu anaitwa Sizaaa! Unase,a sizaa usiniueeee, usiniueee, mara Mnyalu sio kweliiiii, sio kweli Siza anakusingiziaaa. Nikajikausha ni ndoto tu, mi hayo majina sijawahi hata kuyasikia. Wakanidaka kila siku unataja majina hayo hayo 2. Kila siku. Kwanini? Nikakomaa ni ndoto.
Baadae nikatoka, nikaamua kwanza niende nyumbani kwa mama ili aniuguze. Maana ndo wa kuogeshwa, kuoshwa vidonda, na mi mjini sina mume, sina ndugu, ningeishije. Kama nilivowaambia mama yangu Kungwi mzoefuuu. Nikiwa pale naona wali wanakuja wanachezwaa, nasikizaaa kwa pembeniii. Likanijia tu wazo na mimi niwe Kungwi kuongeza kipato. Nikapanga niongee na maza.
Nikamuita kikao, mama nimeona niko tayari kama mwanao wa kwanza wa kike, kuupokea huu mkoba wa ukungwi. Nokee kama mwanafunzi wako na unipike nipikike, niendeleze mikoba ya bibi Asha, bi Radhia, Bi rahma na wengie waliotangulia kabla yao. Mama akachekaaaa sanaaa. " Leila unanisikitishaaa sanaa, umeuzaa huko mjinii wewe mpaka wakakukata kata na mapanga, nikajua ushayajua ya duniaaa, unarudi Msikitini ku swali kumbe ndo unautamani ukungwi, sababu umekoswa koswa kazini, najua hakuna cha majambazi wala nini, kazi zako na kina Siza na Mnyalu mkacharangana mapanga, umeona ushakoswaa sasa usiende tena front ila umalaya wako uwe una ufundisha, wanafunzi wako wanaenda front wanakuletea chochote kitu.
Alinikeraaa, sio siri alijisemea baba mwanamle asiesomaaa ni hasara tupuuu. Nikaamua kuongea nae lugha yake."Sikia mama we umekuwa kungwi miaka karibia 25 na zaidiii hakuna ulichofaidikaaazaidi ya kufa maskini, na ukungwi wako wote baba malaya namba 1, na umalaya wangu nimerithi, na vya kurithi vinazidiii. Mi nataka huu ukungwi ni UCOMMERCIALISE, niutoe kwenye ujimaa wa mila na desturiiik, niufanye ukungwi biashara serious. Tunafunda wali wenye pesa, watoto wa vigogo, mawaziri, warabu, wahindi watu na pesa zao, unue hii elimu mtajiii. Tutanufaikaa sanaa. Think of it. Think of the future.
Nikasikia msonyo mkubwaaa sana. Mxiuuuuuuuuuuuuuuu! We Leila hujielewi, hii elimu ya ukungwi haikuletwa kwenye jamii sababu ya faida. Misingi ya ukungwi yenyewe yamejengwa kwenye kujali utu, upendo na amani. Ndo maana wanachezwa wali. Watu walio mapenzini, wanaenda kuanza kuishi na wenzi wao. Sasa sisi makungwi tunawapa muongozo wa ji si ya kudumu humo ndani. Na huwezi kufundisha upe do ili hali wewe nafsini mwako huna upendo hata nuktaa wala chembe. Huwezi kumfundisha mtu upendo wakati u eweka pesa mbele na utu kando. Hio tu kinyume cha upendo.
Kungwi original kama mimi inanipa faraja kuona mwali niliemchezaa anafurahia ndoa yake, ana amani kwenye ndoa yake, ananiheshimu, ananifurahia na kunijali mwali wake. Upendo niliomfundisha ndo anaushi. Thamani ya hivi vitu vidogo sana kwamo, kwangu ndo kila kitu. Nacheza watu bureee kabisaaa. Baadae wakipata ndo wananiletea shukra i. Wananiheshi wana jamiii wenzangu kwamba nimewapa kitu kizuri maishani mwao.
Leila huna utuuuu,na una thamini sanaa pesa. Nikisema nijiroge nikupe hata nukta ya hii elimu na uhakika utawafundisha machangu, na utatoza pesa ndefuuuu sanaa, bila kujali hao machangu hio elimu wataitumia wapi, mradi wewe ushachukua mgao wako. Mwishowe miiko itanirudi hao hao uzao wako wa machangu professional watatembea na kaka zako, bab ako, wajomba zako na kuvunja ndoa zetu. Fikiria mijitu haina training yoyote ila ni hatari ukiipatia mtaala wa kuelimika je.
Na hata na hivo ushachelewaaa sana. Ukungwi una miiko yake, wa 1 uwe umeolewaaa, wewe hujaolewaaa. Pili kabla hujawa kungwi lazima uwe msaidizi wa kungwi si chini ya miaka 5. Sasa wewe una 29, ukiweka mitani si 34, ukija kupitishwa sasa kwenye mafunzo ya ukungwiiii wenyewe nyonga zishakaaa hizoooo mpaka mafuta ya nyonyo yatagoma. Utatafuta kunivunjiakia kiuno tu. Hii huwezi kuiwezaa mpaka uwe kungwiiii na upitie masomo ya juu ya ukungwi." Akachana msambaaa mpaa chini, akawa ananyongaaa. Unaona hiiii, sasa hapa unaushukia mchi na kuupandiaaa. Inaitwa chizi karogwa tenaaaa. Mwanaume hachomoiiii. Kwenye kudanga huko lazima akukabidhi funguo za Prado. Nakuonesha najua huwezi kuiwezaaa miaka 8000, tena usojidanganye kujaribu utachanik uchi huo kama mgonjwa wa fistulaaa, ushonwe nyuzi bila kuzaaa. Hahaaaa. Kumanage hii distance inachukua miaka ya mazoezi.
Enzi hizo unamuonesha nyakanga hii, hapo ndo unapimwa kama upewe ukungwi au watafute mwingine. Jicho likanitokaaaa. Naionaaa hela wazi wazi, tena inakuja kwa mafungu. Nikasema sikubali. Naendelea kumhadaa huyu mwanamke mpaka niupate ujuzi wake. Nikamtega "Kwa hio wewe mama unaona sawa mtu aolewe na FREE P, jianaume halina mbele wala nyu,aaa, analifugaaa tu, lina mlostishaaa, au akae single kama mimi akisubiria mtu anaelewekaaa." Nikasikia boraanaefuga bwanaaa. Ndo maana nikakwambia hii elimu ya ukungwi misingi yakeni upendo ambao wewe hunaa, umekaa kunufaikaa, kila kitu unataka unufaikeee. Huyo FREE P kaumbwa na Mungu yule yule aliekuumba wewe. Isitoshe ni binadamu kama wewe. Ungekuwa na upendo ungeona mbali zaidi ya ufupi wa akili yako kiwa hela hanaa, na hela kwako ndo duniaaa.
Sawa pesa hana, ila bado mwanaumeee yule. Atakuonesha upendo, akiamka anakuwaza wewe, anawaza akufanyie nini, akupe furaha. Ni kitu adimu sanaaa. Na mashamba yako yote ya miti, mamillion banl, vitabu vi 3 vya passport umeumwaaa hata bwana wa kukuuliza hujambooo? Sijui ulikuwa uanwachaji sanaa wateja wako bila hurumaa. Hahaaa. Kuna kuumwa. Pia mtu hata kama pesa hana, kukupa heshima mbele za ndugu zake na jamiii kwamba mimi huyu mwanamke ndo wa kwangu, nimefikaaaa. Kukumiliki mbele za watu, huyu wangu. Vitu kama hivi pesa haiwezi kununua. Mnabakia nina pesa bank! Pesa ingekuwa mapenzi si bank zote zingekuwa zimetolewa mahari na kuolewaaa. Jioni kila siku una mtu wa kukuetkenyaa, mtu wa kukusemesha, unapata dozi hupimiwi na mtu wala huoni hayaaaa, si mumeoooo. Aaaaaaaah! Jifunze kupenda leila usiangalie maslahi sanaaa.
Kanichambuaaaa kama karanga. Ikabidi mwisho nimuulize "Utanifudisha hunifundishi?" Akakomaa sikufundishiii. Duuuuuh nikajua hanifundishii kweli. Nikamwambia Mama umekosea sanaa, umekataa mwanafunzi kichwa kama mimi, sasa tutakutana kwenye industry ya ukungwi. Mimi nishajiamuali nakuwa kungwiii, na huwezi kunizuiaa, wewe usinifundishe ila kaa ukijua kungwi hauko peke yako duniani.
Mama akasonya tena, labda nisikie umekuwa mwalimu wa umalaya sawa, na utachofundisha sio ukungwi ni umalaya advanced profession, na mimi sijakupa ruhusa kufanya huo ufirauni umejiruhusu mwenyeweee. Utajua mwenyewe na balaa lako."
Nilikaa pale wiki 3, nikarudi kutoa ogo, na nikawa nimeponaaa kabisaaa. Niaksema embu niende saluni kidogo. Kitambo sanaa sijaenda. Na pale nilipokuwa naishi nikahamaa kabisaa, kodi nikaicha, pana mikosiiii na nuksiiii. Kufika pale wakafurahi kuniona ila kama kukawa na sintofahamuuu. Nikaomba kufumuliwaa. Wanakonyezana. Mwisho wakaniambia " Leila tunaomba kama unataka kuja saluni hii, uwe unakuja na zana zako, kuamzisa kitana, mikasi, wembe, sindano kila kitu, utusamehe tu." Nikauliza kwanini mnaninyanyapaaa kimetokea nini?
Wakasema " Siku hizi mama mnyalu anakuja na vifaa vyake vyoteeee mpaka blowdrier, hachangii kifaa na mtu. Yule mama sio mkorofiiii, sio mshariiii, yule itakuwa kajua mumewe kaathirikaaa, na yeye haja athirika, ila wewe ndo umemuambukiza mumewe, hivo anajua unakujaga hii saluni utamuambukiza. Sasa sisi wengine imebidi tuchukue hatua" zile habari zilinistuaaa. Mnyaluuu kaathirika? Nikawauliza nyie mmepimaa mpaka mninyanyapae, ukute nyie ndo ma carrier wakubwa. Sawa bora niwe na vifaa vyangu nijikinge na nyie. Wakaniuzia kila kitu changu.
Nikawaambia nimekuwa kungwi siku hizi, nafundisha elimu duniaa. Wakija wale wateja wenu ma boss boss waambieni kuna kuna kungwi toka commoro, sina hata bei laki 5 tu kwa kozi nzima. Wakasema commission ipo? Nikajibu ipo.
Kufika home na kufika simu inaingia, hello kungwi wa commoro! Hahaaa, nikaitikia hello, nina mwali nahitaji afundwe, huku Mikocheni Ada estate, itakuwa bei gani, mwezi mzima. Nikasema Million. Akasema sawa. Nikamalizana nae. Mmmmmh! Biashara ishanogaaa mapemaa. Nikajaribu kuchana ule msamba naona niko juuu hahaaaa, yani juuuu hata kuukalia sijakaribia, paja zote zinaniuuuuma, hazitanukiii zaidiii ya pale, nikasema nikijilazima fistula itanihusuuuu. Nikampigia mama. Kuna mtejaaa. Akachekaaaa. Hivi ulikuwa serious unataka kuwa kungwi, hujajiaibisha huko bado? Hahaaaaaaaaa! Sipati picha, mwanagu nyonga zilivokukaza, unakata tumbo toka mtoto, hahaaaaa. Nikakata simu. Kesho akaja akaenda kumcheza yu
E mwali. Kwanza kasema wiki tu inamtosha wasipoona tofautiiii kazi atainawa watafute kungwi mwingine. Mwali wa kiarabu.
Mwali kigegoooo, kigegoooo bora hata Leila. Hahaaaaa! Mimi ndo msaidizi wa kungwi, mwali hainui kiuno, naona anwekewa misumari chiniii analiaaaa. Anatandikwa bakora, mi i ndo mchapaji wa hizo bakora, mda mwingine mama ananikonyeza tu ananizomea, unamtandika mwenzio wakati hamnaa hamnaaa mwenyewe. Shughuli kule pevuuuu. Kidogo nighiri ukungwi. Ila Mnyalu kanitemaaaa, umalaya nimeacha, nguo biashara ya msimu si nitakufa njaa mimi. Nikakaza roho.
Mwali anaambiwa chuchumaaa, kama Leilaaa, tanua miguuuu, anatanua kwa woga kungwi anamchota mguu, anapiga yoweee, nakufaaaaa. Mi nachekaaaa sina mbavu. Siku ya 4 naambiwa baki nyumbani sikuhitajiii, mazoezi ya vitendo yameisha leo, tunaanza kumpa maidhaa, na kumfudnsiha vya ndaniii kabisaa. Wewe mume hunaaa, hakuna kuja,mama Munira ashafika Dar, ndo tunaenda nae. Nikawasema sawaaa tu, ninyimeni elimu. Haki nilitamani hata nifunge ndoa ya mkeka na mpiga debe vasi tu ni qualify mafunzo ya ukungwi. Machana nafa ya mazoezi yale mastyleee.
Siku ya kulipwa kaja na milkion, namuuliza comission ananiambia mmaa Munira kapewa 500,000 na yeye 500,000 nauliza mimi je? We sio kungwi wala msaidizi wa kungwi huwezi kupewa mgao wa mwakungwi. We kipereto tu. Duuuh Mama monster ndo huyu.
Akaja mteja mwingine, nikasema malipo kabla, nikawambia kama kawa mi siku zangu 4 za mwanzo, baadae nikafukuzwa mwisho wakambiwa pesa ishalipwa lwangu tangia mwanzo. Wakaja nikawapa laki 3, 3 mi 4. Walisusaa. Kufika Iringa kila mtu, Leila nitumie nimebanwaaa, nyooo, njaa ina kungwiiiii.
Ikawa kila wiki ina mteja mpya. Wanaambiana wale wa mama, kamcheza falnii, kamchezaa flani. Afu mama mtu wa staraaaa, shungi saa 24, swala 5, akiongea hekimaaa, akawamalizaaa waarabu akawamalizaa. Nikawaza hii ya mwali mmoja mmoja hatutofika. Niakleta wazo tuanze darasa, tunapokea wali hat 10 hata 100 pale kwangu tunawaburuzaaa 1 week, tunapiga pesa ndefu mmoja 1m wakiwa 100 kwa wiki tu tunapata 100m. Wakagoma sio miiko, wiki 1, mwali mmoja, ubora wa kazi ni muhimu kuliko pesa, maisha ya mtu yale. Nikasema basi wagawane kila mtu mwali wake walau wiki moja tunaingiza 2m. Wanakubali huku wanalalamika leila utatuua, na tamaa zako, tu etelekeza familia kuja kwenye huu mpango wako, wau e zetu wanalala peke yao, sisi tunakomaa na wateja. Nikawaambia sababu huyu hamna hamna mnapata 1.2 million kila mmoja kwa mwezi na waiting list ni kubwa bora muhamie dar, mkoani ukungwi 50,000 ikizidi 100,000 mnapoteza kipaji.
Cha kufanya mje makungwi hata 30. Mimi naweza kuleta wateja 30 kwa wiki, tukapata pesa nzuri tu. Actuallu mi ndoningepata yingi cause kila mmoja nakata 400,000 ya udalali, wakiwa 30 sio mbaya kwa wiki hela ndefu hio. Haian mtaji, haina kodi, haina gharama za uendeshajii. Nguo nilimuweka mtu asiammie anileetee tu pesa flani ambayo wote tunapata mi nisimame kwanza kwenye ukungwi.
Wakahamia Dar, ila bado ambition yangu ya kuwa na shule ya ukj gwi nayo admit watu wengi ilikuwa pale pale nikawa najilobby kwa amkungiw wengine kama nitapata kungwi njaa avunje mwiko kuendekeza njaa anipe training.
Kutafuta kote huku hela, nilikuwa natafuta hela ya KISASI. Sawa nilisema sitolipa kisasi, ila nilishindwa kabisaa mazeee. Nikajua vita bila pesa ni kujitoa muhanha. Nikaanza kuikusanya pesaa, huku nangoja wakati wangu ufike, nifanye yangu. Sijasahu wala sijasamehe hata robo.
Siku hio nimekaa, mama akasema Leila una mimba! Tena kubwaa tu. Cheki puaaa, cheki shingo, mapigo ya moyo yanadunda mawiliii. Umefanyaa zinaa mpaka umeleta mtoto wa zinaaa. Nilistukaaa. Kama sikuanguka stroke siku hii basi, siangukii tena.
Nikaenda kununua kipimo kitu na box. Doooh! Nikapita dukani kununua majani ya chai pakti 5. Nikachemshaaa jeusiiiii kweli kweli. Mama anauliza unatengeneza hina? Namjibu eeeh hina. Nataka ninipake. Ilivopoa nikanywa sufuria nzima. Najua jioni kazi imeishaaaa. Najilaza najua mda wowote Simba watachezaa. Mpaka asubuhi holaa, mpaka keshooo holaa. Ikapita wiki.
Nikampigia Dr. Kumuuuliza hivi ukitoa mimba chini kuna rudi kama zamani? Akasema hapanaaaa! Kunaweza kusirudiiii, sijui nini. Nika google abortion inavofanywa pyuuuuuuu! Nikaona siwezi kujiua wakatikuna uhai wa mtu bado naudaiii. Niakresearch nikaona blue inatoa mimba! Nikanywa blue 3. Holaaaaaa! Duuuuuuuuh!
Nikamshirikisha Dr, maana nikaona sasa hii mimba kinganganizi kuliko Bashite anavongangani cheo. Dr akanimaliza kabisaaa. Kuwa kwa nilivoichokonoa hio mimba na attempt za kuitoa nilizofanya possibility ya kuzaa mtoto mzima ni ndogo sanaa. Uwezekano wa kuzaa mtoto kilema ni mkubwa sanaaaa. Nilitetemeka.
ITAENDELEA KESHO