Weekend Story! The Grass is always greener on the other side

Weekend Story! The Grass is always greener on the other side

Being wrong is the easy part, taking responsbility for your actions is the hardest part!

Kiukweli toka moyoni mwanguuu, ile simu aliopiga Leila was a final straw. Kama nililishwa nyama ya matako basi niliitapika ghaflaaaa. Yaani kitendo kile linichefuaaa beyond measures. WHY? WHY DID SHE HAD TO THAT? Ni dharau kubwa sanaa kumpa mwanaume mwenzangu mwenye pumbu kama mimi anisemesheee. She could have broken up with me a million ways without insulting my pride. Tena nilivokiwa bwege ningeendelea kumuhudumia even after break up. That is the kind of man i am. Sipendi wanawake wapate shida. Especially wanawake ambao nimewatumia.

Ama kweli ukicheka na mbwa atakufata mpaka msikitini. Na shukrani ya punda mateke. Punda huyu kanipiga teke la tigo na kwato zikazama ndani. Haaaaaaa! Na kilichoniuma sana sijui ni kipi kati ya kunipigia simu mbele ya mwanaume au kuniweka war front, kuni expose nije na SMG,, kwa ajili ya kudai mkopo wa uchi. Who in the world does that to their loved ones? Who?

Nilishajua kuna picha 2 zinaendelea nilikuwa navuta kasi tu nipate picha kamili ila nishajua something was fishy. Dots zilikuwa hazi connect. Hata kama usela huwezi ku walk in kwenye banda la chips then mtu aje akupige doleee. Huweziiiii. Impossible. Anyways. Ila mimi Leila kanikosea heshima sanaaaa.

Sababu mtu mzima, sita mblock, wala nikikutana nae sitompita kimya, nitamsalimia vizuriiii tu. Ila uhusiano baina yetu umekwishaaaa. Na nitafanya yote hayo sio kwasababu i have feelings for still, no, ila because i always treat women kindly, hata beki tatu wangu anajua hilo. Sio mkatili wa kijinsia and i am not planning to start.

It just struck me, i have treated my wife very badly. Very badly. She is always here for me, despite dharau, kiburi na majivuno, she is here happy to see me everytime, never even once asking for anything. Na anajali sanaa, mme wangu unapunguaaa, mme wangu unanenepa, nikiumwa anajaliiii. Kila nachofanya anajali sanaaa.

What have i done for her NOTHING. Kwao bado kuna nyumba ya udongo. Kunizalia kanizalia ila still i have done nothing for her. Absolutely nothing. Hata Leila alipata biashara hawezi kusema kaondoka mikono mitupu. Michepuko mingine naipa vitengo kazini. Ila mke wangu hajaambulia chochote.

Nikaka pale natafakariiii sanaaa. And i vowed to change and atleast give her the respect she deserves. We are most cruel to the people who love us most. Nimeliona hili leo. Kumchungulia kajaaa kitanda kizima kama simtank, kidogo nighairiiii. Ila nikakaza roho. Nikawaza kwa ushenziiii na ufirauni naomfanyia kajitahidi sanaa kuwa vile, na kulala kitanda kimoja na mtu mshenzi kama mimi.

Asubuhi naamkaga mwenyewe, na wala siagagi, si kwangu pale kuna mtu ananidai. Ila siku hio nimejiandaaa, nikamuita Mama Janeth, hili jina la Janeth ndo anamuita mwanangu kinguvuuu, hataki jina Leila, nikimuita mama Leila haitiki hata kama tunatizama hahaaaa. Nikitaka kumnyima kitu, au kutafuta ugomvi nisirudi wiki nzima namuita mama Leila. Asipoitika tu naanza umekuwa na kiburi na dharau sanaaa, hapo hapo nachomoka na kubamiza mlango nakaa hata wiki 2 sirudi.

Akaja, akajua kuna jambo. Nikamwambia "Niandalie chai" Astukaaa. Akaita dadaaa! Nikamuuliza " Nimekwambia wewe, kwani sijui kama dada yupo? Kiburiii mke wangu hiko." Anajitetea sio hivooo, sikumbuki lini umekunywa chai humu. Akaiandaa anataka kuondoka, nikamrudisha, "Ndo ulivofundwa hivo ukimtupia mumeo chai unawahi kulala, wala hukai nae kumuuliza mawili ma watu au kupanga kitu?" Akaketi kimya. Namuuliza Janeth shule vipi? Na maendeleo ya nyumbani pale, kuku wake wanaendaje, maana ndo mradi wake mpya. Nimemaliza nikaacha maagizo "Upike nyama leo si unajua si wahehe kwa nyama, nawahi kurudi leo. Mi naenda mke wangu kazini. Ubaki salam."

Jicho likamtokaaaa. Nimefika mlangoni akasema rudi kwanzaaa, leo ni kwamba unaenda kufa huko njiani amaaaaa? Isije kuwa ndo unaniaga aga mkeo hapa, sijaelewa elewa siku ya leo inavoenda. Unajua nini, rudi ndani baba Janeth hakuna kutoka, leo sio siku nzuri kabisaaa. Itakuwa kuna kitu kibayaa sanaa, huamkagi hiviii. Moyoni nikawaza ama kweli nilikuwa shubhamit, kutenda wema kidogo ishaonekana uchuro. Nikamtoa hofu, hakuna lolote, Mungu mwema, mi naenda kazini na nitarudi salama.

Niko kazini nikampigia simu, kumjulia mchana wake unaendaje? Si mnajua tenaaa! Alipokea simu na kiliooo. Nilijuaaaa mimi anaenda kufa mume wanguuu uwiiiiiii, yewiiiiiiii! Nikamkatisha wewe Maria, unataka kuniua nini mbona unanichuria kifo, mara ya 2 hii kwa siku 1. Akafurahi kusikia sauti yangu. Akasema hupigagi simu mchana, hujawahiiiii, zamani sanaa, sasa nilivoionaaa, nikajua tayariiiii, bomu lishalipuka. Nikamwambia acha uchurooo, mi nipo nipo sanaaa.

Nikamuuliza kati ya iphone 6 na Iphone 6 plus unaipenda ipi zaidi? Akasema mi hata sijui mme wangu ya bei rahisi kati ya hizo nitashukuruuu. Nikamwambia sijakwambia bei, nimekuuliza unapenda ipi? Yupo sijui sasa, ngoja nimuulize Tina yule shoga angu nakupigia. Akanipigia kasema 6 plus nzuriii mwee, ila hii bado inafanya kazi vizuri tu. Nikamuuliza mtoto karudi shule, mpe simu nimsalimie. Nikawasalimia.

Saa 12 kamili niko kwangu, nakagua home work. Toka vidudu sijawahi fanya hio kazi. I wish mngemuona mke wangu anavojitia mama mwenye nyumba. Usiku nikawaita wote, house girl, house boy, wadogo zake mke wangu, wadogo zangu, tusali. Wakaangaliana. Nikawaambia ndo utaratibu mpya kusali kila siku jioni kama familia. Nimegundua nilivokuwa busy mambo mengi hayaendi sawa. Kama kula kila mtu anakula kwa mda wake ndo tabia gani, sipendi mambo ya ajabu ajabu kwangu, mnarudi mda mnaotakaa, huko chuo mnasomaaa au mnafanya umalaya? Sasa nasemaje mjipange upyaaaa, nyie wa chuo mnipe password zenu nakagua matokeo, ole wenuuu ole nikute mna supp. Sahivi niko mkabala na nyie mguu kwa mguu, narudi hapa saa 12, saa 1 na nusu, nafunga geti langu. Alie njee akatafute pa kulala.

Wakawa wanaangaliana, hawana la kusema, hawaa amini kwanza kama jini mkata kamba kapita anga zao. Mke wangu nae yupo pamoja nao kwenye kushangaaa. Utawala mpya walikuwa hawajautegemea, yaani ghafla tu, mambo yamebanwaaa.

Usiku nikampa mke wangu Iphone 6 plus mpyaaa, brand new kwenye box. Akafurahiii sanaaa. Na mwanangu Leila nikampa tablet. Acheze game, na nitakuwa nampigia simu. Mke wangu nahisi alijua ngoma ya kitoto haikeshi, akajua siku 3 nabadilika. Zikapita wiki 2. Na niliwafungia shemeji zangu nje, wadogo zangu si mara moja au 2. Na nikifunga geti, nimefungaaaa. Adabu ilirudi mule ndani. Jumamosi ndo walinikomaaa. Washazoe kubandika kucha, wale wa kiume wanashinda wancheki series. Heheeee! Niliwakabidhi mkasi wa mchongoma, fence iwe safi. Wa kike niliwaambia nikirudi nikute garden hapa la maua. Shemeji na Kaka Monster.

Baada ya wiki 2 za kuwa responsible na loving husband, nikaona huo muda muafaka wa kuanza kupewa tendo la ndoa na mke wangu. Isitoshe hata kama mahari sijatoa, si namlisha na wadogo zake kibaooo, wasinitanieeee. Nikampa taarifa jiandae leo nataka kula mzigo. Akastukaaaa. Hahahaaaa! Na mimi sikutoa maelekezo zaidi.

Usiku nimerudi, najua nakula mzigo. Nishagomba gomba, to be honest i enjoyed kushika nafasi yangu ya baba mwenye house, kuwajambisha jambisha. Nikahakikisha sala imepita, nikaingia chumbani kwangu. Akili yote napewa mzigooo. Mke kavaa night dress, walau hilo safiii. Linakuwaga fii. Moyoni nishasema hata kama hajanyoa nakulaaaa hivo hivo.asinitanieeee.

Namgusaaa akagomaaa. Nikasusa na kugeukia ukutaniii. Akaanza risala ndefu. Mme wangu nafurahi umerudi nyumbani kushika nafasi yako, ndo lilikuwa ombi langu kubwaaa, uache kurudi asu uhi, kuishi kama hutujui au hutuoni, na kweli leo Mungu amenijibuuu. Ila sasa nyakati zimebadilikaaaaa. Huko ulikotembeaaa sina ubakika umerudi salamaaa. Leila simwamini kabisaaa. Ili turudishe ndoa rasmiiii naomba TUKAPIMEEEEE UKIMWIIII. Roho ikafanya Paaaah!

Nikagoma kwenda kupima wiki 2 zikapita hatoi mchezo kavu kavu. Condom ndo napewa mzigo. Nikasema anyways cause ndo nipo kwenye mabadiliko acha nikapime nijue moja. Na mimi hofu yanhu si Leila ni watu kibao nilikuwa nagonga gonga tu. Na kweli mke wa gu ana haki ya kujilinda, na ni jukumu langu kumlinda mke wangu na mwanangh. Na kama kweli ninao, sio tu nitahatarisha maisha yangu tu na waote wanaokaa pale kwangu. Nikaamua NYUMBA NZIMA TUNAENDA KUPIMA UKIMWI. UKISHINDWA KULETA MAJIBU HAMA NYUMBA. Walilalamika, wakatishia kunishtaki TACAIDS nikawaambia mkishanishtaki, mkachukue ada TACAIDS. Nikatoa mwezi 1 kila mtu awe kapima kwa mda wake.

Nilitaka kwenda mwenyewe, nilifika ANGAZA, nikakosa ujasiri nikarudi, nikamwambia secretary wangu amabe nimemla kavu mara kibao, akapime yeye nitampa M5, kama yeye hana basi mi sinaaa, tumekanyagia sanaa ringi. Akaleta vipimo vya mradi, akajipima mbele zangu ikasoma Negative. Akaniambia njoo nikupime, nikagoma, nikasema nipe hiko kipimo. Nilifurahi sanaa, sanaaa. Nilipata moyo.

Nikamkuta mke wangu nikampa kipimo cha secretary, akakigomea, akasema twende mguu kwa mguu, atanisindikiza, nipimwe tungoje majibu. Ni katika safari ngumu sanaa nilizopita, kila nikiwaza secretary negative, napata moyo. Tukafika. Dr. akasema pimeni wote kuwa safe. Mke wangu sababu sio malaya na namjua sio muhuni akakubali fasta fasta, kimbembe mimi baba.

Mda wa majibu, Dr, akasema niwape wote, au nimpe kila mtu private. Mke wangu akasema tupe wote hapa hapaaa, hii ndoa daktariii. Nilijihisi nina bushaaaa. Nikasema nikipiga mechi kavu basi naanza kutembea na vipimo rasmi. Nampima mtu ndo namla kavu. Kama sina ngono zembe baaaaasss. Dr, akatoa ushauri nasaha mrefuuuuu sanaaa. Mwisho akatusomea majibu.

Nikaanza mimi kupewa majibu ya gu, vipimo vinaonesha Mnyalu niko NEGATIVE. Kmaninaaaaaa, ukimwi bongo umeishaaaa, hamnaaa ukimwi. Hamnaaa. Serikali ifunge asasi zote tu maana kazi ya kuumaliza ukimwi imewezekanaaa kwa aslimia 100%. Nilikata viuno ndugu msomajiiii.Sikuwa na shaka kabisaa majibua ya vipimo vya wife, cause alishazaa yule mtoto akapimwa afu sio muhuni hata kama muhuni ni small scale.

Dr akamsome majibu, vipimo vinaonesha POSITIVE, Maria umeathirika na UKIMWI. . Mke wangu aliachia ukunga mmoja tu, akajitupa chini. Mi nilisikia kama nimechomwa mkuki kwenye moyo. Furaha yote ikayeyuka. Nikamuuliza Dr. nini? Nikapora karatasi. Maria POSITIVE. Tukakaa kimyaaaa. Dr shauri shauri na wewe.

Moyoni nikajua pale hamna hamna Dr walichanganya damu, yale majibu yangu wame mix. Nikamwambia twende mke wangu. Njiani nikamwambia tupime na huku. Mke wangu ashavurugika kabisaa, mwenyewe nilivurugikaaa. Majibu napo vile vile MNYALU NEGATIVE, MARIA POSITIVE. Njiani nikampigia rafikia yangu Dr, aniletee vipimo. Pima tenaaa, vile vile mimi nimepona, wife amenasaaa.

Akili ILINASAAAAA NDUGU MSOMAJIIII.
 
mnyalu hajui mke wake alikuwa anakitembeza kisirisiri bila yy kujua
 
Jamani tutaendelea kesho nimechoka kinomaaa kuandika
 
Mh majonzi na masikitiko kwakweli maria wawatu jamani the world is not fair. not fair at all
 
Jamani tutaendelea kesho nimechoka kinomaaa kuandika

Kamanda! Kweli umekuja Kama Jecha Salim Jecha, ukisikia chenga ya mwili. Hii umetuweza. I bet no one not only expected, no clue at all. Upepo wa kisukisuli umetikisa jukwaa. Giza nene.

Hapa nimepata mwaliko but I don't think if I can make it, sio kwa episode hii. Nilikua nategemea Kama kawa team bundi unatushushia adult rated....hii imechoma moyo mnooooo!
 
Life is not fair.

Kiukweli mimi Maria baada ya majibu yale sikutegemea sanaa kama ndo ipo. Nafuu muwe wote mmeunguaa. Usiombe mwenzio awe mzima afu wewe umeunguaa. Nishajikatia tamaa, nikapanga nikifika tu nabeba begi langu, namuaga mwanangu narudi zangu kijijini kulima. Maisha popote. Au najinyonga tu.

I didnt have many regrets kuhusu huu ugonjwa, i was just sorry for myself, kwamba nilipata mume, mume hanitakiiii, hanipendiii, nikahangaika nje kutafuta company and to feel loved, imekuwa bahati mbaya huko nje nimeuzoa wa kuuzoa.

Mnyalu namjuaaaa, alikuwa anatafuta sababu ya kuniacha, na hivi kaipataaaa, baaaas tena. I ttied, God knows i tried to be the perfect wife, and mother. Unfortunately i failled. Sometime we are not in control of what happens to us. Nilikaa kimya, sikuwa na nia ya kuappologise au ku beg for what?

Sanasana nilikuwa naomba Mungu nikae kae hapo kidogo mpaka mwanangu akue, asilelewe na mama wa kambo. On the other hand nilishukuru Mnyalu ni negative akae hapo kidogo kumlea lea huyu mtoto. Hayo ndo yalikuwa amombi yangu makubwa na shukrani zangu.

Kuhusu nani kaniambukiza sikutaka kufatilia sanaa, cause isingebadilisha chochote. It is what it is. Na uamuzi wa kuondoka sikutaka mnyalu awe ana ni nyanyapaa. Bora nikakae kijijini. Maana kabla sijaumwa hali ikuwa vile ndugu msomaji je baada ya kujulikana haya si ndo nitabaguliwa mpaka basi.

Tumefika nyumbani mnyalu akawa nje hukoanafanya shughuli zisizo eleweka. Nikajua tu he was avoiding me. Nikaingia ndani nikapaki begi langu. Nikawaita wadogo zangu na kuwaambia inabidi wahamie hostel, mie ndoa imenishinda ndo naenda kupanda gari la njombe, narudi shmamba kuangalia maisha mengine. Wasiache kuwa wanamuangalia Janet. Waliliaaaaa. Sikutaka kuwaambia sanaaa. Nikamuaga Janet, nae aliliaaaaa.

Sikutaka mnyalu tuonane nikiwa natoka, cause namjuaaaa, angejifanya yeye msafiii duniani hakunaaa, na hivi heavens zime rule in favor of him, angenitangaza kijiji kizima nataka kumuua na ukimwi, mi malaya mpaka ukimwi umekuja kuniumbua.Namjua angezusha scenario, nikaonaaa kama kuukwaa nisha ukwaaa, ngoja niondoke mwenyewe kabla sijatolewa kimya kimya. Nikam time yuko upande wa pili, nikachomokaaa getini, nikaenda kituoni kungoja gari za ubungo.

Nikiwa kituoni gari zikawa za shida shida, mara namuona yule anakuja na wadogo zangu. Nikakodi boda boda fastaa aniwahishe kabla hawajanifikia, wakaniona, nao wakaodi kunifukuzia. Wakanipata. Mnyalu hakusema lolote zaidi alichukua begi kulirudisha nyumbani. Na mimi nikawa narudi taratibu. Nikaingia chumbani, akafunga chumba, kanifungia mimi. Haaaaaaa! Huo mwanzo tu ndugu msomaji.

Anawapa maelekezo asiruhusiwe kutoka nje ya geti, mmmmh! Nikasema hayaaaa. Usiku akaja sasa, ananiuliza ulikuwa unaenda wapi? Nikajibu kijijini kwetu, kuanza maisha mapya. Akaniuliza kwanini? Kweli unaweza kuondoka after 6 yers together bila kuniaga, no goodbye, no message, nothing, unatoroka, unaacha mtoto, imekuwaje? Nikajitetea tu mi bwana sikutaka kukuweka kwenye wakati mgumu wa kunifukuza, kuninyanyasa, nikajiongeza, sababu mwenzangu mzimaa, na bado nguvu unazo, utahitaji kuoa tena, sasa nikaona nikuachie nafasi yako.

Akaniuliza, wewe toka tumekutana nilishindwa nini kuoaaa, kama ningetaka? Nikajua hana lolote kunipa moyo tu. Akasema kitu kimoja kwa ufasaha sanaa. "MAKE IT EASY FOR PEOPLE TO LIVE WITH YOU" Na mimi sikujibu kitu. Tuakalala kimya kimyaaaa.

Akawa bado anawahi kurudi, na yale ,abadiliko alioonesha akayaendeleza. Hakuwa mkatili wala mnyanyapaaa.Kabisaaa. pia hakuwa boyaaa wala mzembee ile naumendesha thubutuuuuu. Ana ni treat vizuri tu, nikikosea hajali nimeathirika au sijaathirika ananipa makavu kama kawaida.

Tukawa tunaenda kwenye ushauri nasahaaa. Wanasema mnaweza kuendelea na ndoa ikitokea kama sisi mmoja anao, mwingine hanaa. Na nasaha zao. Hamuwezi amini Mnyalu alikuwa tayari kujirisk kufata ule upuuzi, mi ndo nikamgomeaaa, hapa ndoa imekufaaaa. Tendo la ndoa sahau. Siwezi kukua afu mtoto abaki Yatima.oooh wataalamu sijui niani, nikamwambia baba HAPANA.

Our sex life ended ila our relationship grew a lot, ikawa tunaongeaaa vizuri zaidiii, heshima ikawepo sanaa, upendo, na amani kwa wingi. Nikashukuru Mungu kwa kweli. And never didi he even once asked me nimeutoa wapi huu ukimwi. Never.

Sana sana alisisitiza hili ni tatizo letusote, cause if he was there for me, maybe ningehangaika niliko hangaika, kwa hio nae ana mchango sawa sawa na mimi kwenye kuleta hili tatizo, ndo maana hanitupii lawama zozote, ila tushafanya makosa, woteee, tuangalietuna move vipi foward kwa upendo. Yeye kama yeye ata take responsibility 100% kwa yaliotokea.

Sikutegemea kwa kweli kama angekuwa muelewaaa. Na nashukuru Mungu sanaa sanaaaaa.

ITAENDELEA KESHO.
 
Hii ni zaidi ya hatari. Unaweza kuchagua team sasa? Haujachelewa bado ila unaweza ukaliwa kichwa vilevile. Hadi sasa msimamo wa ligi hausomeki kabisaaa. Naona @Lara1 kuna watu anataka kuwapa ushindi wa mezani....

Siza haja kukumbusha Mzee wa kuandaa shows, mpinzani wa gillbert?
 
Back
Top Bottom