Ujio wa msomàli niliutafakari kwa kina sanaaa. Niliuwaza mara 1000 na zote ukibadilika badilika, ila not even once nilipatia ujio wake utakavokuwa. Ujio wa kwanza niliwaza utakuwa kupigiwa simu na migration wa USA kwamba wana m deport baada ya ku overstay. Ujio wa pili nilowaza utakuwa wake tu binafsi baada ya kufilisika na maisha kumla Tigo. Ujio wa 3 nilitegemea utakuwa wa kunifata, kunibembeleza tuoane, tukaishi marekani. Low key na mimi marekani nilikuwa naitamanijeeee. Nichokiwa sikitaki ni mimi kwenda kusgua sugua vyoo sijui kufyeka majani. Nikawaza kama msomalo kapata hata kibarua cha kufyeka poaaa tu, mi naenda kuwa hoise wife. Kwanza mwanangu atapata better education, health system ziko better na mimi niishi American dream kidogo.
Ujio wake ulikiwa tofautiiiii kabisaaa na matarajio yangu. I knew Hussein, my Hussein, nimelala nae kitanda kimoja zaidi ya miaka 2. So namjuaaa sio kumfahamu tu. He will always be the lazy ass bum. Kwanza alinitumia sms, nikaisomaaa sikuelewaa kabisaaa. After all this time and every thing he had a nerve ya kusema "Hello i am back, lets meet for lunch and catch up" Really? No sorry, no nothing! Mxiuuuuuuuuuu! Sikwenda wala sikujibu.
Then he showed up uninvited kwangu, he was not the same Hussein ndugu wasomaji. He was bold with iron balls. Looked me, Me! Sally in the eyes and demanded the baby, as if huyo mtoto alinikabidhia na hela kibaooo kibaoo nimtunzieee. Mmmmmmhhhh! Mtoto huyu huyu wa kushonwa huku chini. Tena mkavuuuuu as if nothing happened. Plus mazarau ya kisomali niloyaonaaa kabisaa. Nikasema hata ile nuktaaa ya nia ya kukusamehe basi leo imefutika rasmi.
Na mimi nikamletea attitude si za nchi hii. Msomali sio peke yake mjini hapa. Tangu hapo yeye mtoto mtoto na yeye. Yale yale ya Dee mtoto unamtaka mama mtoto kama hunioniii. Nyokolostiiiiii. Nafuuu hata angenidanganya nakupenda sanaa, Sally, nimerudi sababi yako, i couldnt live without you. Ila kuonesha kilichomrudisha ni mtoto tu, kiliniumaaaa mpaka kwenye uchi ndugu msomajiii. Mbwa huyu nimemfugaaa miaka na miaka, not even once nilimfanyia ndivo sivo. Hata kama shukrani ya punda ni mateke, teke hilo alilonipa ni la Kiboga, na mguu wote umezama ndaniii. Khaaaaaa! I knew how Pendo felt all this while to be unwanted. Nikapitisha final decision simpi mtoto wala nini akafie mbele.
Huku Dee nae ndo ananitaka, ananitaka mpaka basi. Nusu niko tayari kumkubali kwanza Pendo alinikutaaa, kama kuporwa bwana yeye ndo aliniporaaa na mimi ndo namkomboa bwana wangu mikononi mwake. Isitoshe Msomali ndo hanitaki tenaaa, i am not getting any younger, before i know it sitakiwi kila konaaa, naanza kuloga nipate mabwanaaa. Sikuwa na budi kumkubali Dee sababu anampenda mwanangu afu ni zimwi linijualo haliwezi kunila nikaishaaa.
On the other hand baada ya mimi kuionja labor, naujua uchungu wa mtoto, it didnt seem fair, sababu meli yangu imezama, baba wa mwanangu hanisi, i jump my ghosts kwenye meli ya Pendo na kumpora baba wa mwanae kujiokoa mwenyewe. Every body for himself God for us all. Life was not giving me options here. Nikiwaza Tonny tatizo ni moja no one knows him, he is like a ghost , niliishi nae ila therr was something weird about him. Sikujuaga ni nini but i couldnt trust him 100%.
Nikaamua sababu nataka kumpora Pendo bwana maybe we should have a woman to woman chat! It might look a bit savage ila i had no options, ilibidi tu nimsikie mwenyewe ana yapi ya kusema. Pendo ana matatizo yake ila unafiki anauwezaa. Nimejifungua kaja kuniona mara 3. Sasa sijui kuhakikisha mtoto si mumewe. Birthdayza mwanae lazima anialike na lazima anikumbusheee na kunibembeleza niende. Mwanamke ana roho ngumu yule, mpaka niliwahi kuhisi anataka kuniua nini maana mkinga yule. Heheheeee! Kumbe walaaa.
Nikaenda kwake, nikamkuta mwanae na dada. Akatoka chumbani. Akashangaa leo umekuja kwangu bila sherehe kuna nini? Nikamwambia hamna kitu. Akasema karibuuu. Nikaamchana live, bwana i was thinking kurudiana na Dee what do you think,? Mmmmmh! Savage of me! Akaguna tu, akasema mi hamnishtushiiii, si msharudiana kitambooo, au unamaanisha mnataka kuoana iwe official? Maana sikumbuki kama mliwahi kuachana serious zaidi ya kutuchezesha makida wenzenuuu. Nikasema sio kuoana just get back together. Akasema sawaaaa. Mi sina tatizooo. Nishakubaliana na hali kitambo sanaaa. Mtakavo amuaaa. Ila Dee utamuweza?
Nikastukaaaa! Nitamuweza kivipi? Mmmh akagunaa! Unafikiri wewe peke yako ndo unanipasua kichwa na Dee? Kuna mdada huyo anaitwa Fiona anafanya ubalozi wa Sweeden ni mwanamke wa Dee miaka na miaka tena wana mtoto wa kike, mkubwaa kwa mwanangu. Niki mkadiria alimzaa wakati yuko na wewe. Huyo Fiona ana mumewee na kaolewaaa kabisaaa. Na mumewe anajua mtoto wake ila toto ni Dee mtupu. Mi nakusikitikiaa unanyonyesha unalala na Dee, Dee analala na wanawake wengine, na sio Fiona tuuu, mimi pia vikimpanda ananiomba mechi inabidi nimpe, mi shule sikwendaa, jembe sahivi kushika siwezi navumilia tu nitunzwe na mwanangu. Na kuna mwingine mtoto mdogo mwarabuuu wa kariakoo anaitwa Ilham. Malaya yule mwanaume wewe. Mi alinibemendea mtoto na wewe yule mtoto akitembea shukuru Mungu. Mi nakuhurumia we shoga angu shule umeenda, pesa unayo, ndugu zako wanajiweza unahangaika nini, utakija kupata ukimwi bureee. Bora mimi nitasema umasikini wangu umeniuaaa, mzazi wangu hakunipeleka shule. Wewe je?
Hizi habari zilinichoshaaaa sio kidogoooo. Zilinichoshaaa mnooo. Nilizeeka ghafla. Nikiwa kama mwanamke kamili sikumuuliza kwanza Dee mpaka nikamilishe ushahidi kamili wa kutosha ku convict sababu mwanaume bila kumbana kwenye kona anaruka mashtaka yoote na kupoteza ushahidi na kuji victimise. Niliumiaaa moyo sanaaa. Sasa sikujua kama ya msomali au ya Dee ndo yameniumaaa sanaaa. Nikaanza kumtafuta Fioma Facebook nikampata. She looked happily married. Sikuridhika nikaenda mpka ofisini kupeleleza, kila mtu anasema haiwezekani kuwa hivo, wanapendana na mumewe hakuna mfanooo. Mmmmh.
Nikaanza kumpeleza ilham ni nani? Sikupata jibu. Fiona nilimpa maana nilikagua watu anao wa follow Dee, insta mmoja mmoja na hakuwemo. Ila Facebook nikamkuta. Nikamrequest urafiki na kumpata. Huyu Ilham hata hakuwepooo kokote. Like a ghost. Nikaanza kuiwinda simuuu ya Dee. Haina password. Kaingia kuoga nikazama majina ya I hayumoooo. Nikakakua B kama yumo kama Bae, Baby hamnaaa, nikazama L, labda love au my love, holaaa. Nikakagua phonebook yote jina kwa jina. Hata funny names kama fundi bomba, fundi baskeli, juma transporter nayo hamnaaa. Nikawa holaaaa.
Huku msomali nae anazidi kunipanda kichwaniii, naitwa ustawi wa jamiii kila leo. Hachokiii. Stress zikataka kunimalizaaa kabisaa. Nikiwa kati kati ya stress zangu Winny ndo kuniambia ana mimba ya bro hajui afanyaje, itakuwaje mumewee. Kumbe ndoa mnazipendaaa kuchepuka vipi sasa. Nikawa sina cha kumshauti zaidi ya kumwambia hawezi kujuaaaa. Labda yeye ajistukie, kila mtu anajua Winny mtu wa Mungu no one will even suspect. Nikitamka haya no one will even suspect nikapata mwanga huenda Dee nae malaya kweli kweli and we all dont suspect. Sasa leads zote zinaishia no where.
Likanikabaaa, nikashindwa kuvumiliaaa, nikaamua kumuuliza face to face. Alijiletaaa mwenyeweee, nikaanza kumsomea mashataka yake. Alichonipata kwanza hakustukaaa, wala kutaharuki kwamba nimejuaaa, akasema Pendo ndo kalwambia lazimaaa. Sasa Sally we unaongea na X wangu ambae tumezaa nimemuacha unategemea kweli awe na good things to say about me? Really! Sanasana atakujazaaa ujazike uniache acheze azontooo kwamba kanikomoaaa. Mimi ni msafiii, na hata ningekuwa malaya mtu wa kuujua umalaya wangu sio rahisi awe mke wangu wa zamani. Kwani mi mjingaaa nimuoneshee kwamba nazururaaa. Hizo habari kaaa na kutungaaaa zote, tena katumia watu ambao wapo kwenye maisha yangu wanazagaa zagaaa tu akawavisha uhusika.
Huyo Fiona ni child hood friend wangu, ana mumewe siku nyingi sanaa na wamezaa mtoto mkubwaa. Sasa mke wangu ndo kanipa ubaba. Mxiuuuuuu. Huyo Ilham sijui ni nani, mi sina mazoea na watoto acha wa kiarabuuu. Kwanza sio type zangu Udongo wa Dubai. Kukuhakikishia kwamba sina cha kuficha tumpigie fiona, mi napiga na simu yangu, wewe ongea muulize unachotaka. Nikakomaa piga ndio, if he was calling a blaff ndo angejambaaa. Akapigaaa.
Hapo hapo nikahakikisha hajatuma sms kumstua wala nini. Nikamwambia mimi mwanamke wa Dee, akasema ndio mwanamke wa Dee nakusikiliza, mstaarabu hatari, nikasema inavosemekanaa unatembea na Deee, akauliza mimi? Mimi huyu huyu mke wa mtu, tobaaaa! Sio kweli, mimi na Dee we just friends. Longtime friends, na anaese,a hayo lazima ni pendo na insecurities zake. Nikazuga zuga ya mtoto nikayaacha kapuni. I was comvised, na nikajiona mjingaa kishenzi Pendo kunijazaaa afu nikajaaa.
Nikawa niko tayari kumpa Dee mchezoo hapo hapo mda huo huo. Tukaanza kabisaa foreplay na nini, Akavua nguo kufika boxer tu, Msomali akaibuka kama kachanjiwaaa. Dee akashuka na taulo, mi sikusema kitu. Nasikia tu wanavunja vunja sebule yangu. Sikutokaa maana nilijua nikiyoka naweza kumpiga msomali na kitu kizito nikapata murder case, nikaozea jela, mwanangu akateseka. Nikajifungia tu ndani. Dee anamtoshaaa.
Baadae soo limeisha nakuta sebule haifaiiii. Nikazikuta zile karatasi, bwege anataka mtoto serious kabisaaa, bora Dee alivomuweka mahala pake. Nikaziomaa, nyege zote zilikatikaa. Kila mtu anachosema yule mtoto haki yake, siwezi kumnyimaa. Haki ganiii? Kushonwa papa nishonwe mimi, niteseke afu haki haki gani wanayoizungumza. Nitapambana mpaka mwishoooo. Wasiniletee kabisaa mambo ya kijinga na kisengeremaaa.
Nikamuita mwana sheria wangu tuangalie tunazulumu vipi hizo haki. Nikaanza kwanza kumwambia kwanza sio raia, kafoji passport, ni msomalii wa mogadishuuu, Og. Lawyer akasema hio ibaki siri yetu ukisema mahakamani utajifunga mwenyewe. Mana wewe ndo umemdhamini ilihali ukijua sio raia. Mmmmh balaa. Basi ananiuliza kama najua chochote cha kumdiscredit mahakamani sijui. Lawyer akaniambia hapa ,ama unapotezaaa. Chupi ilinibanaaa. Akasema kama ni hivi bora muongeee tu myamalize. Nikam fire yule lawyer degree yake itakuwa ya chupiii tu, sheria hazijui vizurii. Nikamchukua lawyer wa Dee. Story hio hio. Nikaona wananitania, nikazama Marealle advocates nikavunja bank, nako story hio hio.
Watu wanaongea kiwepesi sababu hawanijui uwezo wangu. Mimi mahakama imempa msomali haki ya kumchukua mwanangu, anaenda kwake na demu wake wa kisomali wanacheza cheza na mwanangu, hapo mi nilishonwa nyuzi zisizo na idadi, kisu juu, kifatacho kwenye hii story nyumba ya msomali na demu wake nimeitia kiberiti na petrol, na niko jelaaa. Jamaniiii, mi usengery sipendagikabisaa. Sio mtu wa kuonewa na kutokuchukia hatua. Ndo maana nilihangaika sanaa kutafuta msaada wa kisheria maana ikishindikana nitaanza kutumia njia zangu nazozijua mwenyewe.
Nikatafuta lawyer mwingine dogo dogo, akaniambia nikumbukee msomali aliniambia nini? Lawyer gaidiii. Dirty lawyer kweli kweli exactly who i needed. Akaniambia tumtafute mdogo wake wa kike, ambae hakiwa na la maana la kusema zaidi ya kumsifu kala yake. Nikamfata mpaka Eva nae hakiwa na la maana. Lawyer kiboko anasema kumbukaaa kumbukaaaa, ikishindikana mtongozeee tena .
Siku nimekaaa ikanijia kichwani wana mdogo wao aliepoteaaa. Nikamshirikisha dogo janja. Akasema hapo Jackpot. Hajapotea, he is running from his familly. Where there is smoke , there is fire. Hii lead ni nzuriii sana. Tumtafute huyo mdogo wao, lazima kuna kitu anakijuaaa. Hata kisipotusaidia mahakamani kitasaidia hata kumblackmail msomali.
Nikamwambia msomali na pesa yotealio nayo kashindwa kumpata, sisi ndo tutampata kweli. Na network yote ya wasomali bado kamkosaa. Mmmmmh! Akasema uwezekano upo, the guy is running from his family not us, tutampata tu. Trust me, mimi ndo dogo Janja. Nikaitikia tuuuu, lakini sikuwa convised.
Tukaanza kumfatilia mdogo wake wa USA, followers wake, wasomali tupu na wanavofanana balaaa. Nikakata tamaaa. Akasema tu focus on birthdays. Yule dada sijui celebrity wa kisomali birthday wish 378 likes 1000 unampataje mtu sasa hapo. Lawyer akasema mdogo wao atakuwa in 20s tufatilie profiles za wanaojirudia kumuwish happy birthday au ku likekwa miaka mi 5. Jamaniii. Nikamuajiri Feisal. Focus ni profile zile empty mtu hapost chochote au, anapost vitu visivoeleweka. Tukapata kama 5, ambazo zimelike mpaka harusi, mpaka mtoto.
Akasema tuhamie kwa Msomali, msomali sio mtu wa social media. Ana post chache sanaa tena za zamani. Ila account kama 2 katika zile zime like post kadhaa. Akasema hawa wa 2 huenda ni mtu mmoja na ndo mdogo wao, au mmoja wao ndo mdogo wao. Tuka create account na kumrequest urafiki. Aka accept.
Tukaanza kuchat chat akasema yupo Rome, nikamdanganya mi nipo Millan. Tunachat tuna chat. Akasema we should meet up. Namjua kwa picha tena akiwa mdogo sanaa. Mara niwaze au sio yeye. Lawyer anasema ni yeye kabisaa. Na kweli nae alisema ana kaka na dada ila walipotezana kwenye vita. Nimemdanganya mimi mwenyewe msomali nimekimbia vita sijui familia yangu ilipo wala nini. Nilimkolezaaaa. Akasema tukutaneee atakuja Millan. Na mimi nipo bongo.
Ikabidi nimwambie Dee ishu yote na kwa mwanangu naenda hata guantanamo acha huko Rome. Dee was supportive sanaa. Tukafanya manuvaaa nikaenda for the meeting. Tulikubaliana kukutana cafe. Nime google hatariiii. Mi nikawahi kufika, Dee akabaki hoteliniii. Nimeenda cafe. Kweli akaja na ni mwenyewe kabisaa, wamefanana kabisaaa. Ile anakaribia kufikaa akapiga uturn.
Mi kuanza kumkimbizaaa, maliq its me, akasema back off, back off, kumbe ni wewe umetumwa Hussein. Umetumwa na kaka yangu hussein. Huku nyuma nasikia Maliq, msauti wa Hussein. Akasema napanda metro mkinifata nawashtaki, i am over 18 hizi nchi za watu. Hamtakiwi kuingilia uhuru wangu. Ikawa baas tenaaa. Hussein aliliaaa. Nilimhurumiaaa ila nilijihurumia zaidiii.
Kurudi bongo nikamfukuza yule lawyer kazi, kauza CD kwa Hussein alipo mdogo wake. Aliapia Miungu yote sio yeye ila nguvu ya pesa naijua vizuriiii. Hessein kashindwa kumpata mdogo wake miaka yote mimi kumpata yeye atokeee sio rahisi. Na tunaojua hili dili ni mimi, lawyer na Dee. Na Dee kumsaidia Hussein ni sawa na jua kuwaka usiku.
ITAENDELEA KESHO.