Who is your man!
Kiukweli mimi Sally nampenda sanaa sanaaa, hakuna mwanamke ntampenda huyu. Sijui kwanini. Ila hasomekiii hasomekiii ndugu msomaji. Pasua kichwaa kweli kweli. Tofauti kabisaaa na wanawake wenzie. Mambo yake anayajua yeye.
Nachompendea kwanza anapenda mikasiii. Hobby yake kabisaaa kupigwa show za kibabe. Sio mpaoa mbembelezaneee. Na mimi miaka yote nammega kiselaaa tu. Sio kwamba napenda kujiseviaaa na kujipigiaa free of charge. Hachukui pesa yangu hata 100. Hataki zawadi hataki nini.
Karibuni nimepanga kabisaaa liwalo na liwe namuoa. Eti hataki kuolewaaa!!!!!? Khaaaaa! Mnaweza jua !asihara kweliii. Afu sio mdogo mseme ana umri mkononi. Yaani hii ni critical case. Kila nikimgusiaaa swala la ndoa lazima liishe na yeye kunitibuaaa
Sally mi nakupenda sanaa sanaaaa! Nakupenda leo, nakupenda keshoo. Kwanini hutaki nikupe heshima unayo stahili? I want the whole world to know i love you to the moon and back! I want you to be my wife, to claim you before the wholeworld you are mine. Sielewi what is holding is back.
Kuspma husomiii useme mwanafunzi. Kazi unafanya business zako uko vizuriii sanaaaa. Kutambulishanaa hutakiii, hakuna unachotakaaaa zaidi ya kupigana miti mimi na wewe basi. Kuzaa hunizaliii. Mi umri umeenda i want more, i need more. Kupendana tunapendana sanaaaa sasa najua kuna kitu kina kuhold back sijajia ni nini but najuaaaa!
Sikia baby D, mimi kuna hustles nazikamilisha sijui kama unanisoma, maisha ni zaidi ya cheti cha ndoa! Upo? Maisha ni zaidi ya last name yako! Maisha ni zaidi ya kuzaa.Mapemaaaa tulivotakana nilikuuliza Utaniwezaaaa?
Ukajitia muelewa sasa naona unataka kunipanda kichwani. Mi bado natafuta maisha. So should you! Kwa maisha gani ulio nayo bwana ya kutaka kuoaaa? Acha kunioa mimi kuoaaa! Kwanza unaishi kwenu, plus maisha wote mi na wewe tunaunga unga tu. We dalali wa vifaa vya ujenzi, mi dalali wa nguo. Hatuna mtaji hatuna ushuzi wowote afu tukazae una akili kweli wewe?
Acha uboyaaa! Mimi Sally maisha nimeyakamiaaa, lazima nitatoka tuuuu! Iwe isiweeee. Hata kama ikibidi nizeeke sina familia wala nini kutoka kimaisha lazimaaa nitokeee. Kitaelewekaaaa. Sasa usinichanganye, mdingi kafogjt sanaa ila sahivi yupo nae mishen town tu.
Mtoto yule Faisal anamshindaaa! Mara kibao sikuku anamtuma huku aje nimnunuliemie nguo. Mara ada aje achukue kwangu, afu nimuongezee na mjukuu juuu. Hivi unanitakia mema kweli. Usitake niseme sanaaa. Mengine siri yeyeamilia
Ndo majibu yeka siku zoote yeye na pesaa, pesa na yeye. Anatafuta pesaa hakuna mfano na hana bahatisasa. Wotehatuna bahati. Tofauti yeye mzee wake ana uwezo uwezo, alikuwaga nao zamani, na anapataga vipesa vya dili za msimuuu. Ila yeye sio mtu wa kichukua pesa kwa Mzee wake. Kaka zake wako poaaa sanaa, sema wameoa familia kama wameolewaaa huko. Hawana msaada nae.
Nikajiongeza kumbembelezaaa! "Sally mi mwanaume nakuoa hivo hivo sishindwi kukulisha wewe na mtoto wangu. Mi mwanaume nitapambanaaaaa! Lets get married, pleaseee!
Akaghunaaa ghuna aflabi ya dharauuuu hiii. Nikaaa kimyaaaa. Ila moyoni nikaamua namuoa hivo hivo kinguvuuuu! Kwanza baba yake musilamu safi afu mzee wake poa sanaaaa! Bado ana mambo flani ya kizungu si baharia yuleee. Mtu safi sanaaa! Navosema mtu safi ndugu msomaji msidhani safi juu juu.
Zamani mi mzee wake nilikiwa namuogopaaa kinomaaaaa! Si najisevia binti yake kiselaaa! Sasa vijana wengii wanapenda kuchat chata nae maskani, wanamualika wanamnunulia kahawa kama hayupo vusy anasimulia story za kibaharia na mambo ya mimeli ya kigiriki. Mambo ya majuuu! Mambo ya dollars! Ku hustle na nini. Inakuwa safi sanaaa.
Nilivoanza kujipigia Sally, ile heshima nikawa namkwepa tuu, si kashakuwa baba mkwe, afu hali yangu ya chini na familia uetu pia siooo. Mzee ashatanguliaaa niko na maza anafanya fanya vibiashara vya ujenzi na mimi ndo na hangaika nae. Sasa yeye ana mtaji mimi sinaaa. Nikawa na ile fear kwamba hatoni approve.
Maana mzee nae nuksiii, qna mjengo, gari zake za maana, ana nyororo lake la shingoni pure gold, mi pete pete ya thamaniii. Havai siku hizi sababu kashika dini sanaa! Ila zamani humkosi na hivo vitu.
Alipitia majaribu saaanaaa! Kwanza mkewe kazqa nje huyo mtoto wa mwisho, mtoto mwarabu kabisaaa! Kwa hio sio siriii. Akasamehe na kuendelea na mkewe. Watu wanamjazaaa wanamjazaaa wapiiii! Anasema mkewe kafanya vile sababu yeye hakuwepo kumtunzaaa, kama ni makosa basi yake yeye mwanaume kuondoka kda mrefuuu angeishi vipi na ashki.
Akamkubali yule mtoto, kitanda hakizai haramuuu. Tukajua ndo mwishooo wa mapito yao. Alivorudi maisha yalikaza katikati hatariiii. Hela ya kula hamnaa. Nje ndo hayupo tenaa. Mkewe ndo ashazoea vibahashaaa. Ikawa mtihaniiii.
Hamad mdogo wa mkewe shemeji mtu, akapata pesa za madini, pesa ndefuuuuu! Akaja kumtafuta dada yake. Dada kiburiii kiburiiii. Uzuri watoto wakubwa kasoro huyo Feisal, wengine wako sekondari. Akaanza kudai talaka yake! Aondoke na mdogo wake Arusha.
Baharia akamnyima talaka, kwamba yeye anampenda sanaa mkewe. Mke akapeleka watoto boarding wote, afu akatoroka na kaka ake Arusha. Kamuacha baharia hana kazi wala kibaruaaaa! Afe njaaa sijui. Maana gari washauzaaa. Vitu kibaooo baki nyumbaaa tu.
Baharia kaanza kwenda sokoni kujichanganya mizigo anabeba, vibarua baruaa anafanyaaa, apate pesa ya kula. Feisal akaugua boarding, akarudishwaaa nyumbani na walimu, maana mama mtu simu kabadilisha kabisaaa! Hapatikaniii namba zote. Akampokeaaa, gharama za hospital sasa. Ndo akaenda kuuza cheni lake nyororo la shingoni kwa wahindi sonara.
Peaa yoote kamuuguza yule mtoto peke yake, Analala kwa mgonjwa hospital, anaamkia vibarua kariakoo sokoni, mchana hospitali, anarudi sokoni, jioni hospitali. Alilazwa karibia miezi 2. Wakatoka kurudi nyumbani.
Sasa kariakoo nyota yake ndo ikangaaa! Anajua kifaransa! Wakongo wakija anaotwa atafsiri kwenye maduka biashara ifanyike, anapewa ujira. Wakongo wakatokea kumuamini sanaaa! Akaanza sasa kuwa dalali wa wakinga. Mizigo anachukua mali kauli, anawauzia wakongo, wakilipa analipa.
Mda si mda akafungua duka kubwa la nguo Congo. Mke ulipita mwaka, hapigi simuuu, hatumi sms, sana sana kaka yake ndo anakuja kulipa ada za watoto. Akamwambia usije tena ada ninayo. Akiulizwa mke wangu yuko wapi? Anafanya nini? Kaolewa tena au vipi hasemiii.
Watoto kwawatoa boarding kuwarudisha day, washakuwa minundaaa hatariii. Hawaambiwiii kitu. Mwenyewe akasalimu amri. Sally ndo kibojo yake. Wale wa kiume walinyooshana maana ikawa ngumi zinapigwaaa, baba mwenyewe bahariaaa. Ngumi ngumi mpaka wakanyooka.
Sally wa kike, afu malezi aliopewa siooo, kumpiga haweziii, Salky mwenyewe mzitooo, kitendo cha mama mtu kuondoka nyumbani kilimuathiri sanaaa! Aliumia aa sanaa. Maana yeye ndo alimuhitaji mama yake kuliko maelezo.Akiguswaa tu anase!a nitaondoka nikuache kamama mama bila kukuaga na hutonipataaa! Dady Monster! Basi baba anakuwa mpoleee!
Wale wakiume wote alifanikiwa kuwapuga stop kwenda kabisani. Warudi dini yake. Ila Sally Jumapili anapelekwa kanisani, na sadaka anampa, kila jumapili nguo mpyaaa. Sally kiboko ya bahariaaa.
Baada ya miaka mi 3 mama yao akarudi tu. Alirudi kama alivoondoka. Mchana, akakuta baharia hayupo. Akaingia ndani kwake kwani ana daiwa. Majirani wakaja kumchunguliaaa kwa mbaliii kama ni yeye au macho yao.
Anajikoshaaa tu, nimerudi tu kulea wanangu, nimeshndwa kuishi bila wanangu, mimi sio mke wa bahari, nq!saidia tu malezi. Moyobi wanasema umezima simu miaka mi 3. Mtoto kafanyiwa operation, baharia kauguzaa kauguzaana wewe usitoke mafichoni. Leo hii ndo iba uchungu sanaaa? Wakawa wanagoja kwa hamu sanaa baharia arudiii. Waone songombingooo! Walishangaa kuna kuchaaa! Hamna hata majibizano.
Siku mpaka siku wako poaaa tu, wakawa wanajua wanalea tuuu, wakashangaa na sehemeji yuleeee mapesaa kaja kukaa hapo hapo kafuliaaa kaishaaa! Ndo kisa cha kurudiii. Tukasem bahariaaaa ni ishu ingineeee.
Alivojua mi ni mkwewe bikawaxa ataleta nomaaaa walaa! Ndo kwanza anafurahiii akiniona mkweee! Mkweee! Ataninunulia sodaa. Hivo yani! Tutazungumzaaa! Nikapanga niseme nae kwamba nataka kumuoa Sally! Nione atanisaidia vipi.
Najua alhamisi anakaaga kijiweni sanaaa! Nikamwambia shida yanguchember,akaniambia tu Sally humuweziiii! Akili yake haijatuliaaa kuanzisha familia. Sally kama mama yake! Hana uamuzi mmoja na akiamua kitu kaamuaa. Atakusumbuaaa sanaaa. Humiwezi wewe, wewe mpole anakuendeshaa. Anatakiwa mwanaume gaidiii ambae kamzidi kila kitu ndo atamuheshimu na itawezekana kumcontrol
Wewe Dee huweziii. Nyie ni Christians mna ndo moja usiipoteze kwa Sally. Sawa unaweza kufanya nae harusi ila huwezi kumuoa. Ndoa ni hali ya utayari wa mwanamke kukupa sapoti,heshima na unyenyekevu wake katika maisha yako. Sasa mwanangu mie yule fighter hatokupa chochote kati ya hivo. Ana mipango yake mingineeee.
Alinimaliza nguvuuuu sanaaa sanaaa. Nikashindwa kuvumiliaaa nikamtumia sms unakubali nikuoe au tuachane? Akajibu TUACHANE kwa herufi kubwa, neno moja tuuuu, just like that! Niliumiaaaa sanaa sanaaaa!
Bikiwa najipanga kwenda kumuomba msamaha maana maumivu ya moyo hayapoi kwa ganzi, bikawa nasikia sikia Sally anaonekana na Boy mpya wa kishuaaa hatari. Ana Escudo. Sikuamini mpaka nilipoona mwenyeweeee. Nikaumia mara laki 8 ya mwanzooo. Chakula hakishukiii. Nilikondaaa.
Nikaanzisha mahisiano na mdada anaitwa Pendo, muuza hardware tu, ya kupunguza stress. Kiukwelihuyu Pendo simpendi wala sijawahi kumpendaaa. Alikuwa ananitumia sms kwamba kabielewa kanipendaaa na nini. Na sio Kinondoni tunapokaaa, huku Bugurunii kazini kwangu. Sio hata mwabamke elekezi basi tu kipoozeo xha nafsi.
Moyo badoo unaumaaa! Dar naiona ndogooo! Ikipita Escudo miguu inaisha nguvu nakaa kwanza. Nilimueleza Pendo kila kitu akawa muelewa ananipa moyo, ananionesha mapenzi hatariii. Kidogo alinipa faraja sanaaa. Still kukaa Dar nikaona nasafocate bado.
Pendo akaniambia Congo, Kinshasa building materials ni dili sanaaa. Sanaaa! Kamsikia boss wake anaongea na wazaire. Nilikuwa na million 3 tu ya akiba, asubuhi nikamuaga mama naenda Zaire, akajua masihara akase!a wasalimie.
Kila siku namtania naenda Zaire anacheka. Nikafatilia passport nikapata. Nikapanga mishe za safari, sikuaga mtu. Mpaka nipo kwenye bus nikamwambia Mama mi naenda Zaire serious. Akanisihii nirudiii kuna vitaaa ndo ikawa imetokaaa. Nikampigia na Pendo, alisikitika ila akasisitiza nisi msahau kabisaaa.
Kama mnadhani nilitoka basi mrudi shule mkajifunze kudhaniaaa upyaaaa! Kufika tu Kinshasa nikatapeliwa million 3 zoteeee na simu na kibegi changu. Nikawa alostooo, nchi ya watu, tena Africa nchi yenyewe, sina mia, sina passport, sina chochote, Namba ya mama na Pendo ninazo kichwani, nawaambiaje sasa kwamba maisha yamenila Tigo.
ITAENDELEA KESHO SAA 4 USIKU