Weekend Story! Glory Be To God!

Weekend Story! Glory Be To God!

Infidelity addiction!

Habari za sally zilinisikitisha sanaaa! Zilimsikitisha kila mtu kwa kweli, hakuna hata mtu mmoja aliefurahia sijui lakini ila kwa haraka haraka yule mtoto alikuja na huzuni nyingi sanaaa. Ila toto zuriiii, nenee hiloooo. Toto la kisomali, zuriiii kweli kweli. Kila mtoto ni mzuri ila hili lilikuwa toto haswaaa. Mama yake alishonwa sababu mtoto alikuwa mnene sana na mzitooo. Afu misuli yake ya chini dhaifuuu. Na hapo ni hela ndefu aliweka hospital.

Binafsi niliumia cause Sally was agood friend, japo ananikuwadia kuwadia kaka yake she is a nice person and we have history. Roho ilinichomokaaaa sio kidogo. Afterall Tonny alivojiongezaa, na Tonny mshikaji wetu tukawa tumempa moyo ajiongezeee, mimi ndo kocha wake. Nimezaa watoto wa 3 na siwafichi mume wangu alikuwa boya tu kuna mambo nahitaji anifanyie hafanyi, so sikutaka Sally nae apate mateso yangu namwambia Tonny fanya A,B,C it will work out.

Nilimjaza mtoto ni wako, msomali kaka nae mda bila bila wewe kupita tu ndo mimba itokeee, lazima wewe ni baba. Basi anajitahidiiii mbayaaaa. Jinsi dunia ilivokuja kutula kiboga bila KY wala mate hamna anejua. Tukabakia tu kujiuliza but WHY.? Haisaidiiii kitu ndo tushaliwa ndogo sie tena na maishaaaa. Pale hospital sijui Tonny alipataje taarifa , maana alivo mamas boy mama mtu alishachoka kungoja Tonny aoe, haoiiii, walau hata kimjukuu nacho holaaa. Mama wa watu kaja na mwae hospital sasa sijui nani alimuongoza mwenzie njia ya kurudi nyumbani.

Mi niko na mume wangu sebleni naona Tonny gari ya Tonny inapaki kwetu. Nikakimbilia chumbani na kumwambia baba wa 3 mwambie sipooo. I cant deal na yeye mda huu kwa kweli. Niko nasikilizaaa, baba wa 3, anajikakamua kumuangalia tonny usoni kumdanganya Winny kaitwa kwao alfajiri leo ndo kaendaaa. Sasa mwanangu Traves yupo hapo sebleni anasikia, asiingilie, Babaaa mama yupo chumbaniiii, kaingi sasa hivi. Hahaaaaaa! Baba yake anazuga mda ule aliondoka wewe ulikuwa unachezaaa nje, Traves anakomaaa yupo chumbaniii, nimemuonaaa, anakuja chumbani mamaaaa maaaa! Baba mtu anamwambia nitakupiga Traves akaingia ndani chumbani huyu huku mama nimempataaa. Si nilisema mama yupo chumbaniii. Mxiuuuuuu!

Huku baba Traves ikabidi tu aseme makubwaaa ya jongo, itakuwa karudi sijamuonaaa. Kumbe mke wangu ulirudiii, mi sijajua namwambia Tonny haupo, vipi huko nyumbani bi mkubwa anasemaje. Ile kuzugaaa tu, ila Tonny mtu mzima ashajua mchezo wote kama namkimbia na mume wangu ndo accomplice wangu. Akaaga tu bila kusema alichotaka kusemaaa. Tukabakia na mume tunacheka tu kwa aibu.

Baadae mi na Tonny tukakaa chini kuangalia plan B twende vipi. Tonny akasema yeye mtoto sio shida kama Sally akikubali. Sasa sally haaminiki, kama kujitoa Tonny ashajitoa vya kutoshaaa jamani.khaaaa. Nikaanza kumkatisha tamaaa, washazaa wale mahawara hawaachani wanapeana likizo tu isio na malipo ila wazazi ndo kabisaaa mtoto ni link mbaya sanaaa. Sikushauriii.

Nachomekea kwanini usitoke na Jolline, mbona mzuriiii tu na anahamasishaaa. Nahisi Tonny hakumpenda jolline. Namwambia try to get to know her, you might click who knows? Ila Sally sio achana nae kabisaaa. It was not meant to be. Mimi nasema hivooo ujue basiiii. Angangania why? Kwani kuzaa ni nini dear mbona kwangu sio ishu si na mimi atanizalia. Nikakomaa sasa kumpigia chapuo Jolline.

Huku na huku Betina shoga ake Sally akawa shoga anguuu wa hajaaa. Shoga kuliko hata sally. Of lately Sally alikuwa kavurugwaaa, she was mean and rude. Afu analeaa na hayupo in mood. Naona msalaba wake alitaka kutubebesha. Anamuona kila mtu mbaya kwake au anahusika na yalio mtokea kwa namna moja au nyingine.

Tukawa mda mwingi tuna spend na betina, ambao sisi wake za watu outing zetu na watoto, na waume zetu hivooo. Mambo ya kibibi. Ndo kuanza sasa kupeana ubuyuuu mpaka nikamwambia nacheat na X wangu. Mmmh alishangaaa sanaa. Akaniambia acha mara moja huo upuuzi tena shukuru Mungu hujabambwa. Basi namuelewesha njaa ndo inasababisha hayooo. Ananitukanaaa njaa gani.

Ananisimulia mumewe aliachishwa TBL kazi yuko mwaka wa 4 nyumbaniii. Anamlisha na kumvishaaa kila kitu na haoni shidaa kabisaaa. Nikagunaaaaa tu, moyoni najisemea huo sasa ndo ufaler maana sio ufa la wa kiswahili. Hehheeeeee! Mniacheeee. Nikajua kwanza muongo ukute mumewe sawa kazi hana ana madili kibaooo ananipotezaa tu. Watu hawaaminiki.

Kadri navokaa nae najua kumbe kweliii mwenzanguu ndo iko hivo tena mumewe anasifi mke wangu jembeee sanaaa. Mbele za watu. Nikashangaaa tu ila alikuwa bado hajanishawishiii. Anaendelea kuniambia kwani hizo shida mlizokuwa nazo mwanzo yeye alikuwa hazipati? Useme labda yeye anakula bata nyie mnateseka? Mkila mchicha na yeye si anakula huo huo? Mkiishi pabaya na yeye si analala humo usiku sasa kwanini umlaumu kwamba iko hivo wakati sio enterly his doing ni maisha tu.

Akasema tena shukuru hata hayo maishaaa. Mume umepataa shogaaa. Wanaume hawawezi shurba si unaona msomali kakimbiaaa? Kwani unadhani mumeo anavokaa ana ngaa sharubu hapewi michongo ya kwenda USA au Dubai kujipooza kidogo na maishaaa? Anapata kibaooo. Sema nini michongo ile hutakiwi kuwa na familiaaa. Ila yeye kaamua kilicho bora hata kama mtakula mawe Famililah! Mradi yuko na wewe mkewe na wanae kila siku anawaonenii anamshukuru Mungu wake. Huo sasa ndo upendo wa kweli sio mali.

Mmmmmh! Kidogo alianza kunishawishiii nikaanza majaribio ya kuachana na ule mchepuko wangu mkuu kaka ake Sally na michepuko saidiziii kama mi 2 hivi. Si mnajua ukishaonja nyama ya mtu basi huachiii kula, ndo kuonja kuchepuka nikajikuta nishafikisha ma bwana wa 3. Nikaachana na wa 2 kwanza hilo kubwa lao lilihitaji maamuzi magumu.

Safari ya china ikawa imefika, na ndo tunakutana kubwa alo huko, nikasema ngoja kwanza anipe mahela mengi ninunue mzigo mpaka niridhikeee ndo namtemaaa. Siwezi kumtemaa kizembe hivii hiviii. Bahati kama hizi haziji mara 2. Tukapanga kukutana Hongkong tufanye yetu kwa raha zetu. Mume ndo kanipeleka airport kwa moyo mmoja anajua wife anapambana na hali yetu, kumbe mapambano ni kwa njia za kikomandooo.

Nimepanda business class, emirates, nikawaza hivi Winni mimi huyuu huyuu nakaa business leo? Loooooh! Kweli haramu tamuuu. Nitaweza kweli kuliacha hili bwana languuu na ma business class haya. Mungu nisaidie. Dubai kulala hotel si mnajua mambo ya businesss hakuna kupigwa baridi airport. Nimefikaa najiandaa kwenda hotel sasa nikajipumzishe, nimelipiwa mpaka tour ya mjini, jamani haramu tamuuu.

Nikiwa kwenye 5 star emirates hotel si nikamuona shubhamiiit mmoja, nae yuko hapo, hapooo kumbe. Tena sikumjua nikajua namfananishaaa. Najiuliza ndio au sieeee. Kawa mzuriii mara miaaa maluuni yule. Shoga etu anateseka kumbe senge linakula maisha Dubai. Nikaamua ngoja niliconfront kama silo lenyewe Mungu atanisaidia. Nikaliita Huseniiii ya kiswahili kabisaa sio Hussein ya kiarabu. Akashtukaa akageuka akanionaa, liko Winny! Linakuja linataka kunikumbatiaaa.

Nikamwambia huna hayaaaaa, msengerema wewe. Anashangaa kwani tuna ugomvi, ndio tuna ugomvi kumuacha Sally namna ile ndo nini? Anajibaraguza its complicated. Nikamuuliza na toto lako la kisomali Mungu anavojua kukuchoma duniani toto limekufanana mpaka minywele yenu inayoteleza kama vuzi za mzungu. Akashangaa mtoto? Sally ndo kakudanganya? Mi sio baba yake. Alinitia hasiraaa, ingekuwa sio nchi ya watu ningemkunjaaaa zaidi ya betina alivomkunja michael na mchepuko wake. Basi tuuuu.

Nikamwambia hayaaa, kaendelee na usengery uliokuwa unafanyaaa. Akaondokaaa. Akarudiii mtoto kazaa lini. Sikutaka hata kumjibuuu ashanitoka rohoni jumla jumlaaa. Kajiongeleshaaa mimi walaa simjibu, nikasem huyu mbwa kumbe mkatili alikuwa anajifanya humble sababu hakuwa na hela kipindi kile mafaaan kabisaaa. Nikaingia room kwangu na kuloki. Kesho Msomali huyu hapa na maswali kibaooo, nikamwambia sikia wewe kuku, ushasema mtoto sio wako, basi maswali ya nini? Atapewa baba mwingine. Naomba tusibanane, sikujui sijawahi kukujua na wala hapa sijakuonaaa. Tufanye hatujaonaaa tangu utoke Dar. Nikamuacha anahangaika kama anataka kutagaaa.

ITAENDELEA KESHO.
 
Back
Top Bottom